Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Jinsi ya kufanya
Mgeni

Je, ninahitaji kujua nini kabla ya kuhudhuria Tukio la Mtandaoni kwenye Zoom?

Zoom ni tovuti ya wahusika wengine kwa ajili ya mikutano kwa njia ya video na inaweza kutumiwa kwenye kompyuta, kompyuta ndogo na vifaa vya mkononi.

Mahitaji ya mfumo na muunganisho wa intaneti

Kabla ya kuhudhuria tukio lako, hakikisha kifaa chako kinakidhi mahitaji ya mfumo wa Zoom na uujaribu muunganisho wako wa intaneti kwa kujiunga na mkutano wa majaribio.

Ili kupata maelezo zaidi kuhusu mahitaji ya mfumo kwa ajili ya kompyuta, soma makala yaMahitaji ya Mfumo kwa ajili ya PC, Mac na Linux katika Kituo cha Msaada cha Zoom. Ili kupata maelezo zaidi kuhusu mahitaji ya mfumo kwa ajii ya kifaa cha mkononi, soma makala ya Mahitaji ya Mfumo kwa ajili ya iOS, iPadOS na Android. Ili kujaribu muunganisho wako wa intaneti, jiunge na mkutano wa majaribio.

Kudumisha faragha yako wakati wa kutumia Zoom

Faragha yako ni muhimu kwetu. Hapa kuna hatua ambazo tumechukua ili kusaidia kulinda faragha yako wakati wa matukio ya mtandaoni, pamoja na vidokezi kwa ajili yako ili kulinda faragha yako wakati wa kutumia Zoom. Ikiwa mpangilio wowote kati ya hii hautatumika katika tukio lako, tutakutaarifu kabla ya kuweka nafasi.

Jinsi Airbnb husaidia kulinda faragha yako unapotumia Zoom:

  • Kitambulisho cha mkutano kinacholindwa na nenosiri kinaundwa kinasibu kwa kila tukio
  • Matukio hayawezi kurekodiwa kupitia Zoom
  • Video ya mgeni inazimwa wakati wa kuingia kwenye chumba cha mkutano cha Zoom
  • Wageni hawawezi kushiriki skrini zao wakati wa tukio
  • Wageni hawawezi kuzungumza moja kwa moja na wageni wengine kupitia Zoom
  • Mafaili hayawezi kuhamishwa kupitia Zoom
  • Sehemu ya "chumba cha kusubiri" inawashwa kama chaguo-msingi, ikiwawezesha wenyeji kuwakaribisha wageni katika chumba cha mkutano wa Zoom kibinafsi

Vidokezi vya kukusaidia kulinda faragha yako:

  • Usishiriki na mtu mwingine yeyote kiunganishi cha mkutano wa Zoom kinacholindwa na nenosiri
  • Tumia toleo la kisasa zaidi la programu ya Zoom
  • Kuwa na ufahamu wa mazingira yako na kuna nini nyuma yako unapokuwa kwenye kamera—mwenyeji wako na wageni wengine wataweza kuyaona
  • Zima kinasa sauti hadi uwe tayari kuzungumza
  • Kuwa makini unapotumia huduma ya gumzo ya kikundi kwani washiriki wote wataweza kusoma unachochapisha
  • Ikiwa hutaki kutoa jina lako kamili kwa wageni na wenyeji wa tukio lako, unaweza kutumia jina tofauti au utumie jina lako la kwanza tu unapoingia kwenye Zoom
  • Tafadhali usipige picha ya skrini ya mwenyeji au wageni wengine bila idhini yao

Maelezo mafupi

Ili kufanya iwe rahisi kwa watu wenye ulemavu na mahitaji mengine ya ufikiaji wajiunge na matukio ya mtandaoni, tumewezesha utendaji wa manukuu yaliyofungwa kwenye Zoom. Huduma za maelezo mafupi zinaweza kutolewa na mwenyeji au mwenyeji mwenza, Zoom, au watoa huduma wa wahusika wa tatu na haziwezi kupatikana katika lugha zote.

Utiririshaji wa moja kwa moja

Katika visa vingine, tunaweza kutiririsha matukio ya mtandaoni kwa kutumia tovuti kama Facebook, YouTube, au Kaltura. Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi mikutano ya Zoom inavyotiririshwa moja kwa moja kupitiaYouTube na Facebook katika Kituo cha Msaada cha Zoom. Ikiwa tukio la Airbnb litatiririshwa moja kwa moja kwenye tovuti ya mhusika wa tatu, tutakuarifu kabla ya kuweka nafasi.

Utapokutana na mwenyeji wako

Utapokea kiunganishi cha kujiunga na tukio mtandaoni katika barua pepe yako ya uthibitisho na katika barua pepe ya ukumbusho itakayotumwa kabla ya tukio la mtandaoni kuanza. Unaweza pia kuipata katika taarifa ya nafasi uliyoweka inayopatikana kwenye ukurasa waSafari.

Ingia katika Zoom angalau dakika 5 mapema ili kuhakikisha kila kitu kinafanya kazi vizuri na kwamba umefika kwa wakati kwa ajili ya tukio. Ni muhimu kutambua kuwa mwenyeji wako ana chaguo la kuwakataa wageni waliochelewa na kwamba wageni wanaowasili kama wamechelewa hawastahiki kurejeshewa fedha. Pata maelezo zaidi katika makala yetu ya Sera ya Kurejesha Fedha ya Mgeni wa Matukio.

Matatizo kwenye Zoom

Hakikisha una kiunganishi sahihi kwa ajili ya tukio lako la mtandaoni. Ikiwa kiunganishi hakifanyi kazi, funga Zoom na ujaribu kiunganishi hicho tena. Ikiwa bado hakifanyi kazi, mtumie ujumbe mwenyeji wako ili kuhakikisha kama ana matatizo kwenye Zoom.

Ikiwa Zoom inakutaka uweke nenosiri, mtumie ujumbe mwenyeji wako kupitia Airbnb ili kuomba nenosiri.

Mwishowe, ikiwa mwenyeji hana tatizo lolote, tembelea Kituo cha Msaada cha Zoom.

Matatizo ya faragha au usalama wakati wa tukio

Ukikabili maudhui yoyote yasiyofaa, au ikiwa una tatizo linalohusu faragha au usalama wakati wa tukio lako, wasiliana na usaidizi wa jumuiya wa Airbnb kisha uripoti. Toa taarifa za kutosha kadri iwezekanavyo na Airbnb itachunguza suala hilo.

Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili