Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Je, Sera ya Sababu Zisizozuilika inatumika kwenye nafasi niliyoweka wakati wa janga la COVID-19?

  Kidokezi: Lazima ukidhi masharti fulani ya kughairi chini ya Sera yetu ya Sababu Zisizozuilika, lakini unaweza kughairi wakati wowote kulingana na sera ya kughairi ya mwenyeji wako. Unapotafuta maeneo ya kukaa, tumia kichujio cha Kughairi kunakoweza kubadilika ili kusaidia kuchagua ukaaji unaokufaa zaidi.

  Makala yetu rasmi ya inaeleza kwa kina jinsi sera ya sababu zisizozuilika inavyotumika kwenye kughairi kwa sababu ya COVID-19

  Huu hapa ni muhtasari wa kukusaidia kujua ikiwa nafasi uliyoweka inastahiki.

  Nafasi uliyoweka inastahiki ikiwa yote yafuatayo ni sahihi

  • Umeweka nafasi mnamo au kabla ya tarehe 14 Machi, 2020
   • na tarehe ya kuingia ni ndani ya siku 45 kuanzia leo
   • na bado hujaghairi
   • na bado hujaingia
   • na janga la ugonjwa linakuzuia kukamilisha nafasi uliyoweka

  Ikiwa mambo hayo yote ni kweli, unaweza kuighairi wewe mwenyewe na utapewa machaguo ya kughairi na kurejeshewa fedha wakati wa mchakato huo. Ili kughairi chini ya sera hiyo, utahitaji kutoa hati au kuthibitisha kuwa huwezi kukamilisha safari yako kwa sababu ya COVID-19.

  Kumbuka: Ikiwa unaugua COVID-19, unaweza kughairi chini ya sera hiyo bila kujali maelezo ya nafasi uliyoweka kwa kuwasiliana na timu yetu ya usaidizi wa jumuiya. Utaombwa kuthibitisha hali hii kwa nyaraka.

  Nafasi uliyoweka haistahiki ikiwa unaghairi kwa sababu ya COVID-19 na ikiwa yoyote kati ya mambo yafuatayo ni kweli

  • Iliwekwa baada ya tarehe 14 Machi, 2020 au
  • Tarehe ya kuingia ni zaidi ya siku 45 kuanzia leo au
  • Ilikuwa tayari imeghairiwa au
  • Tayari umeingia

  Ikiwa hustahiki na ukaghairi, fedha utakazorejeshewa zitaamuliwa na sera ya kughairi ya mwenyeji wako, nasi tutaonyesha kiasi cha fedha utakazorejeshewa kabla hujathibitisha kughairi. Katika hali hii, malipo ya wenyeji na malipo yanayorejeshwa kwa wageni yanatolewa kulingana na sera ya kughairi ya mwenyeji uliyokubali wakati ulipoweka nafasi.

  Kumbuka: Nafasi iliyowekwa inapoghairiwa, Airbnb hutoa malipo yoyote ambayo mwenyeji anastahili na malipo yoyote ambayo mgeni anapaswa kurejeshewa kulingana na sera ya kughairi ya mwenyeji. Kwa sababu hiyo, nafasi zilizoghairiwa kabla ya mpango huo kutangazwa au kupanuliwa hazitafikiriwa tena.

  Machaguo ya ziada ikiwa nafasi uliyoweka haistahiki

  Ikiwa mipango yako inaweza kubadilika, unaweza kufikiria kushirikiana na mwenyeji wako ilikubadilisha nafasi uliyoweka kwenda kwenye tarehe ya baadaye.

  Unaweza pia kuwasiliana na mwenyeji wako ili kuomba kurejeshewa fedha za ziada, naye akikubali, anaweza kutumia Kituo cha Usuluhishi ili kukutumia pesa kwa njia salama.

  Kumbuka kuwa sera tofauti zinatumika kwenye nafasi zilizowekwa za ndani nchini China bara na kwenye nafasi za Luxe au Luxury Retreats.

  Ulipata msaada uliohitaji?

  Makala yanayohusiana