Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Mchakato wa hatua 5 wa Airbnb wa kufanya usafi wa kina

  Mchakato wa hatua 5 wa kufanya usafi ni mkusanyo wa mazoea ya kufanya usafi ambayo Wenyeji wote wanahitajiwa kufuata baada ya mgeni kuondoka na kabla ya mwingine kuingia, pamoja na kufuata sheria na miongozo ya eneo lao.

  Hatua ya 1: Jitayarishe

  Matayarisho mazuri yanaweza kukusaidia wewe pamoja na timu yako kufanya usafi kwa ufanisi na usalama zaidi. Hakikisha:

  • Pitisha hewa safi kwenye sehemu hiyo kabla na wakati wa kufanya usafi, pale inapowezekana
  • Tumia dawa za kuua viini zilizoidhinishwa na wakala wa udhibiti wa eneo lako kwa ajili ya matumizi dhidi ya COVID-19
  • Daima soma kwa uangalifu maelekezo na maonyo yaliyo kwenye bidhaa zako za kufanya usafi
  • Nawa mikono yako au uitie dawa ya kuua viini

  Hatua ya 2: Safisha

  Kusafisha ni wakati unapoondoa vumbi na uchafu kwenye sehemu mbalimbali, kama vile sakafu na sehemu za juu za kaunta. Hakikisha:

  • Unafagia, unavuta vumbi na/au kupiga deki kwenye maeneo kabla ya kutakasa
  • Safisha vyombo na nguo kwa kutumia joto la juu zaidi linalowezekana
  • Unapangusa sehemu ngumu kwa sabuni na maji

  Hatua ya 3: Takasa

  Kutakasa ni wakati unatumia kemikali kupunguza idadi ya bakteria zilizo kwenye sehemu kama vile vitasa vya milango na rimoti za televisheni. Hakikisha:

  • Unanyunyizia sehemu zinazoguswa mara nyingi katika kila chumba kwa kutumia dawa ya kuua viini iliyoidhinishwa
  • Iache dawa ya kuua viini ibaki kwa muda uliowekwa kwenye kibandiko cha bidhaa hiyo
  • Iache sehemu hiyo ikaushwe kwa hewa

  Hatua ya 4: Hakiki

  Ili kupata orodha kaguzi mahususi za kufanya usafi, nenda kwenye Vidokezi > Kufanya usafi. Hakikisha:

  • Rejelea mazoea bora katika kila orodha kaguzi ya chumba kwa chumba ili kuhakikisha kwamba maeneo yote yamesafishwa na kutakaswa baada ya kila ukaaji
  • Shiriki mazoea haya bora na timu yako ya kukaribisha wageni na wataalamu wa kufanya usafi

  Hatua ya 5: Andaa upya

  Ili kusaidia kuzuia maambukizi ya kuenea, ni muhimu ukamilishe kusafisha na kutakasa chumba kabla ya kubadilisha vifaa kwa ajili ya mgeni anayefuata. Hakikisha:

  • Unanawa mikono yako kabla ya kubadilisha vifaa vya wageni, vitambaa na vifaa vya kufanya usafi
  • Unaondoa kwa njia salama au kusafisha vifaa vya usafi na vifaa vya kujikinga
  • Usiingie tena kwenye chumba baada ya kutakaswa
  • Unasafisha vifaa vyako baada ya mgeni kuondoka na kabla ya mwingine kuingia

  Mchakato huu unategemea kitabu cha mwongozo wa kufanya usafi cha Airbnb, ambacho kilitengenezwa kwa kushauriana na wataalamu katika tasnia za usafi na dawa.

  Ukiwa kwenye akaunti yako, unaweza kwenda kwenye Vidokezi > Kufanya usafi ili kupakua kitabu kizima cha mwongozo wa kufanya usafi na upate nyenzo zaidi, mafunzo na orodha kaguzi mahususi za kufanya usafi.

  Kuahidi kufuata mchakato wa kufanya usafi wa kina kunahitajika kwa matangazo yote

  Wenyeji ambao hawatakubali mazoea ya usalama ya COVID-19, ikiwemo mchakato wa hatua 5 wa kufanya usafi wa kina, huenda wasiweze kukubali nafasi mpya zinazowekwa.

  Mazoea haya yanahitaji uvaaji wa barakoa na kuepuka mikusanyiko unapohitajika kufanya hivyo na sheria au miongozo ya eneo husika na kufuata mchakato wa hatua 5 wa kufanya usafi wa kina. Wenyeji ambao wanakiuka mara kwa mara au kwa kiasi kikubwa viwango vya kufanya usafi wanaweza kupewa maonyo, kusimamishwa na wakati mwingine, kuondolewa kwenye tovuti ya Airbnb.

  Kushiriki na wageni ahadi yako ya kufanya usafi wa kina

  Baada ya wewe au mshiriki wa timu yako ya kukaribisha wageni kuahidi kufuata mchakato wa kufanya usafi, ahadi yako ya kufanya usafi wa kina itaonyeshwa kwa wageni kwenye tangazo lako.

  Ulipata msaada uliohitaji?

  Makala yanayohusiana