Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Nani anaweza kuwa na akaunti ya Airbnb

  Watu ambao hutishia au kuhatarisha wengine hawana nafasi katika jumuiya yetu.

  Tunachoruhusu

  • Uthibitishaji mbadala: Tunaelewa kwamba si wanajumuiya wote wanaoweza kutoa picha ambazo zinalingana na kitambulisho chao kwa sababu mbalimbali. Katika visa hivi, tunakuomba uwasiliane nasi ili tuweze kukusaidia kukamilisha njia mbadala ya uthibitishaji.

  Kile ambacho haturuhusu

  • Upotoshaji wa utambulisho au kutolingana: Akaunti zinapaswa kuwakilisha kwa usahihi muundaji wa akaunti na kutoa taarifa, picha au hati zinazolingana na utambulisho wa mtu huyo.
  • Watumiaji wenye umri mdogo: Watu walio chini ya umri wa miaka 18 hawaruhusiwi kuunda akaunti ya Airbnb au kuweka nafasi. Katika sehemu ya kukaa au kwenye Tukio, lazima waandamane na mtu mzima.
  • Makosa fulani yanayopatikana baada ya kuchunguza historia ya mtu (Marekani pekee): Uchunguzi wa historia ya mtu unaweza kufanywa kwa watumiaji ili kutambua kama walihukumiwa. Tunafanya uchunguzi ili kutambua nyakati ambapo walihukumiwa kwa ajili ya makosa mahususi ambayo yanaweza kuonyesha kuongezeka kwa hatari ya usalama katika jumuiya yetu na tunautumia kuamua wakati ambapo watu waliopatikana na hatia fulani huenda wasiruhusiwe kutumia tovuti yetu.

  Kushirikiana na kundi hatari: Watu wanaoshirikiana na makundi yenye msimamo mkali, makundi ya chuki na makundi ya uhalifu uliopangwa hawaruhusiwi kuwa na akaunti kwenye Airbnb.

  Tuko hapa kukusaidia

  Ikiwa unashuhudia au unapitia tabia ambayo inakwenda kinyume na sera zetu, tafadhali tujulishe.

  Ingawa miongozo hii haijumuishi kila hali inayowezekana, imebuniwa ili kutoa mwongozo wa jumla kwa sera za jumuiya ya Airbnb.

  Ulipata msaada uliohitaji?

  Makala yanayohusiana