Vidokezi vya usalama vya kuchagua eneo
Kusafiri kwa ujumla kunamaanisha kutumia wakati na pesa zako mwenyewe. Kwa hivyo unataka kuhakikisha kwamba unapata eneo linalokufaa. Hivi ni baadhi ya vidokezi vya kukusaidia kusafiri ukiwa na uhakika, ukijua kwamba umefanya uamuzi sahihi.
Kutafuta kile kinachokufaa
Kwanza kabisa, pata sehemu ambayo inakidhi mahitaji yako kwa kutumia vichujio vyetu vingi vya utafutaji. Unapoona eneo unalolipenda sana, soma kwa uangalifu wasifu wa Mwenyeji na maelezo ya tangazo, ukizingatia hasa vistawishi, sheria za nyumba na sera ya kughairi.
Soma ukadiriaji na tathmini
Daima tunapendekeza usome maoni kutoka kwa wageni wengine kama njia bora ya kupata sehemu inayokufaa. Utapata ukadiriaji kuhusu mambo kama vile usafi na usahihi, pamoja na tathmini za kina kutoka kwa wasafiri wenzako. Wageni wanaweza tu kuandika tathmini baada ya kukamilisha safari yao, kwa hivyo unajua maoni unayosoma yanatoka kwa mtu ambaye kwa kweli alikaa hapo.
Tathmini vipengele vya usalama
Ni vyema ukaangalia vigunduzi vya moshi na kaboni monoksidi kwenye nyumba hiyo, ambavyo unaweza kupata katika orodha ya vistawishi chini ya sehemu ya Usalama wa Nyumba.
Soma zaidi kuhusu vigunduzi vya moshi na kaboni monoksidi katika Kituo chetu cha Msaada.
Pata majibu ya maswali yako
Nyenzo yetu ya kutuma ujumbe kwa usalama ni njia salama na rahisi kwako ya kumuuliza Mwenyeji mtarajiwa maswali yoyote ambayo unaweza kuwa nayo kabla ya kuweka nafasi. Baada ya kuweka nafasi, unaweza pia kumtumia ujumbe ili kuratibu mchakato wa kuingia, kuuliza maswali ya ziada na kuwasiliana wakati wote wa safari yako.
Wasiliana na ulipe kila wakati kwenye Airbnb
Jiweke salama wewe mwenyewe, malipo yako na taarifa yako binafsi kwa kuendelea kutumia tovuti yetu iliyo salama katika mchakato wote—kuanzia mawasiliano hadi kuweka nafasi na malipo. Hupaswi kamwe kuombwa utume pesa kwa njia ya benki, kutoa taarifa za kadi ya benki au vinginevyo kumlipa Mwenyeji moja kwa moja. Ikiwa hii itatokea, tafadhali iripoti kwetu mara moja.
Fanya ukaguzi wa usalama
Mara baada ya kuwasili, ni vizuri kutafuta taarifa za usalama na vifaa vinavyofaa vya dharura, kama vile kizima moto au kisanduku chenye vifaa vya huduma ya kwanza. Ikiwa huna uhakika mahali kitu fulani kilipo, usisite kumuuliza Mwenyeji wako. Daima ni bora kuwa tayari.
Chunguza arifa za usafiri na maonyo ya eneo husika
Iwe unasafiri ukitumia Airbnb au la, ni jambo la busara kutafiti mahali uendako kabla ya wakati na uwasiliane na ubalozi wa eneo lako ili kupata maonyo yoyote ya usafiri au matakwa maalumu. Kwa mfano, wasafiri kutoka nchini Marekani wanapaswa kuwasiliana na Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ili kupata taarifa za viza na maonyo ya usafiri.
Pata maelezo zaidi kwenye ukurasa wetu wa usalama wa Mwenyeji na mgeni.
Tuko hapa kukusaidia
Ikiwa kuna jambo la dharura linaloendelea, tafadhali wasiliana na huduma za dharura za eneo lako au mamlaka za utekelezaji wa sheria ili upate usaidizi.
Kwa matatizo mengine ya usalama, tunapatikana saa 24 kwa siku. Soma zaidi kuhusu jinsi ya kuwasiliana nasi katika Kituo chetu cha Msaada.
Kumbuka: Katika hali ya dharura au ikiwa usalama wako binafsi unatishiwa, wasiliana mara moja na polisi wa eneo husika au huduma za dharura.
Makala yanayohusiana
- MgeniVidokezi vya usalama kwa Wenyeji wa sehemu za kukaaPata taarifa kuhusu majukumu ya kukaribisha wageni, pamoja na mazoea bora ili kuhakikisha wageni wako wana taarifa na nyenzo wanazohitaji.
- MgeniIkiwa hujihisi salama wakati wa safariIwapo unahisi kama unaweza kuwa hatarini au usalama wako binafsi unatishiwa, wasiliana na mamlaka za eneo husika mara moja.
- MgeniUsalama wa Wenyeji na wageniIli kusaidia kuhakikisha ukaaji salama, matukio na maingiliano, shughuli fulani na tabia haziruhusiwi katika jumuiya yetu.