Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa

  Omba kurejeshewa fedha

  Ikiwa ungependa kuomba kurejeshewa fedha kabla au baada ya safari yako, maombi ya kurejeshewa fedha za kiasi chochote yanaweza kushughulikiwa kupitia Kituo chetu cha Usuluhishi.

  Tunapendekeza ujadili kiasi chochote cha fedha za kurejeshewa na Mwenyeji wako kupitia uzi wako wa ujumbe wa Airbnb kabla ya kuwasilisha ombi katika Kituo cha Usuluhishi. Hata hivyo, ikiwa wewe na Mwenyeji wako mmeshindwa kufikia makubaliano ndani ya saa 72, utaona chaguo la kuiomba Airbnb isaidie kuwapatanisha.

  Kumbuka: Una hadi siku 60 baada ya tarehe ya kutoka ya nafasi uliyoweka kuwasilisha ombi kwenye Kituo cha Usuluhishi.

  Ikiwa unakumbana na tatizo wakati wa ukaaji wako, unaweza kumtumia Mwenyeji wako ombi la kurejeshewa fedha kupitia programu yako ya Airbnb. Ni muhimu kutuma ombi hilo ndani ya saa 24 baada ya kugundua tatizo hilo la kusafiri.

  Ulipata msaada uliohitaji?