Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  China Bara: Sababu zisizozuilika kwa ajili ya COVID-19

  Imesasishwa terehe 25 Juni, 2020

  Makala haya yanaelezea fidia na mahitaji kwa ajili ya ughairi unaohusiana na COVID-19 chini ya sera yetu ya sababu zisizozuilika kwa ajili ya nafasi ambazo wageni kutoka China bara waliweka kwa ajili ya sehemu za kukaa na Matukio ya Airbnb huko China bara. Ikiwa nafasi iliyowekwa tayari imeshaanza (muda wa kuingia umepita) sababu hii isiyozuilika haitumiki. Kwa nafasi zozote zilizowekwa isipokuwa nafasi zilizowekwa China bara, rejelea makala yetu ya COVID-19 ya sababu zisizozuilika kwa maelezo kuhusu mambo yanayoshughulikiwa. Ili ughairi chini ya sera hii, utatakiwa kutoa hati zinazothibitisha sababu yako isiyozuilika.

  Nafasi zilizowekwa zinazoshughulikiwa

  Sera inatumika kwenye nafasi ambazo wageni kutoka China bara waliweka kwa ajili ya sehemu za kukaa na Matukio ya Airbnb huko China bara. Inaruhusu kughairi nafasi iliyowekwa ikiwa mambo yafuatayo ni kweli:

  • Imeathiriwa na ushauri rasmi wa serikali wa kusafiri au kizuizi ambacho kinakuzuia kusafiri kutoka mahali ulipo au kwenda mahali unakoelekea na
  • Iliwekwa mnamo au kabla ya tarehe ambayo ushauri au kizuizi kilitangazwa na
  • Tarehe ya kuingia si zaidi ya siku 30 kabla ya tarehe ya kughairi

  Sera haitumiki kwenye nafasi zilizowekwa ambazo tayari zimeghairiwa:

  • Kabla ya tarehe ya matangazo husika ya serikali au
  • Kulingana na makubaliano ya pamoja kati ya mwenyeji na mgeni

  Fikiria, kwa mfano, mlipuko wa COVID-19 jijini Beijing mnamo Juni 2020. Serikali ya Wananchi wa Manispaa ya Beijing na idara ya kudhibiti magonjwa ilitangaza tarehe 13 Juni, 2020 kwamba viwango vya hatari katika maeneo fulani jijini Beijing viliongezwa kuwa hali ya kadri au ya juu. Katika mfano huu, sera haitumiki kwenye ughairi wowote uliofanywa kabla ya tarehe 13 Juni, 2020, au kwenye nafasi zilizowekwa baada ya tarehe hiyo.

  Hati zinazohitajiwa

  Ikiwa nafasi uliyoweka inastahiki, tafadhali wasiliana nasi ndani ya siku 14 tangu tarehe ya kughairi. Utaombwa utoe hati zinazoonyesha sababu inayokuzuia kusafiri au kukaribisha wageni. Tutatathmini hati hizo kisha tuwasiliane nawe. Kunaweza kuwa na ucheleweshaji kwa sababu ya hali ya sasa ya COVID-19.

  Hati kwa ajili ya watu walioathiriwa

  Kwa wageni au wenyeji wa sehemu za kukaa na Matukio ya Airbnb:

  • Ikiwa eneo unaloishi limetiwa alama kama eneo la hatari ya kadiri au hatari kubwa ya COVID-19 kama inavyoelezwa na mamlaka, au ikiwa rangi ya Kifuko chako cha Afya inaonyesha nyekundu au njano, utahitaji kutoa picha ya skrini ya Kifuko chako cha Afya, tangazo rasmi la tathmini ya eneo hilo la kiwango cha hatari pamoja na uthibitisho wa makazi na/au uthibitisho wa eneo lako kama picha ya skrini ya programu yako ya ramani
  • Ikiwa umetambuliwa kuwa na COVID-19, unashukiwa kuwa na COVID-19, au umewekwa karantini kwa sababu ya COVID-19, unahitaji kutoa uthibitisho wa matibabu au hati zinazohusu hali hiyo zilizotolewa na mamlaka

  Hati za vizuizi vya eneo

  Ikiwa eneo la sehemu ya kukaa au Tukio la Airbnb limewekewa vizuizi vya kusafiri kwa sababu ya COVID-19, mwenyeji anahitaji kutoa hati za mahali ambapo sehemu ya kukaa au Tukio la Airbnb liko. Hii ni pamoja na:

  • Agizo la karantini kutoka kwa mamlaka za eneo husika
  • Vizuizi rasmi vya kusafiri au matakwa mengineyo yanayohusiana na COVID-19 kutoka katika serikali za eneo husika
  • Tangazo au arifa ya kuzuia kuingia au kutoka kwa ajili ya jengo au sehemu hiyo

  Hati kwa ajili ya hali nyinginezo za COVID-19

  • Uthibitisho wa kwamba usafiri wako wa ndege au ardhi umeghairiwa na mtoa huduma ya usafiri kwa sababu ya COVID-19 au sera husika za umma
  • Beji yako ya mfanyakazi au hati zinazohusika zilizotolewa na mwajiri wako ambazo zinaonyesha majukumu yako ya matibabu au ya kudhibiti ugonjwa kuhusiana na COVID-19

  Jinsi inavyofanya kazi

  Ikiwa wewe ni mgeni, unaweza kutathmini sera ya kughairi ya nafasi uliyoweka na upate machaguo ya kughairi kwa kuchagua safari yako kutoka kwenye Ukurasa wa safari. Ikiwa nafasi uliyoweka haijumuishwi, sera ya kughairi ya mwenyeji itatumika kama kawaida.

  Ikiwa wewe ni mwenyeji, utapata taarifa katika dashibodi yako ya mwenyeji.

  Tunakuhimiza uwasiliane na mwenyeji wako au mgeni ili mzungumzie kughairi na kurejesha fedha.

  Taarifa zaidi

  Tumechuja makala ili kuisaidia jumuiya yetu wakati huu katika Kituo cha Nyenzo. Unaweza kupata taarifa ya hivi karibuni kuhusu mwitikio wetu wa COVID-19, kuanzia mabadiliko ya sera hadi nyenzo kwa ajili ya wenyeji na wageni.

  Unaweza pia kusoma sera ya sababu zisizozuilika ili upate maeleo kuhusu kushughulikiwa kwa hali zisizohusiana na COVID-19.

  Ikiwa wewe ni mwenyeji, tunapendekeza ufuatilie mahitaji ya eneo husika kuhusu kuzuia na kudhibiti COVID-19. Tunapendekeza uwasiliane na mgeni wako mapema na uthibitishe kiwango cha hatari katika eneo anakotoka na iwapo ana uthibitisho wa hali ya afya unaohitajika kwenye eneo lako.

  Tunawaomba wanajumuia wote wazingatie heshima, ujumuishaji na sera yetu ya kutobagua wakati wa kuingiliana na wanajumuiya wengine wa jumuiya yetu.

  Tutaendelea kutathmini matumizi ya sera hii. Tafadhali angalia ukurasa huu mara kwa mara kwa habari za hivi karibuni na taarifa mpya.

  Ulipata msaada uliohitaji?

  Makala yanayohusiana