Masharti ya kisheria
Kukaribisha wageni wenye mahitaji ya ufikiaji
Kukaribisha wageni wenye mahitaji ya ufikiaji
Tunakaribisha na kusaidia watu wenye mahitaji ya ufikiaji. Wanajumuiya wetu wanapaswa kuamini kwamba Wenyeji wao watatoa taarifa sahihi kuhusu vipengele vinavyohusiana na ufikiaji.
Kile tunachoruhusu
- Msamaha kwa wanyama wa usaidizi kwa ajili ya afya au usalama wa Mwenyeji: Ikiwa Mwenyeji hawezi kukubali wanyama wa usaidizi kwa sababu kama vile kwamba mnyama huyo anaweza kuwa tishio la moja kwa moja kwa afya na usalama wa mkazi wa kudumu kwenye nyumba yake, Wenyeji wanaweza kupewa msamaha ikiwa watatujulisha kabla.
- Maombi ya kuondoa wanyama wa usaidizi ambao hawadhibitiwi na mtunzaji wao: Ikiwa mnyama wa usaidizi wa mgeni hadhibitiwi na mgeni huyo, Wenyeji wanaweza kuomba kuondolewa kwa mnyama huyo. Kwa mfano, ikiwa mnyama huyo ameachwa bila uangalizi wakati wa ukaaji au hajafunzwa kwenda choo.
Kile ambacho haturuhusu
- Kukataa nafasi iliyowekwa kwa sababu ya mahitaji ya ufikiaji ya mgeni: Isipokuwa kuwe na msamaha uliodhinishwa, Wenyeji hawawezi kukataa, kughairi au vinginevyo kubadilisha nafasi iliyowekwa kwa sababu mgeni ana mnyama wa usaidizi au kifaa cha usaidizi.
- Kuongeza ada kwa sababu ya mahitaji ya ufikiaji ya mgeni: Wenyeji hawapaswi kutoza ada ya ziada kwa ajili ya wanyama wa usaidizi au vifaa vya usaidizi.
- Kukataa maombi yanayofaa kutoka kwa wageni ya kutosheleza mahitaji ya ufikiaji: Wenyeji wanapaswa kukubali maombi yanayofaa ya makazi yenye ufikiaji. Ni jambo linalofaa kumwomba Mwenyeji aondoe sofa lake kutoka kwenye mlango ili mgeni anayetumia kiti cha magurudumu aingie vizuri sebuleni (iwapo kuna nafasi ya kusogeza sofa hilo na iwapo Mwenyeji ana uwezo wa kusogeza sofa). Hata hivyo, si jambo linalofaa kumwomba Mwenyeji apanue mlango wa nyumba yake ili kuweza kutoshea kiti cha magurudumu.
- Kutendewa bila usawa: Isipokuwa kuwe na msamaha ulioidhinishwa, Wenyeji wanapaswa kuwatendea wageni wote kwa usawa kuhusiana na sheria na tabia, bila kujali mahitaji yao ya ufikiaji.
- Matusi: Mtu yeyote, awe mgeni au Mwenyeji, hapaswi kurushiwa matusi kwa msingi wa ulemavu wake—ikiwemo kudharau huduma ambayo mnyama wake wa usaidizi au kifaa chake cha usaidizi kinatoa au kutumia maneno mengine yoyote ya kibaguzi.
- Upotoshaji wa vipengele vya ufikiaji: Matangazo lazima yajumuishe taarifa sahihi kuhusu vipengele vya ufikiaji vilivyopo kwenye sehemu hiyo na eneo linaloizunguka. Wenyeji wanapaswa kuwa wazi na kujadili maelezo yanayohusiana na ufikiaji ndani ya utungo wa ujumbe na mgeni yeyote aliye na mahitaji ya ufikiaji yanayojulikana.
Tuko hapa kukusaidia
Ikiwa unashuhudia au unapitia uzoefu wa tabia ambayo inakwenda kinyume cha sera zetu, tafadhali tujulishe.
Ingawa miongozo hii haijumuishi kila hali inayowezekana, imebuniwa ili kutoa mwongozo wa jumla kuhusu sera za jumuiya ya Airbnb.
Makala yanayohusiana
- Mgeni
Wanyama hatari
Tafuta sheria kwa wenyeji kuhusu kufuga wanyama hatari. Jinsi Airbnb inavyosaidia ufikiaji
Pata kujua tunachofanya ili kufanya iwe rahisi kwa watu wenye ulemavu na mahitaji mengine ya ufikiaji kusafiri kwenye Airbnb na jinsi tunavy…- Mgeni
Sera ya Ufikiaji
Jumuiya yetu imejengwa juu ya kanuni za ujumuishaji, kujisikia nyumbani na heshima, ambayo inajumuisha kukaribisha na kusaidia watu wenye ul…
Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili