Ruka kwenda kwenye maudhui
  Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Je, masharti ya Airbnb juu ya silaha katika tangazo ni nini?

  Viwango na Matarajio yetu vinahitaji silaha zote zilizopo kwenye nyumba ya tangazo zihifadhiwe vizuri na kwa uthabiti. Kama silaha inaonekana wazi au inaweza kugunduliwa na wageni, wenyeji wanahitajika kueleza uwepo wake katika Sheria za Nyumba zao. Wageni vile vile wanahitajika kutoa taarifa ya na kupata idhini kwa silaha zozote zilizohifadhiwa kiusalama kabla ya kuweka nafasi, na wanapaswa kufanya hivyo kwa kutumia kipengele cha kutuma ujumbe.

  Kama taarifa ya awali ya silaha iliyohifadhiwa kiusalama haitolewi na mwenyeji au mgeni anapendelea kughairisha uwekaji nafasi, Airbnb itaruhusu ughairishaji bila adhabu.

  Zingatia: Silaha zote zilizopo kwenye nyumba lazima zihifadhiwe kiusalama bila kujali kama taarifa inayozihusu imetolewa. Watu wanaokiuka tarajio hili wanaweza wakasimamishwa au kuondolewa kwenye tovuti.

  Nini kinachukuliwa kama silaha

  Mtambo wowote ambao unaweza kutumika kufyatua kitu kinachoweza kufyatuliwa, unachukuliwa kama silaha. Hii ni pamoja na, lakini si tu: Silaha za moto za kawaida, bunduki zinazofyatuka kwa tumia mgandamizo wa hewa, vifaa vya kujilinda au kuzuia kama bastola za kushtua zinazotumia umeme, kinyunyizio cha pilipili, risasi za aina yoyote, na silaha za moto za bandia.

  Aina zinazokubalika za uhifadhi salama

  Masanduku au makabati yaliyofungwa na funguo na vifaa vya hifadhi vilivyo dhahiri vinakubalika kama chaguo za kuhifadhi. Hifadhi iliyo salama lazima ithibitishe kwamba watumiaji walio na ruhusa tu ndio wenye uwezo wa kuifikia.

  Ulipata msaada uliohitaji?