Ruka kwenda kwenye maudhui
  Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Vitu vya msingi vya Airbnb

  Mnyama wa usaidizi ni nini?

  Katika Airbnb, mnyama anayetoa msaada huhusisha yoyote yafuatayo:

  Mnyama wa Huduma: Mbwa aliyefundishwa kufanya kazi au kushughulika kwa manufaa ya mtu mwenye ulemavu, ikiwa ni pamoja na ulemavu wa kimwili, kihisia, kiweledi, au kiakili. Wakati mwingine wanyama hawa hujulikana kama mbwa "macho", wanyama wasaidizi, wanyama wa huduma, au wanyama wa usaidizi. Mifano ya kazi ambazo mnyama wa huduma anaweza kufanya ni pamoja na, lakini sio tu:

  • Kuwasaidia watu ambao ni vipofu au wasioona vizuri katika kutembea na kufanya kazi nyingine
  • Kuwaarifu watu ambao ni viziwi au wasiosikia vizuri wakiwa katika uwepo wa watu au sauti
  • Kutoa ulinzi usio na ukali au katika kazi ya kuokoa
  • Kuvuta kiti cha magurudumu
  • Kumsaidia mtu wakati wa mshtuko
  • Kuwajulisha watu kuhusu kuwepo kwa mzio
  • Kutafuta na kurudisha vitu kama dawa au simu
  • Kutoa msaada wa kimwili na usaidizi wa uwiano na uthabiti kwa watu wenye ulemavu wa uhamaji
  • Kuwasaidia watu wenye ulemavu wa kiakili na wa neva kwa kuzuia au kukatiza tabia za msukumo au za uharibifu

  Mnyama wa Usaidizi wa Kihisia: Airbnb hufafanua wanyama wa usaidizi kwa kujumuisha Wanyama wa Usaidizi wa Kihisia. Hawa ni wanyama wanaotumiwa kama sehemu ya matibabu na / au tiba ili kusaidia kwa shughuli za kila siku za kikazi, sio tu aina fulani ya wanyama na si lazima wafundishwe ili kumsaidia mtu katika kazi fulani. Wakati mwingine wanyama hawa hujulikana kama wanyama wa faraja au wanyama wa tiba.

  Je, wenyeji wanahitajika kukubali wanyama wa usaidizi?

  Kwa kawaida, ndiyo, isipokuwa ikiwa kuna tishio kwa afya au usalama (angalia chini). Katika Airbnb, tunatambua kuwa wanyama wa usaidizi si sawa na wanyama vipenzi na wana jukumu muhimu sana kwa wamiliki wao. Kama ilivyoelezwa katika Sera ya Kutobagua, wenyeji wanatarajiwa kwa kiasi fulani kukubali uwekaji nafasi unaohusisha mnyama msaidizi kuwapo, hata ikiwa sheria ya tangazo/nyumba zinasema "wanyama vipenzi hawaruhusiwi".

  Pindi gani mwenyeji anaweza kumwambia mgeni amuondoe mnyama anayetoa huduma?

  Mwenyeji anaweza kumwambia mgeni aondoe mnyama wa huduma ikiwa:

  1. Mnyama hayuko chini ya udhibiti na msimamizi wa mnyama hajachukua hatua nzuri ya kumdhibiti
  2. Mnyama hajafunzwa kuenda haja nje ya nyumba

  Katika hali yoyote, mwenyeji lazima ampe nafasi mgeni kutumia nyumba bila mnyama ikiwa mgeni atachagua. Kumbuka kwamba ukizingatia nafasi yao katika kutoa huduma au msaada wa kihisia, wanyama wa usaidizi hawapaswi kuachwa peke yake kwenye tangazo.

  Je, wageni wanapaswa kutoa taarifa za uwepo wa wanyama wa usaidizi kabla ya kuweka nafasi?

  Hapana. Wakati wageni hawahitajiki kusema ikiwa kuna mnyama anayetoa msaada kabla ya kuweka nafasi, mara nyingi tunatia moyo kuwe na mawasiliano ya wazi ili kuhakikisha kuna ushirikiano mzuri kwa wahusika wote.

  Je, ni sawa kulipa ada ya ziada, au kuongeza ada ya usafi, ili kufidiwa uwepo wa wanyama wanaotoa usaidizi?

  La, chini ya Sera ya Kutobagua ya Arbnb, wenyeji hawapaswi kulipisha ada ya ziada kwa wageni wenye wanyama wa usaidizi.

  Je, ni sawa kuomba nyaraka za wanyama wa usaidizi?

  Airbnb haihitaji nyaraka wakati wa kusafiri na mnyama wa kutoa msaada. Nchini Marekani, wageni hawatakiwi kutoa nyaraka kuhusu wanyama wanaotoa huduma na hakuna mchakato wa kuthibitisha kisheria kwa wanyama wanaotoa huduma. Ikiwa mgeni atasema kwamba ana mnyama wa huduma, mwenyeji anaweza kuuliza:

  1. Ikiwa wanyama wa msaada huhitajika kwa sababu ya ulemavu
  2. Ni kazi gani au shughuli gani ambazo mnyama amefunzwa kufanya

  Ikiwa unasafiri nje ya Marekani, tafadhali kumbuka kwamba masharti yanaweza kuwa tofauti. Airbnb inatambua kwamba baadhi ya mamlaka zinaweza kupiga marufuku kwa wanyama wote, ikiwa ni pamoja na wanyama wa usaidizi, na wenyeji hawahitaji kuvunja sheria za serikali au kuchukua hatua ambazo zinaweza kuwatia matatani kisheria.

  Je, mwenyeji anaweza kuomba kulipwa ikiwa mnyama ameharibu nyumba yao kupita kiasi?

  Ndiyo, kwa njia sawa tu kwamba mwenyeji ana haki ya kubaki na kiasi au amana nzima ya ulinzi ya mgeni ili kulipa fidia kwa uharibifu unaosababishwa na mgeni. Ingawa ni jambo linaloeleweka kwa mwenyeji kutazamia kwamba mnyama anayetoa msaada amezoezwa na hatasababisha uharibifu wowote, Dhamana ya Mwenyeji na amana ya ulinzi bado iko chini ya uangalizi wa mwenyeji ikiwa ajali itatokea.

  Itakuwa vipi ikiwa nina wasiwasi wa hali ya afya au usalama kuhusiana na wanyama wa msaada?

  Ni muhimu kutambua ukweli wa kwamba mnyama wa msaada, iwe ni mnyama wa huduma au mnyama anayetoa usaidizi wa kihisia, huwa na jukumu muhimu katika uwezo wa mgeni wako wa kusafiri. Hata hivyo, ikiwa tangazo lako lina sehemu ya pamoja na mnyama wa usaidizi anaweza kuhatarisha afya au usalama wako na wengine (mf. mizio na wanyama vipenzi ambao hawawezi kuwa pamoja na wanyama wengine kwa sababu za kiusalama), hautahitaji kuwakaribisha wageni hao wenye wanyama wanaowasaidia. Tafadhali uwe wazi na mwenye heshima unapowasiliana na wageni kuhusu jambo hili. Tunashauri pia utoe taarifa kuhusu mizio yoyote au shaka kuhusu usalama wa wanyama wako katika sehemu ya pamoja iliyo katika maelezo ya tangazo lako ili uweze kuwajulisha wageni wanaotarajiwa.

  Nilikataliwa uwekaji nafasi kwa sababu nina mnyama wa msaada. Nifanye nini?

  Airbnb inachukua taarifa za ubaguzi katika jumuiya yetu kwa umakini sana.

  Ikiwa unaamini umebaguliwa kwenye tovuti yetu, tafadhali wasilisha ripoti kupitia fomu hii. Tafadhali toa maelezo hususa na mtaje mtu unayeamini amevunja Sera yetu ya Kutobagua. Unaweza pia kuripoti jumbe au maudhui mengine unayoamini yanakiuka sera yetu. Maelezo zaidi juu ya mchakato wa kutoa ripoti unapatikana hapa.

  Tutachunguza hali na huenda tukakuuliza utupe nyaraka zaidi za ziada. Tutatoa pia msaada wa kibinafsi wa kuweka nafasi ili kuhakikisha unapata sehemu ya kukaa.

  Ulipata msaada uliohitaji?
  Je, hupati unachohitaji?
  Pata maudhui ya makundi mahususi katika sehemu hizi nyingine za Kituo cha Msaada.