Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Kuingiliana kwa uaminifu

  Hakuna mtu yeyote anayepaswa kujipotosha au kupotosha nia zake wakati akitumia Airbnb.

  Kile tunachoruhusu

  • Utambulisho wa biashara: Ikiwa ulijiunga na Airbnb kama biashara au kampuni, utahitajika kuthibitisha kitambulisho chako cha biashara, anwani na nambari ya simu.
  • Orodha ya hesabu wakilishi: Tunawaruhusu Wenyeji kutangaza vyumba vingi chini ya tangazo moja la "uwakilishi" katika nyakati ambapo vyumba vinafanana vya kutosha kiasi cha kuzingatiwa kuwa vibadala (kwa mfano, katika hoteli au fleti zilizowekewa huduma). Hata hivyo, vyumba hivi lazima viwe na vistawishi, mipangilio ya vitanda, ukubwa, mapambo na anwani sawa.

  Kile ambacho haturuhusu

  • Upotoshaji wa utambulisho: Unapothibitisha utambulisho wako kama mmiliki wa akaunti, taarifa zote zilizowasilishwa lazima ziwe za kweli na sahihi. Nyaraka za uwongo au ghushi haziruhusiwi.
  • Kishawishi cha malazi na kubadilisha: Mwenyeji hapaswi kuwapotosha wageni kwa kutoa sehemu ya kukaa ambayo ni tofauti sana na makazi halisi ambamo wageni watakaa, hata kama anwani ni ile ile.
  • Maombi ya malipo ya ziada yasiyotarajiwa: Wenyeji hawapaswi kuomba malipo ya ziada ambayo hapo awali hayakutolewa mapema na Airbnb au kukubaliwa na mgeni kabla ya kuweka nafasi.
  • Ripoti na madai ya uwongo: Wakati wa kuwasilisha madai au kuripoti tukio lolote kwa Airbnb, lazima utoe taarifa ya kweli na sahihi.
  • Unyang’anyi: Kutumia vitisho vya moja kwa moja au visivyo vya moja kwa moja ili kupata kitu kutoka kwa mtu mwingine hakuna nafasi katika jumuiya yetu.
  • Kutumia Airbnb vibaya au kwa hila: Hakuna mtu anayepaswa kutumia lugha ya matusi, mbinu za hila au kutoa vitisho (vya vurugu au visivyo vya vurugu) wakati wa kuwasiliana na Airbnb au mmoja wa wawakilishi wetu.

  Tuko hapa kukusaidia

  Ikiwa unashuhudia au unapitia uzoefu wa tabia ambayo inakwenda kinyume cha sera zetu, tafadhali tujulishe.

  Ingawa miongozo hii haijumuishi kila hali inayowezekana, imebuniwa ili kutoa mwongozo wa jumla kwa sera za jumuiya ya Airbnb.

  Ulipata msaada uliohitaji?

  Makala yanayohusiana