Machaguo ya kughairi kwa sababu ya COVID-19
Nafasi zilizowekwa mnamo au kabla ya tarehe 14 Machi, 2020
Ikiwa uliweka nafasi mnamo au kabla ya tarehe 14 Machi, 2020 na COVID-19 inaathiri mipango yako ya kusafiri, unaweza kufahamu machaguo yako ya sasa ya kughairi na kurejeshewa fedha kwa kwenda kwenye ghairi nafasi uliyoweka kisha uchague Mipango yangu ya kusafiri imebadilika kwa sababu ya janga la ugonjwa wa COVID-19.
Kulingana na hali zako, unaweza kuona moja au zaidi ya machaguo yafuatayo:
- Kurejeshewa fedha kulingana na sera ya kughairi ya Mwenyeji wako
- Kurejeshewa fedha taslimu kamili baada ya kuwasilisha nyaraka rasmi kwa ajili ya kutathminiwa
- Salio la safari la sababu zisizozuilika
- Mwombe Mwenyeji wako akurejeshee fedha zote
Nafasi zilizowekwa baada ya tarehe 14 Machi, 2020 na kabla ya tarehe 31 Mei, 2022
Ikiwa uliweka nafasi baada ya tarehe 14 Machi, 2020 na kabla ya tarehe 31 Mei, 2022 na COVID-19 inaathiri mipango yako ya kusafiri, sera ya kughairi ya Mwenyeji wako itatumika. Hata hivyo, ikiwa unaugua COVID-19, hii inalindwa chini ya Sera yetu ya Sababu Zisizozuilika.
Ikiwa nafasi uliyoweka haistahiki kurejeshewa fedha zote, unaweza kumtumia Mwenyeji wako ujumbe wakati wowote ili kujua ikiwa angependa kukurejeshea fedha za ziada kupitia Kituo cha Usuluhishi.
Nafasi zilizowekwa mnamo au baada ya tarehe 31 Mei, 2022
Ikiwa nafasi yako iliwekwa mnamo au baada ya tarehe 31 Mei, 2022 na COVID-19 inaathiri mipango yako ya kusafiri, sera ya kughairi ya Mwenyeji wako itatumika. Sera yetu ya Sababu Zisizozuilika hailindi ughairi unaohusiana na COVID-19 kwa nafasi hizi zilizowekwa.
Mambo mengine unayopaswa kufahamu
Taarifa iliyo hapo juu haitumiki kwenye nafasi zilizowekwa za Luxe, ambazo zinadhibitiwa na Sera tofauti ya Kuweka Tena Nafasi na Kurejesha Fedha ya Luxe. Kwa nafasi za Luxe zilizowekwa kabla ya tarehe 20 Machi, 2020, angalia mwitikio wa Airbnb Luxe kwa COVID-19 na uwasiliane moja kwa moja na mbunifu wa safari yako ukiwa na maswali yoyote.
Sera tofauti zinatumika kwa nafasi zilizowekwa za ndani nchini Korea Kusini.
Makala yanayohusiana
- MgeniKughairi safari kutokana na sababu zisizozuilikaPata maelezo kuhusu matakwa na jinsi ya kuchukua hatua zinazofuata.
- MgeniSera ya Sababu Zisizozuilika na virusi vya korona (COVID-19)Pata maelezo juu ya kile kinachojumuishwa kwenye COVID-19 chini ya sera yetu ya sababu zisizozuilika.
- MgeniSera ya Sababu ZisizozuilikaPata maelezo kuhusu jinsi kughairi kunavyoshughulikiwa wakati matukio yasiyotarajiwa usiyoweza kudhibiti yatatokea baada ya kuweka nafasi na…