Ninaweza kutoaje ripoti ya ubaguzi kwa Airbnb?
Sera ya kutobagua ya Airbnb iliundwa ili kulinda jumuiya yetu na tunachukulia ripoti za ubaguzi kwa uzito sana.
Ili kuripoti maudhui kutoka kwenye wasifu, matangazo, au ujumbe ambao unaamini unakiuka sera yetu ya kutobagua, bofya au ubofye ikoni ya bendera .
Ili kuripoti ujumbe unapotumia programu ya Airbnb, bofya ikoni zaidi, kisha ubofye Ripoti.
Ili kuripoti tukio la ana kwa ana, au kutuma ripoti ya kina, wasiliana nasi. Tafadhali toa maelezo mahususi na umtambulishe mtu unayeamini amekiuka sera ya kutobagua.
Kumbuka: Katika hali ya dharura, au ikiwa usalama wako binafsi unatishiwa, wasiliana na polisi wa eneo husika au huduma za dharura mara moja.
Tunachofanya na ripoti
Timu yetu ya usaidizi wa jumuiya inashughulikia ripoti na inaweza kufuatilia nyaraka za ziada. Ikihitajika, pia tutatoa usaidizi mahususi wa kuweka nafasi ili kukutafutia sehemu tofauti ya kukaa.
Ikiwa mtu amekiuka sera yetu ya kutobagua tutachukua hatua ya kurekebisha. Hii inaweza kujumuisha maonyo, kusimamishwa, au kuondolewa kwa akaunti.
Tafadhali kumbuka kwamba, kwa sababu za faragha, hatuwezi kushiriki matokeo ya uchunguzi huu.
Makala yanayohusiana
- Airbnb inatumia data jinsi gani kufanya kazi dhidi ya ubaguzi wa rangi?Pata maelezo zaidi kuhusu mbinu tunayotumia ili kusaidia kutengeneza vipengele vipya na sera ili kushughulikia ubaguzi wa rangi.
- MgeniSera ya KutobaguaTafadhali tathmini Sera yetu ya Kutobagua.
- MgeniKupambana na chuki, unyanyasaji na ubaguziTunataka Wenyeji na wageni wetu wawe na sehemu za kukaa na Matukio yasiyokuwa na unyanyasaji na ubaguzi.