Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Kuna vidokezi vipi vya usalama kwa wageni wa maeneo ya ukaaji?

  Hivi ni baadhi ya vidokezi vya kukusaidia kusafiri ukiwa na uhakika.

  Tafuta na uweke nafasi ukiwa na uhakika

  Pata kile hasa unachotafuta kwa kutumia vizuri vichujio vyetu vingi kama vile bei, aina ya nyumba na vistawishi. Umepata nyumba unayoipenda? Hakikisha umesoma wasifu wa mwenyeji na maelezo ya tangazo kikamilifu—ukizingatia hasa vistawishi, sheria za nyumba na sera ya kughairi.

  Soma viwango na tathmini

  Soma maoni ya wageni wa awali ili yakusaidie kupata sehemu inayokufaa. Utapata viwango kuhusu vipimo mbalimbali vya ubora, kama vile usafi na usahihi, na tathmini za kina zenye maoni halisi. Wageni wanaweza kuandika tu maoni baada ya kukaa kwa mwenyeji huyo, basi unajua kwamba maoni unayosoma yanategemea mtu aliyekaa hapo.

  Tathmini vipengele vya usalama

  Unapoweka nafasi kwenye Airbnb, unapaswa kutathmini taarifa ya iwapo mwenyeji ameripoti au hakuripoti vigundua moshi na kaboni monoksidi kwenye eneo hilo. Utapata maelezo haya kwenye ukurasa wa tangazo chini ya Vistawishi.

  Vigundua kaboni monoksidi havitumiki sana katika maeneo mengi duniani, basi tunapendekeza ununue chako mwenyewe uendapo safari, hasa ikiwa sehemu unayokaa haina chochote. Hiki hapa ni kielelezo kimoja cha kigundua kaboni monoksidi cha kubebeka.

  Jibiwa maswali yako

  Kifaa chetu cha kutuma ujumbe kwa njia salama ni njia salama na rahisi kwako kuuliza mwenyeji mtarajiwa maswali yoyote uliyo nayo kabla ya kuweka nafasi. Baada ya kuweka nafasi, unaweza pia kumtumia mwenyeji wako ujumbe ili kupanga uingiaji na kuuliza maswali ya ziada, na kuendelea kuwasiliana muda wote wa safari yako.

  Nyakati zote wasiliana na kulipa kupitia Airbnb

  Jilinde mwenyewe na pia malipo yako na taarifa zako za kibinafsi kwa kutumia tovuti yetu salama wakati wa mchakato huo wote—kuanzia mawasiliano hadi uwekaji nafasi na malipo. You should never be asked to wire money, provide credit card information, or otherwise pay a host directly. Ukiombwa, tafadhali toa ripoti kwetu mara moja.

  Kagua usalama

  Mara ukiisha kuwasili kwenye nyumba au tukio lako, hakikisha unajua mahali vilipo vifaa vyote vya hali ya dharura na taarifa ya usalama. If you’re not sure where something like the first aid kit or fire extinguisher is, don’t hesitate to ask your host. Ni bora kuwa tayari sikuzote.

  Fanya utafiti wa arifa na maonyo ya ndani ya usafiri

  Iwe unasafiri na Airbnb au hapana, nyakati zote inafaa kufanya utafiti mapema kuhusu eneo unakoenda, na uwasiliane na ubalozi wako ulio karibu iwapo kuna maonyo ya usafiri au mahitaji mahususi. Kwa mfano, wasafiri kutoka Marekani wanapaswa kuwasiliana na Wizara ya Mambo ya Njekuhusu taarifa za viza na maonyo ya usafiri.

  Pata maelezo zaidi kwenye ukurasa wetu wa Imani na Usalama.

  Kumbuka: Katika hali ya dharura, au ikiwa usalama wako binafsi unatishiwa, wasiliana na polisi wa eneo hilo au huduma za dharura mara moja.

  Ulipata msaada uliohitaji?

  Makala yanayohusiana