Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Jinsi ya kufanya
Mgeni

Pata sera ya kughairi kwa ajili ya sehemu yako ya kukaa

Labda unahitaji tu utulivu wa akili kabla ya kuweka nafasi au pengine unahitaji kughairi sasa hivi. Hivi ndivyo unavyoweza kupata sera ya kughairi kwa ajili ya sehemu yako ya kukaa:

Kabla ya kuweka nafasi

Unaweza kupata maelezo ya kughairi kwenye ukurasa wa tangazo na wakati wa mchakato wa kuweka nafasi—kabla hujalipa.

Baada ya kuweka nafasi

Sera na machaguo yako ya kughairi yanaweza kupatikana kwenye sehemu ya Safari zako wakati wowote. Bofya tu Onyesha maelezo ya safari kisha utapata Sera yako ya kughairi. Nyakati na tarehe tunazoonyesha za sera za kughairi zinategemea saa za eneo la tangazo. Tarehe za mwisho za kughairi ili kurejeshewa fedha hupimwa kuanzia wakati wa kuingia wa tangazo katika saa za eneo hilo au saa 9:00 alasiri ikiwa wakati wa kuingia haujabainishwa.

Ikiwa unataka kujua fedha utakazorejeshewa, anza kughairi nafasi uliyoweka na tutakuonyesha mchanganuo wa kina. Kulingana na muda wa ukaaji wako, unapoghairi na sera ya kughairi inayotumika kwenye nafasi uliyoweka, unaweza kurejeshewa sehemu ya fedha ikiwa utaghairi baada ya kuingia - pata maelezo zaidi kuhusu sera tofauti za kughairi.

Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi marejesho ya fedha yanavyofanya kazi kwa ajili ya kughairi. Kumbuka kwamba kiasi kinachorejeshwa kamwe hakitazidi kiasi halisi ulicholipa wakati wa kughairi—pata maelezo zaidi kuhusu kiasi kinachorejeshwa.

Sababu zisizozuilika

Je, dharura au janga la asili lilivuruga nafasi uliyoweka? Unaweza kustahiki kurejeshewa fedha kutokana na sababu zisizozuilika. Ikiwa unahitaji kughairi kwa sababu ya janga la COVID-19, pata maelezo kuhusu machaguo yako.

Sera za kughairi kwa ajili ya Wenyeji

Ikiwa wewe ni Mwenyeji au unataka kupata maelezo zaidi kuhusu sera za kughairi zinazopatikana, tafadhali rejelea sera za kughairi za tangazo lako.

Matatizo unayopata ukiwa safarini

Ukikumbana na matatizo unapofika kwenye nyumba uliyowekea nafasi ambayo mwenyeji hawezi kutatua haraka, unaweza kulindwa chini ya Sera yetu ya Kuweka Tena Nafasi na Kurejesha Fedha.

Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili