Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Je, Matukio ya Mtandaoni ni nini?

  Matukio ya mtandaoni ni vipindi vya video vya moja kwa moja, vyenye maingiliano ambavyo vinahusisha makundi madogo tu. Yanatoa ufikiaji kwa wenyeji weledi, maingiliano ya mtandaoni na njia nzuri ya kuungana na watu ulimwenguni kote.

  Tofauti kati ya matukio ya ana kwa ana na ya mtandaoni

  Matukio ya mtandaoni yanaandaliwa kwenye Zoom. Zoom ni tovuti ya wahusika wengine inayotoa huduma ya mikutano kwa njia ya video na inaweza kutumiwa kwenye kompyuta, tabuleti na vifaa vya mkononi.

  Viwango vya ubora

  Kama matukio ya ana kwa ana, matukio ya mtandaoni lazima yakidhi viwango vya ubora. Aidha, matukio ya mtandaoni lazima pia yakidhimahitaji ya ziada.

  Tathmini za wageni

  Wageni wana siku 30 za kuandika tathmini baada ya tukio kumalizika. Wanaweza kutoa maoni ya faraghani kwa ajili ya mwenyeji wao na maoni ya umma kwa ajili ya wageni wa siku zijazo. Soma zaidi kuhusu jinsi tathmini zinavyofanya kazi kwa matukio ya ana kwa ana na ya mtandaoni.

  Mabadiliko kwenye nafasi zilizowekwa

  Unaweza kughairi hadi siku 7 kabla ya wakati wa kuanza au ndani ya saa 24 baada ya kuweka nafasi, au ubadilishe nafasi uliyoweka hadi saa 72 kabla ya tukio kuanza.Sera za mabadiliko kwenye nafasi zilizowekwa zilizopo ni sawa kwa Matukio ya Airbnb ya mtandaoni na ya ana kwa ana.

  Bei

  Matukio ya mtandaoni bei yake ni kwa mtu mmoja kwa chaguomsingi. Wageni wanapaswa kuweka nafasi kwa ajili ya kila mtu anayejiunga na tukio. Hata hivyo, ikiwa mwenyeji anakubali wageni kuweka nafasi moja kwa kila kifaa, anaweza kuwajulisha wageni kwenye ukurasa wake wa tukio chini ya Utakachofanya na Jinsi ya Kushiriki.

  Kurejesha fedha

  Kwa matukio ya mtandaoni, wageni wanastahiki kurejeshewa fedha zote ikiwa kuna matatizo yoyote ya kiufundi, kama vile matatizo ya sauti au video, yanayotokea kwa sababu ya vifaa vyao wenyewe au kifaa cha mwenyeji. Unaweza kusoma sera kamili ya kurejeshewa fedha kwenye makala ya Sera Matukio ya Kurejesha Fedha ya Mgeni.

  Kituo cha Usuluhishi

  Ikiwa unahitaji kutuma au kuomba pesa au kulipia huduma za ziada na mwenyeji au mgeni wako, kama vile kuomba kurejeshewa fedha nje ya sera ya kughairi, tumia Kituo cha Usuluhishi.

  Ulipata msaada uliohitaji?

  Makala yanayohusiana