Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Ni vidokezo vipi vya usalama kwa mwenyeji wa maeneo ya kukaa?

  Kuwa mwenyeji wa sehemu ya kukaa kuna majukumu kadhaa. Hizi ni baadhi ya nyenzo za kukusaidia unapoendelea.

  Wasiliana kwa njia ya busara

  Kila mara lipa na uwasiliane kupitia Airbnb. Tumia mfumo wa kutuma ujumbe wa Airbnb ili ujue wageni wako na ushiriki matarajio kuhusu safari au sehemu yako.

  Soma wasifu na tathmini za wageni wako watarajiwa na utafute nambari za simu zilizothibitishwa, mitandao ya kijamii iliyounganishwa na marejeo. Ikiwa wageni watarajiwa hawana uthibitisho wowote wa wasifu, unaweza kuwaomba wajaze baadhi yake.

  Ziamini hisia zako: Ikiwa una wasiwasi kuhusu nafasi iliyowekwa, usiikubali.

  Jaza sheria zako za nyumba na mwongozo wa nyumba

  Kujaza sheria zako za nyumba na mwongozo wa nyumba husaidia wageni kujua nini cha kutarajia. Jumuisha chochote ambacho ungependa watu wafahamu kabla hawajaweka nafasi—kwa mfano, iwapo (au wapi) kuvuta sigara kunaruhusiwa, iwapo maeneo fulani hayaruhusiwi kuingia, nenosiri lako la Wi-Fi, au ikiwa wageni wanapaswa kuvua viatu kabla ya kuingia ndani.

  Ikiwa janga linaathiri eneo lako na ungependa kusaidia kwa kuwakaribisha watu wanaohitaji makazi ya dharura, unaweza kutangaza sehemu yako bila malipo.

  Hakikisha una bima

  Mpango wa Bima ya Ulinzi ya Airbnb hutoa kinga ya dhima ya msingi ya hadi USD 1,000,000 kwa kila tukio iwapo kutatokea dai la mhusika mwingine la majeraha ya mwili au uharibifu wa mali zinazohusiana na ukaaji wa Airbnb.

  Unaweza pia kuzungumza na mtoa bima wako kuhusu kuongeza safu ya ziada ya ulinzi pamoja na bima ya mpangaji au mmiliki wa nyumba.

  Weka mahitaji ya tangazo lako

  Unaweza kuwahitaji wageni wakamilishe uthibitisho fulani kabla ya kuweka nafasi, kama vile kitambulisho kilichothibitishwa.

  Kuweka amana ya ulinzi kwenye tangazo lako pia kunaweza kukukinga katika tukio la ajali, kama vile divai iliyomwagika kwenye zulia.

  Soma makala za Airbnb za Kukaribisha Wageni kwa Kuwajibika

  Tunawahimiza wenyeji kufikiria kwa uangalifu kuhusu majukumu yao. Kukaribisha wageni hukupatia uzoefu mzuri, lakini kunaambatana na kiwango fulani cha kujizatiti. Tumekusanya makala za ukaribishaji wageni kwa kuwajibika ambazo zinaweza kukusaidia kuanza kujifunza kile kinachohitajika ili kuwa mwenyeji katika eneo lako.

  Kumbuka: Katika hali ya dharura, au ikiwa usalama wako binafsi unatishiwa, wasiliana na polisi wa eneo husika au huduma za dharura mara moja.

  Ulipata msaada uliohitaji?

  Makala yanayohusiana