Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Lini ununue bima ya safari

  Kila mtu anapaswa kuzingatia kununua bima ya safari—inaweza kukulinda dhidi ya hasara ya kifedha isiyotarajiwa au mabadiliko ambayo lazima ufanye kabla au wakati wa safari yako. Hata hivyo, pengine tayari una bima kwa sasa, kwa hivyo iangalie kabla:

  • Kadi yako ya benki inaweza kutoa bima ya kukodisha gari au mafao mengine ya kusafiri
  • Sera ya mmiliki wa nyumba yako inaweza kutoa bima ya kushughulikia wizi au upotevu wa mali binafsi unapokuwa mbali na nyumbani
  • Mwajiri wako anaweza kutoa mafao ya kusafiri kwa wafanyakazi

  Mambo ya kuzingatia

  Kila bima ni tofauti, kwa hivyo tathmini sheria, bima, masharti na mazuio kwa uangalifu na usisite kuwasiliana na mtoa huduma ukiwa na maswali.

  Bima zinaweza kujumuisha:

  • Kughairi safari: Wakati sababu fulani zinazoshughulikiwa zinakuzuia kusafiri, kama vile hali ya hewa au mgomo wa wafanyakazi, ugonjwa, majeraha, kifo au usumbufu unaohusiana na kazi
  • Kukatiza safari: Kurudishiwa gharama endapo utahitaji kukomesha safari yako mapema
  • Gharama za matibabu: Kurudishiwa gharama za matibabu kwa sababu ya ugonjwa au ajali ambayo inafanyika wakati wa safari yako
  • Huduma za usaidizi wa dharura: Usaidizi unaposafiri kwa sababu ya mahitaji muhimu, kama vile usafirishaji wa dharura, uhamishaji wa matibabu, miadi ya daktari na viza zilizopotea au kuibiwa
  • Ulinzi wa mizigo iliyopotea na kuharibika: Kushughulikia endapo mali yako binafsi imepotea, imeibiwa au kuharibiwa unapokuwa safarini
  • Ghairi kwa Sababu Yoyote (CFAR): Kurudishiwa gharama kwa ajili ya safari nzima au sehemu ya gharama za safari zilizotokana na kughairiwa kwa safari yako kwa sababu yoyote

  Pata maelezo zaidi kuhusu bima ya safari

  Airbnb inatoa taarifa hii kwa madhumuni ya elimu tu na haitoi bima ya safari wala haipendekezi bidhaa au huduma za kampuni yoyote ya bima ya safari, mawakala au madalali.

  Ulipata msaada uliohitaji?

  Makala yanayohusiana