Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Kuandaa Tukio la mtandaoni

  Jiunge na jumuiya ya Wenyeji inayounganisha ulimwengu kwa njia mpya kabisa.

  Kabla ya kuwasilisha tukio lako la mtandaoni, tafadhali somaviwango na matakwa kwa ajili ya Matukio ya Airbnb na matakwa mahususi kwa Matukio ya mtandaoni.

  Mchakato wa kuwasilisha

  Unapowasilisha tukio lako ili liidhinishwe, utahitaji kutoa:

  • Kichwa cha tukio lako
  • Maelezo, ikiwemo mahali unapotangazia na kile kinachofanya pawe maalumu
  • Maelezo ya shughuli yako, ikiwemo ajenda iliyobainishwa wazi
  • Sifa, historia au hati zako za utambulisho
  • Maelekezo kuhusu kile ambacho wageni wanapaswa kuleta
  • Picha zenye ubora wa juu za tukio lako, ikiwemo picha yako ukiwa unaongea mbele ya kamera yako au kompyuta ili kuonyesha kwamba tukio hilo linafanyika mtandaoni
  • Kitambulisho cha picha, kwa kuwa utaombwa uthibitishe utambulisho wako

  Mara tu unapokuwa na wazo zuri na kupanga maelezo yote,anza kuwasilisha. Fahamu nini cha kutarajia baada ya kuwasilisha.

  Jinsi zinavyofanya kazi

  Zoom

  Matukio ya mtandaoni hufanyiwa kwenye Zoom, programu ya mikutano ya video ya wahusika wengine, ambayo utahitaji pia kwa ili ajili ya mchakato wa kuwasilisha. Hapa kuna kila kitu unachohitaji kujua kuhusu kutumia Zoom kwa ajili ya Matukio ya Mtandaoni.

  Kuweka nafasi na kuhudhuria

  1. Kuweka nafasi hufanya kazi kwa njia ile ile kama kunavyofanya kazi kwa Matukio ya ana kwa ana
  2. Wakati wa kutiririsha utakapofika, wageni watapokea kiunganishi cha kujiunga kwenye mkutano wako wa Zoom
  3. Kisha unaweza kutumia kipengele cha Chumba cha Kusubiri cha Zoom ili kuwaruhusu waingie baada ya kuthibitisha kwamba wameweka nafasi

  Ikiwa unakubali kuruhusu wageni kadhaa wajiunge kwa kutumia kifaa kimoja, wajulishe wageni katika maelezo yako kuwa wanahitaji tu kuweka nafasi moja. Unaweza pia kuandaa Matukio ya makundi binafsi, ambapo wageni wanaweza kuweka nafasi zote kwa ajili ya Tukio kwa tarehe na wakati mahususi.

  Bei na malipo ya ziada

  Unachotoza ni juu yako kwa ajili ya Matukio ya makundi ya umma na ya binafsi. Unaweza kutaka kuanza kwa bei ya chini na uiongeze baada ya mazoezi fulani na tathmini kadhaa zenye ukadiriaji wa nyota 5. Kama ilivyo kwa Matukio ya ana kwa ana, Airbnb itamtoza Mwenyeji ada ya huduma, isipokuwa kama ni tukio la wajibu kwa jamii.

  Matukio ya mtandaoni yanawekewa bei kwa kila mtu kama chaguo-msingi. Ikiwa nafasi iliwekewa mtu mmoja kisha utambue kwamba kuna wageni 2 kwenye Chumba chako cha Kusubiri, unaweza kumwomba amlipie yule mtu wa ziada katikaKituo cha Usuluhishi.

  Ulipata msaada uliohitaji?

  Makala yanayohusiana