Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Jinsi ya kufanya

Nini kitafanyika iwapo nitapata matatizo ya kiufundi wakati wa Tukio la Mtandaoni?

Ikiwa kuna matatizo yoyote ya kiufundi kama vile matatizo ya video au sauti ambayo yanawazuia wageni kushiriki katika tukio la mtandaoni, wana haki ya kurejeshewa fedha.

Wenyeji wa matukio ya mtandaoni

Ikiwa unapata matatizo yoyote ya kiufundi yanayokuzuia kuliongoza, kama vile matatizo ya video au sauti, utahitaji kuwarejeshea fedha wageni wako. Kutuma fedha zinazorejeshwa:

  1. Nenda kwenye Kalenda yako
  2. Pata tukio mahususi ambalo ungependa kughairi
  3. Bofya Ghairi tukio
  4. Bofya matatizo ya Zoom kama sababu
  5. Thibitisha kughairi

Hutapewa adhabu kwa kughairi kwa sababu ya matatizo ya kiufundi na wageni wako wote watarejeshewa fedha zote. Unaweza kuwatumia wageni wako ujumbe ili kuwajulisha kuwa fedha wanazorejeshewa zipo njiani na wanaweza kuweka nafasi tena ya tukio lako kwa wakati tofauti.

Kumbuka kwamba utaweza tu kurejesha fedha za tukio hadi wakati wa mwisho wa tukio hilo. Kwa mfano, ikiwa tukio lako linaanza saa 4: 00-5: 00 asubuhi, utaweza tu kughairi na kuwarejeshea fedha zote wageni wako hadi saa 5:00 asubuhi. Baada ya saa 5:00 asubuhi, hutaweza kughairi ikichukuliwa kwamba tukio liliendelea kama ilivyopangwa. Ikiwa utakosa fursa hii na mgeni anahitaji kurejeshewa fedha, tafadhali wasiliana na Usaidizi wa Jumuiya ili upate msaada.

Wageni wa matukio ya mtandaoni

Ikiwa una magumu yoyote ya kiufundi yanayokuzuia kujiunga na tukio, kama vile matatizo ya video au sauti, unaweza kuomba kurejeshewa fedha katika Kituo cha Usuluhishi. Ili kuomba urejeshewe fedha:

  1. Nenda kwenye kichupo cha Safari
  2. Pata tukio mahususi ambalo ungependa kuomba urejeshewe fedha
  3. BofyaOnyesha maelezo
  4. Bofya Tuma au uombe pesa

Baada ya kuomba urejeshewe fedha, unaweza kuweka nafasi tena kwenye tukio hilohilo kwa wakati tofauti.

Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili