Ruka kwenda kwenye maudhui
  Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Kwa nini Matukio ya Airbnb ambapo nimekaribisha wageni yameghairiwa?

  Mnamo Machi 11, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kuzuka kwa ugonjwa wa COVID-19 kuwa ni janga la ulimwengu. Kulingana na mwongozo wa serikali na wataalamu wa afya ya umma kuhusu umbali kati ya watu, Matukio ya Airbnb yalisitishwa mnamo tarehe 18 Machi, 2020, na sitisho hilo litaendelea hadi angalau tarehe 30 Aprili, 2020 ili kulinda afya na usalama wa jumuiya yetu.

  Tunaamini kuwa kuchukua hatua hii kwa muda mfupi ni muhimu katika kuchangia kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi hivyo, na kwa muda mrefu hatua hiyo itadumisha matukio kama njia ya kuaminika ya kuungana na wengine ulimwenguni.

  Nafasi zilizowekwa zitafanyiwa nini

  Ikiwa uliweka nafasi kati ya tarehe 18 Machi na 30 Aprili, 2020, nafasi hiyo imeghairiwa kiotomatiki. Wageni wako watapokea au wamekwishapokea rejesho la fedha zote, ikiwemo rejesho la ada zote za huduma za Airbnb. Airbnb haitachukua ada zozote zinazohusiana na nafasi iliyowekwa.

  Kuweka nafasi ya matukio baada ya tarehe 30 Aprili

  Wageni wanaweza kuweka nafasi ya tukio lolote linalopatikana kwenye kalenda yako baada ya tarehe 30 Aprili, 2020. Airbnb itaendelea kufuatilia hali ulimwenguni na tutaifahamisha jumuiya yetu ikiwa hali itabadilika.

  Sera za kughairi Matukio ya Airbnb

  Mara baada ya Matukio ya Airbnb kuanza tena, sera ya kughairi matukio itatumika kwenye ughairi wowote. Kughairi kunakohusiana na COVID-19 kunashughulikiwa chini ya sera yetu ya sababu zisizozuilika. Tathmini makala yetu yasababu zisizozuilika kwa sababu ya COVID-19 ili kupata maelezo kuhusu hali zinazozingira COVID-19.