Ruka kwenda kwenye maudhui
  Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Habari za hivi punde kuhusu COVID-19
  Ili upate machaguo ya kughairi na kurejesha fedha, chagua nafasi iliyowekwa kwenye ukurasa wa Safari. Sera yetu ya sababu zisizozuilika inatumika tu kwenye nafasi fulani zilizowekwa. Ikiwa tarehe yako ya kuingia ni baada ya tarehe 15 Septemba, rudi hapa tena tarehe 15 Agosti, 2020 ili kupata habari za hivi punde.

  Ninapaswa kujua nini kuhusu usalama wa moto na monoksidi ya kaboni ninaposafiri?

  Vifaa muhimu vya usalama na ulinzi vinavyopaswa kuwa katika nyumba yoyote. Sisi huwahamasisha wenyeji kuweka vigundua moshi na monoksidi ya kaboni (CO) katika sehemu zao, lakini pia ni muhimu kwa wageni kuendelea kuwa na ufahamu na kuchukua tahadhari za usalama wakati wowote—na kwa njia yoyote—wanaposafiri.

  Unapoweka nafasi kwenye Airbnb, unapaswa kutathmini taarifa kuhusu ikiwa mwenyeji amaripoti uwepo wa vigundua moshi na monoksidi ya kaboni kwenye nyumba au la. Utapata maelezo haya kwenye ukurasa wa tangazo chini ya Vistawishi.

  Vigundua monoksidi ya kaboni ni nadra katika sehemu nyingi duniani, kwa hiyo tunakushauri kununua kimoja ili ukibebe wakati unasafiri, hasa ikiwa hakipo katika nyumba unamokaa. Huu hapamfano wa kigundua monoksidi ya kaboni kinachobebeka.

  Taarifa ya usalama kutoka katika shirika la Msalaba Mwekundu la Marekani

  Monoksidi ya kaboni (CO) ni gesi isiyoonekana, isiyo na harufu, isiyo na rangi ambayo huundwa wakati nishati (kama vile petroli, kuni, makaa ya mawe, gesi ya asili, propani, mafuta na metani) inapokosa kuteketea kikamilifu. Inaweza kuzalishwa na vifaa vya kuchoma nishati katika nyumba, ikiwa ni pamoja na tanuri, majiko makubwa, hmitambo ya kupasha maji moto na meko ya kupasha chumba joto, viwango vya juu vya monoksidi ya kaboni vinaweza kuua. Unachoweza kufanya:

  • Usitumie jenereta, grili, jiko la kambi, au petroli nyingine, propani, gesi ya asili, au meko ya makaa ndani ya nyumba, maegesho, chumba cha chini ya ardhi, sehemu ya kutambaa chini ya sakafu, au sehemu yoyote isiyopeneza hewa moja kwa moja.
  • Weka vifaa hivi nje, mbali na milango, madirisha na mipenyo ambayo inaweza kuruhusu monoksidi ya kaboni kuingia ndani.
  • Kufungua milango na madirisha au kutumia viyoyozi havizuii monoksidi ya kaboni kwenye nyumba. Ingawa monoksidi ya kaboni haiwezi kuonekana au kunuswa, inaweza kusababisha hali ya kulemazwa kikamilifu na kifo haraka. Hata kama husikii harufu ya moshi inayotokea, bado unaweza kuathiriwa na monoksidi ya kaboni. Ikiwa unaanza kujihisi mgonjwa, mwenye kizunguzungu, au mdhaifu wakati unatumia jenereta, nenda palipo na hewa safi mara moja—usichelewe.
  • Kengele za monoksidi ya kaboni * lazima ziwekwe katika maeneo ya katikati katika kila ngazi ya nyumba yako na nje ya maeneo ya kulala ili kutoa onyo la mapema la kukusanyika kwa monoksidi ya kaboni.
  • Betri zinapaswa kupimwa mara kwa mara na kubadilishwa inapohitajika.
  • Ikiwa kengele ya monoksidi ya kaboni inapiga kelele, nenda haraka palipo na hewa safi nje au kwenye dirisha lililo wazi au mlango wa nje. Hupaswi kamwe kupuuza kengele ya monoksidi ya kaboni; gesi hii inaweza kudhuru na unahitaji kupata hewa safi. Piga simu kwa huduma za dharura mahali ulipo kwa usaidizi ukiwa katika eneo la hewa safi na ukae hapo mpaka wafanyakazi wa dharura wawasili ili kukusaidia.

  Tembelea www.redcross.org/homefires kwa taarifa zaidi.

  * Ili kuwasiliana na hadhira ya kimataifa, Airbnb mara nyingi hutumia maneno "kengele" na "kigunduzi" kwa kubadilishana.

  Jina, nembo na vifaa vya hakimiliki vya shirika la Msalaba Mwekundu la Marekani vinatumiwa kwa ruhusa ya shirika hilo, utumiaji huu haupaswi kufasiriwa kumaanisha uidhinishaji, ulioelezwa au wa kudhaniwa, wa bidhaa, huduma, kampuni, maoni au nafasi ya kisiasa. Nembo ya shirika la Msalaba Mwekundu la Marekani ni alama ya biashara iliyosajiliwa na inayomilikiwa na shirika la Kitaifa la Msalaba Mwekundu la Marekani. Kwa taarifa zaidi kuhusu shirika la Msalaba Mwekundu la Marekani, tafadhali tembelea redcross.org.

  Ulipata msaada uliohitaji?