Ruka kwenda kwenye maudhui
  Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Muda wa kusubiri kwa wakati huu ni mrefu kuliko kawaida
  Kwa sababu ya virusi vya korona (COVID-19), kwa sasa tunapokea idadi kubwa ya maombi na huku tukiwa na idadi pungufu ya wafanyakazi. Ikiwa nafasi uliyoweka bado iko mbali na zaidi ya saa 72, tafadhali wasiliana nasi karibu na tarehe yako ya kuingia ili tuweze kuwasaidia wale wanaohitaji usaidizi wa haraka. Ili kubadilisha au kughairi nafasi uliyoweka, nenda kwenye ukurasa wako wa safari au dashibodi ya mwenyeji.

  Kwa nini Matukio ya Airbnb niliyowekea nafasi yameghairiwa?

  Mnamo tarehe 11 Machi, 2020, Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kuzuka kwa ugonjwa wa COVID-19 kuwa ni janga la kimataifa. Kulingana na mwongozo wa serikali na wataalamu wa afya ya umma kuhusu umbali kati ya watu, Matukio ya Airbnb yalisitishwa mnamo tarehe 18 Machi, 2020, na sitisho hilo litaendelea hadi angalau tarehe 30 Aprili, 2020 ili kulinda afya na usalama wa jumuiya yetu.

  Tunaamini kuwa kuchukua hatua hii kwa muda mfupi ni muhimu katika kuchangia kupunguza kasi ya kuenea kwa virusi hivyo, na kwa muda mrefu hatua hiyo itadumisha matukio kama njia ya kuaminika ya kuungana na wengine ulimwenguni.

  Nafasi zilizowekwa zitafanyiwa nini

  Ikiwa uliweka nafasi kati ya tarehe 18 Machi na 30 Aprili, 2020, nafasi hiyo imeghairiwa kiotomatiki. Utarejeshewa au umekwisha rejeshewa fedha zote kwenye njia ya malipo uliyotumia kuweka nafasi ya tukio. Pata maelezozaidi kuhusu jinsi mchakato wa kurejesha fedha hufanya kazi.

  Kuweka nafasi ya matukio baada ya tarehe 30 Aprili

  Unaweza kuweka nafasi kwenye tukio lolote linalopatikana baada ya tarehe 30 Aprili. Airbnb itaendelea kufuatilia hali ulimwenguni na tutaifahamisha jumuiya yetu ikiwa hali itabadilika.

  Sera za kughairi Matukio ya Airbnb

  Mara baada ya Matukio ya Airbnb kuanza tena, sera ya kughairi matukio itatumika kwenye ughairi wowote. Kughairi kunakohusiana na COVID-19 kunashughulikiwa chini ya sera yetu ya sababu zisizozuilika. Tathmini makala yetu yasababu zisizozuilika kwa sababu ya COVID-19 ili kupata maelezo kuhusu hali zinazozingira COVID-19.

  Ulipata msaada uliohitaji?