Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Jinsi Mpango wa Balozi unavyofanya kazi

  Mabalozi ni Wenyeji Bingwa wanaowasaidia watu ulimwenguni kote kugundua faida za kukaribisha wageni. Wanapata tuzo ya ada ya mwalikwa wanapoleta Wenyeji wapya kwenye Airbnb na kutoa ushauri wa ana kwa ana na nyenzo za kuwasaidia Wenyeji wapya kufanikiwa.

  Kuwa Balozi

  Ikiwa wewe ni Mwenyeji Bingwa na unataka kushiriki uzoefu wako na Wenyeji wapya, basi unaweza kuwa Balozi.

  Faida za kuwa Balozi ni pamoja na:

  • Unapowaalika au kuwashauri Wenyeji wapya, utapokea tuzo za thamani ya juu kuliko unavyoweza kupata nje ya mpango wa Balozi
  • Unaweza kuwaalika wenyeji wengi bila kikomo
  • Unapata ufikiaji wa vipengele vya kipekee, nyenzo na vidokezi

  Ili kustahiki mpango huo, lazima uwe Mwenyeji Bingwa na akaunti yako lazima iwe ya kuaminika. Ili kutuma ombi la kuwa Balozi, tembelea ukurasa wa tovuti wa Mpango wa Balozi.

  Kudumisha hadhi yako ya Balozi

  Kila baada ya miezi mitatu, tunaangalia ili kuhakikisha kwamba unaendelea kukidhi vigezo vifuatavyo:

  • Umedumisha hadhi ya Mwenyeji Bingwa
  • Akaunti yako inaendelea kuwa ya kuaminika
  • Umekamilisha angalau mwaliko mmoja katika miezi mitatu iliyopita

  Mabalozi ambao hawatimizi vigezo vya robo mwaka wanakaribishwa kutuma ombi tena baadaye.

  Kuwa Balozi

  Kuna njia mbili za kuingiliana na Wenyeji wapya: kwa kuwaalika kwenye Airbnb na kusaidia kujibu maswali wanapounda tangazo au kwa kuungana nao kupitia mpango wa Muulize Mwenyeji Bingwa.

  Kuwaalika Wenyeji wapya

  Ili kuwaalika Wenyeji watarajiwa, nenda kwenye dashibodi yako ya Balozi, nakili kiunganishi chako cha kipekee cha mwalikwa na ukishiriki kupitia njia unazopendelea: ujumbe, barua pepe, mitandao ya kijamii, n.k. Wenyeji watarajiwa wanaotumia kiunganishi chako cha mwalikwa watafika kwenye ukurasa mahususi ulio na jina lako na picha ya wasifu, ambapo wanaweza kuunda tangazo jipya. Tafadhali kumbuka kwamba utapokea tuzo kwa ajili ya mwalikwa iwapo Mwenyeji mpya uliyemwalika atafuata kiunganishi chako cha kipekee cha mwaliko na kuunda tangazo katika kipindi hicho hicho.

  Unaweza kumwalika mtu yeyote ambaye ni mpya katika huduma ya kukaribisha wageni kwenye Airbnb, hata ikiwa tayari ana akaunti ya Airbnb. Itampasa akaribishe wageni kwenye nyumba nzima ndipo upate tuzo — Wenyeji wa vyumba vya kujitegemea au vya pamoja hawastahiki. Pia, mtu yeyote ambaye hapo awali alipokea mwaliko kutoka kwa mtu mwingine au anayetumia programu iliyounganishwa na API, hastahiki kuwa mmoja wa waalikwa wako. (Watu wanaoishi China Bara pia hawastahiki.) Unaweza kuwaelekeza Wenyeji watarajiwa kwenye ukurasa wa tovuti wa Balozi ili kupata maelezo zaidi kuhusu Mabalozi.

  Kushiriki kwenye mpango wa Muulize Mwenyeji Bingwa

  Ikiwa umeidhinishwa kuwa Balozi wa Wenyeji Bingwa, tutakuunganisha na Wenyeji wapya kupitia mpango wetu wa Muulize Mwenyeji Bingwa. Unaweza kuwaongoza kupitia mchakato wa kuunda tangazo lao wenyewe, kutoa ushauri kuhusu mambo kama kufanya usafi na kupiga picha sahihi, kushiriki uzoefu na vidokezi na ujipatie tuzo unapofanya hivyo. Mara baada ya kukamilika kwa nafasi ya kwanza aliyowekewa Mwenyeji mpya, umemaliza!

  Utaweza kufikia dashibodi ambapo unaweza kufuatilia miunganisho ya Mwenyeji wako mpya na uangalie maendeleo yake katika safari yake. Airbnb ina maktaba ya vidokezi, mapendekezo na warsha za kusaidia safari yako na Wenyeji watarajiwa. Tutawezesha nyenzo zetu zipatikane ili kusaidia kujibu maswali yanayoweza kuulizwa.

  Faida za kuwa Balozi

  Jinsi tuzo zinavyohesabiwa

  Kiasi unachojipatia kutokana na kuwaalika na kuwashauri Wenyeji wapya kinategemea mambo kadhaa, ikiwemo eneo na aina ya tangazo lao. Kwa sababu hiyo, unaweza kupokea malipo tofauti kwa ajili ya kila mwalikwa anayefuzu au kila Mwenyeji unayemsaidia kupitia mpango wa Muulize Mwenyeji Bingwa. Iwapo Mwenyeji wako mpya atafanya mabadiliko yoyote kwenye tangazo lake, hii inaweza kuathiri jinsi ambavyo kiasi cha malipo unayopokea kinahesabiwa. Ili kutazama tuzo yako ya pesa taslimu, tembelea Dashibodi yako ya Balozi.

  Utakapolipwa

  Utalipwa wakati Mwenyeji mpya uliyemwalika au kumshauri kupitia Muulize Mwenyeji Bingwa, atakamilisha nafasi ya kwanza aliyowekewa inayofuzu. Nafasi aliyowekewa lazima iwe na thamani ya angalau USD100 au sarafu sawa ya nchi husika (kabla ya kodi na ada) na lazima ikamilike kabla ya siku 150 baada ya kumwalika. Hii haimaanishi kwamba bei ya kila usiku ya tangazo hilo jipya lazima iwe zaidi ya USD100, lakini inamaanisha kwamba thamani ya jumla ya nafasi aliyowekewa (ikiwemo usiku wote) lazima izidi USD100.

  Nafasi zilizowekwa zinazofuzu lazima ziwe halali — nafasi bandia zilizowekwa, nafasi zilizowekwa na familia au marafiki, makubaliano ya kugawana tuzo za mwalikwa au mipango mingine ya hongo inakiuka sheria za mpango. Mwenyeji aliyealikwa lazima pia awe mpya katika kuduma ya kukaribisha wageni kwenye tovuti, kumaanisha kwamba nyumba hiyo inatangazwa na mtu huyo kwa mara ya kwanza na kwamba hajawahi kutangaza nyumba nyingine yoyote kwenye Airbnb hapo awali.

  Malipo yanayotumwa kwa kawaida hufanyika takribani siku 14 baada ya mgeni kutoka kwenye nafasi iliyowekwa inayofuzu. Kwa mfano, ikiwa tarehe ya kutoka kwenye nafasi iliyowekwa inayofuzu ni tarehe 10 Januari, kwa kawaida malipo yatatumwa karibu tarehe 24 Januari.

  Miongozo ya Balozi

  Mabalozi wanapaswa kuzingatia miongozo hii:

  1. Ili kuunda muktadha kwenye usaidizi unaotoa, huenda ikafaa iwapo ungejitambulisha kama Balozi ambaye lengo lake ni kuwasaidia Wenyeji wapya kuanza huduma yao kwenye Airbnb kwa mafanikio.
  2. Mabalozi si wafanyakazi wa Airbnb na hawafanyi kazi chini ya mwelekezo wa wafanyakazi wa Airbnb. Hii lazima idhihirishwe kwa waalikwa katika mawasiliano yako. Mabalozi ni makandarasi wa kujitegemea wenye biashara zao wenyewe na hawapaswi kujumuisha jina, nembo na IP nyingine za Airbnb katika nyenzo zote za uuzaji kama vile majina ya vikoa, majina ya biashara, chapa, zabuni kwenye maneno muhimu, akaunti za mitandao ya kijamii au vitambulisho vingine vya chanzo. Maelezo zaidi yanaweza kupatikana kwenye Sheria na Masharti ya Mpango wa Mwalikwa na Balozi.
  3. Hupaswi kamwe kutoa ushauri wa kisheria au ushauri mahususi unaohitaji leseni au utaalamu katika taaluma hiyo, kama vile kodi au kutoa vibali, katika kazi yako kama Balozi.
  4. Usiwatumie waalikwa wako barua pepe kiholela. Heshimu faragha yao na uwasiliane tu na watu ambao wamekubali kuwasiliana na wewe.
  5. Katika machapisho ya mitandao ya kijamii, unapaswa kutumia #AirbnbAmbassador.
  6. Katika barua pepe na nyenzo nyingine, unapaswa kujumuisha ufichuzi kama vile "Kama Balozi wa Airbnb, ninajipatia mapato unapokuwa Mwenyeji."
  7. Mabalozi hawana ruhusa ya kuunda nyenzo ya uuzaji, ikiwemo matumizi ya tovuti na machapisho kwenye mitandao ya kijamii, ambayo yanaweza kuwafanya watu wafikiri kwamba yanatoka kwa Airbnb au kuhusishwa na Airbnb kwa njia inayopotosha.

  Angalia Sheria na Masharti haya ya Mwalikwa na Balozi ili kupata maelezo zaidi.

  Ulipata msaada uliohitaji?