Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Kinachotarajiwa kutoka kwa wageni

  Tunatarajia wageni wetu watekeleze viwango fulani na kuwajali na kuwaheshimu Wenyeji wao, majirani wa Wenyeji na wanajumuiya wengine wowote ambao wanaweza kukutana nao.

  Kile ambacho haturuhusu

  • Kudharau jumuiya jirani: Wakati wa ukaaji wao au tukio, wageni lazima waheshimu jumuiya jirani na sheria zake. Hii ni pamoja na lakini si tu: saa zilizotengwa za kukaa kimya, maeneo ya kuegesha na saa, idadi ya magari yanayoruhusiwa na utupaji sahihi wa takataka na uchafu katika maeneo yaliyotengwa.
  • Kutoheshimu makubaliano ya nafasi iliyowekwa: Wageni lazima watii viwango vilivyowekwa na Wenyeji kwa ajili ya kila nafasi iliyowekwa maadamu viwango hivyo havikinzani na sera za Airbnb. Hii ni pamoja na lakini si tu: nyakati za kuingia na kutoka, idadi ya wageni, ruhusa kwa ajili ya wanyama vipenzi au uvutaji sigara na sheria nyingine za Wenyeji mlizokubaliana nazo wakati wa kuweka nafasi.
  • Kutoheshimu sehemu: Wageni hawapaswi kuacha eneo walilokaa au uwanja wake katika hali ambayo inahitaji kufanyiwa usafi mkubwa mno au wa kina au ukarabati unaozidi hali ya kawaida ya uchakavu. Ada za usafi zimekusudiwa tu kulipia gharama ya usafi wa kawaida unaofanywa baada ya mgeni kuondoka na kabla ya mwingine kuingia. Wageni wanapaswa pia kurudisha funguo zozote kama wahusika wote wawili walivyokubaliana.
  • Kuchakura vifaa vya usalama: Wageni hawapaswi kukata au vinginevyo kuficha vifaa vyovyote vya usalama vinavyoruhusiwa na ambavyo vimefichuliwa ifaavyo.
  • Ufikiaji wa mali binafsi ambayo si yako: Wageni hawapaswi kuingia kwenye maeneo yoyote ambayo yameonyeshwa wazi kwamba usiingie, yaliyofungwa au yaliyo na taarifa binafsi au ya siri.

  Jifunze zaidi kuhusu Sera ya Karamu na Hafla na Viwango vya Uaminifu wa Wageni.

  Tupo hapa kukusaidia

  Ikiwa unashuhudia au unapitia uzoefu wa tabia ambayo inakwenda kinyume cha sera zetu, tafadhali tujulishe.

  Ingawa miongozo hii haijumuishi kila hali inayowezekana, imebuniwa ili kutoa mwongozo wa jumla kuhusu sera za jumuiya ya Airbnb.

  Ulipata msaada uliohitaji?

  Makala yanayohusiana