Ruka kwenda kwenye maudhui
  Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Sera ya sababu zisizozuilika na virusi vya korona (COVID-19)

  Imesasishwa terehe 31 Machi, 2020

  Mnamo Machi 11, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) lilitangaza kuzuka kwa ugonjwa wa virusi vya korona, unaojulikana kama COVID-19, kuwa janga la ulimwengu. Tangu wakati huo, mlipuko huo umeenea haraka huku serikali ulimwenguni kote zikichukua hatua za haraka ili kupunguza kuenea kwa COVID-19.

  Kwa sababu hiyo, tunachukua hatua hizi ili kujumuisha ugonjwa wa COVID-19 chini ya sera yetu ya sababu zisizozuilika ili kusaidia kuilinda jumuiya yetu na kuleta utulivu. Tafadhali angalia ukurasa huu mara kwa mara kwa mabadiliko kuhusu ujumuishaji.

  Kidokezi: Ikiwa wewe ni mgeni, unaweza kupata machaguo ya kughairi na ya kurejesha fedha kwa kuchagua safari yako kutoka Ukurasa wa safari. Ikiwa wewe ni mwenyeji, utapata taarifa katika dashibodi yako ya kukaribisha wageni.

  Muhtasari

  Nafasi za sehemu za kukaa na Matukio ya Airbnb zilizowekwa mnamo au kabla ya tarehe 14 Machi 2020, zikiwa na tarehe wa kuingia kati ya tarehe 14 Machi 2020 na tarehe 31 Mei 2020, zimejumuishwa kwenye sera na zinaweza kughairiwa kabla ya kuingia. Wageni ambao wanaghairi watakuwa na machaguo anuwai ya kughairi na urejeshaji wa fedha, na wenyeji wanaweza kughairi bila malipo au athari kwa hadhi yao ya Mwenyeji Bingwa. Airbnb itarejesha fedha, au itatoa salio la safari ambalo linajumuisha, ada zote za huduma kwa ughairi uliojumuishwa. Ili ughairi chini ya sera hiyo, utatakiwa kuthibitisha ukweli wa na/au kutoa hati za ushahidi wa sababu zako zisizozuilika.

  Sera ya kughairi ya mwenyeji itatumika kama kawaida kwa nafasi zilizowekwa baada ya tarehe 14 Machi, 2020.

  Kughairi kutashughulikiwa kulingana na bima ya sababu zisizozuilika inayotumika wakati wa kuwasilisha.

  Ikiwa nafasi iliyowekwa tayari imekwishaanza (muda wa kuingia umepita) sababu hii isiyozuilika haitumiki

  Sera tofauti zinatumika kwa nafasi zilizowekwa nchini China bara na kwa nafasi zilizowekwa za Luxe au Luxury Retreats.

  Nafasi zilizowekwa ambazo zimejumuishwa

  Nafasi zilizowekwa mnamo au kabla ya tarehe 14 Machi 2020

  Nafasi za sehemu za kukaa na Matukio ya Airbnb zilizowekwa mnamo au kabla ya tarehe 14 Machi 2020, zikiwa na tarehe ya kuingia kati ya tarehe 14 Machi 2020 na tarehe 31 Mei 2020, zinaweza kughairiwa kabla ya kuingia. Hii inamaanisha kwamba wageni watakaoghairi watapokea, kwa chaguo lao, salio la safari au kurejeshewa fedha kamili, wenyeji wanaweza kughairi bila kutozwa wala kuathiri hadhi yao ya Mwenyeji Bingwa na Airbnb itarejesha fedha, au itatoa salio la safari kwa kiasi kinachojumuisha ada zote za huduma.

  Nafasi za sehemu za kukaa na Matukio ya Airbnb zilizowekwa mnamo au kabla ya tarehe 14 Machi 2020, zikiwa na tarehe ya kuingia baada ya tarehe 31 Mei 2020, hazijajumuishwa kwa sasa kwenye sera yetu ya sababu zisizozuilika za COVID-19. Sera ya kughairi ya mwenyeji itatumika kama kawaida.

  Ikiwa uwekaji nafasi tayari umeshaanza (tarehe ya kuingia imepita) sababu hii isiyozuilika haitatumika.

  Nafasi zilizowekwa baada ya tarehe 14 Machi 2020

  Nafasi za sehemu za kukaa na Matukio ya Airbnb zilizowekwa baada ya tarehe 14 Machi 2020 hazitajumuishwa chini ya sera yetu ya sababu zisizozuilika, isipokuwa ambapo mgeni au mwenyeji ameambukizwa COVID-19. Masuala yanayohusiana na COVID-19 ambayo hayajumuishwi ni pamoja na: usumbufu wa usafiri na kughairi; ushauri na vikwazo vya usafiri; ushauri wa kiafya na karantini; mabadiliko katika sheria inayotumika; pamoja na maagizo mengine ya serikali—kama vile maagizo ya kuhamisha watu, kufungwa kwa mpaka, marufuku ya kukodisha nyumba kwa muda mfupi, na amri za kuwataka watu wasitoke maeneo walipo. Sera ya mwenyeji ya kughairi itatumika kama kawaida.

  Sera yetu ya sababu zisizozuilika imekusudiwa kuwalinda wageni na wenyeji dhidi ya hali ambazo hazikutarajiwa ambazo hutokea baada ya kuweka nafasi. Baada ya tamko la Shirika la Afya Duniani kwamba ugonjwa wa COVID-19 ni janga la kimataifa, sera ya sababu zisizozuilika haitatumika tena kwa sababu COVID-19 na matokeo yake hayapo tena miongoni mwa masuala yasiyotabirika au yasiyotarajiwa. Tafadhali kumbuka kutathmini kwa uangalifu sera ya mwenyeji ya kughairi wakati wa kuweka nafasi na uzingatie chaguo ambalo linakubali mabadiliko.

  Inavyofanya kazi

  Ikiwa wewe ni mgeni, unaweza kutathmini sera ya kughairi ya nafasi uliyoweka na upate machaguo ya kughairi na ya kurejesha fedha kwa kuchagua safari yako kutoka Ukurasa wa safari. Ikiwa wewe ni mwenyeji, utapata taarifa katika dashibodi yako ya kukaribisha wageni.

  Taarifa na rasilimali kuhusu virusi vya korona

  Tumekusanya na kuhariri makala ya kusaidia jumuiya yetu katika wakati huu kwenye Kituo cha Nyenzo. Unaweza kupata taarifa za hivi karibuni kuhusu majibu yetu ya COVID-19, kutoka kwa mabadiliko kwenye sera hadi rasilimali kwa wenyeji na wageni.

  Unaweza pia kusoma sera ya sababu zisizozuilika ili kupata maelezo zaidi kuhusu ujumuishaji wa hali zisizohusiana na COVID-19.

  Tunawaomba wanajumuiya wote kuwa waangalifu wa heshima, ujumuishaji, na sera yetu ya kutobagua wanapoingiliana na wanajumuiya wetu wengine.

  Tutaendelea kutathmini matumizi ya sera hii. Tafadhali angalia ukurasa huu mara kwa mara kwa mabadiliko na taarifa mpya.

  Ulipata msaada uliohitaji?

  Ingia ili kupata usaidizi mahususi

  Pata msaada na kutoridhishwa kwako, akaunti, na zaidi.
  Jisajili