Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Jinsi ya kufanya

Kujizatiti kwa Airbnb kuhusu ufikiaji na ujumuishaji wa walemavu

Ufikiaji kwenye tovuti na programu yetu

Tunaonyesha kujizatiti kwetu kwenye ufikiaji wa kidijitali wa tovuti na programu yetu katika njia tatu za msingi:

 • Timu mahususi za wahandisi, wabunifu, na mameneja wa programu za kiufundi zinazozijikita katika kusitawisha bidhaa ambazo kila mtu anaweza kutumia
 • Jitihada za kufuata viwango vya maendeleo vilivyowekwa na Miongozo ya Ufikiaji wa Maudhui ya Tovuti
 • Utafiti uliofanywa na watu wenye mahitaji ya ufikiaji ambao utaalamu na uzoefu wao unaathiri uendelezaji na maboresho ya bidhaa

Sehemu za kukaa zilizo na vipengele vya ufikiaji

Wenyeji wanaweza kuangazia vipengele vya ufikiaji kwenye nyumba zao na kuwapa wageni taarifa muhimu zinazowawezesha wageni kufanya maamuzi sahihi kuhusu iwapo nyumba hiyo inawafaa.

Vipengele vya ufikiaji vinajumuisha machaguo kama vile ufikiaji wa nyumba bila ngazi na vyumba anuwai, upana wa mlango unaozidi 32" (sm 81) na marekebisho ya ziada ya bafuni kama vile bafu lisilo na ngazi, kiti cha kuogea au vyuma vya kushikilia. Wenyeji wanaoweka vipengele vya ufikiaji kwenye tangazo lao wanatakiwa kupakia angalau picha moja kwa kila kipengele, ambayo hutathminiwa na timu yetu ili kukidhi miongozo yetu.

Wageni wana chaguo la kuchuja matokeo ya utafutaji kwa mchanganyiko wowote wa vipengele vya ufikiaji. Wageni wanaweza pia kuvinjari Aina ya Zinazofikika, mkusanyiko wa nyumba za kipekee zilizo na vipengele vya ufikiaji vilivyothibitishwa kama vile ufikiaji wa nyumba bila ngazi na angalau chumba kimoja cha kulala na bafu na marekebisho ya ziada kwenye bafu.

Matukio yenye vipengele vya ufikiaji

Wenyeji wanaweza kuangazia huduma anuwai zinazohusiana na kutembea, mawasiliano na hisia za Tukio lao ambazo zinaweza kuwezesha ushiriki wa wageni wenye mahitaji ya ufikiaji.

Kuanzia ufikiaji halisi wa mahali, hadi ikiwa mawasiliano ya lugha ya ishara ni chaguo, hadi ikiwa wageni wanaweza kufikia sehemu tulivu ya mapumziko, vipengele hivi vinawasilisha taarifa muhimu kwa wageni ambazo zinawasaidia kufanya uamuzi wao wa kuweka nafasi. Vipengele vyovyote vilivyoongezwa vinahitaji maelezo ya kina kutoka kwa Mwenyeji ambayo yanakidhi miongozo ya Airbnb. Wenyeji wanaweza pia kujiandikisha ili kuruhusu watu wanaosaidia wageni wenye ulemavu wajiunge kwenye Tukio bila gharama ya ziada kwa kutumia bei yetu ya Mtoa Huduma ya Ufikiaji.

Sawa na Sehemu za Kukaa, wageni wanaweza kuchuja matokeo yao ya utafutaji kulingana na vipengele vya ufikiaji ili kupata Tukio linalowafaa.

Wanyama wa huduma

Mwenyeji anahitajiwa kukubali mnyama wa huduma (hata kama haruhusu wanyama vipenzi), isipokuwa kwa sababu chache za afya na usalama. Pata maelezo zaidi kuhusu sera yetu ya mnyama wa huduma.

Sera ya Kutobagua

Jumuiya ya Airbnb imejengwa juu ya kanuni za ujumuishaji na heshima na hatuungi mkono ubaguzi wa aina yoyote kwa mujibu wa Sera yetu ya Kutobagua. Wenyeji hawawezi kumbagua au kumkataa mgeni kwa sababu ya ulemavu wake. Tafadhali ripoti aina yoyote ya ubaguzi ulioupitia kwenye Airbnb.

Wasiliana nasi

Tunaendelea kujitahidi kuifanya Airbnb ifikike zaidi. Kwa maswali yoyote ya ziada au wasiwasi wasiliana nasi ili kuongea na mwanatimu wetu.

Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

 • Mgeni

  Kukaribisha wageni wenye mahitaji ya ufikiaji

  Tunakaribisha na kuwasaidia watu wenye mahitaji ya ufikiaji. Wanajumuiya wetu hawa wanapaswa kuamini kwamba Wenyeji wao watatoa taarifa sahi…
 • Mgeni

  Sera ya Ufikiaji

  Jumuiya yetu imejengwa juu ya kanuni za ujumuishaji, kujisikia nyumbani na heshima, ambayo inajumuisha kukaribisha na kusaidia watu wenye ul…
Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili