Mapendekezo yataonyeshwa baada ya kuandika kwenye sehemu ya utafutaji. Tumia mishale ya juu na chini ili kutathmini. Tumia ingia ili kuchagua. Ikiwa maneno yaliyochaguliwa ni kifungu cha maneno, kifungu hicho kitawasilishwa kwenye utafutaji. Ikiwa pendekezo hilo ni kiunganishi, kivinjari kitaelekeza kwenye ukurasa huo.
Jinsi ya kufanya
Mwenyeji

Familia za wenyeji zilizo na watoto

Familia huwa na mchanganyiko wa watu mbalimbali na wageni hutafuta maeneo ambayo yanaweza kuwakaribisha wote, ikiwemo watoto wadogo zaidi. Inapendeza zaidi ikiwa unaweza kutoa vistawishi maalumu au vifaa vya usalama ambavyo familia zinaona vinafaa na ina bonasi ya kufanya eneo lako livutie zaidi kwa watu wengi zaidi. Haya ni baadhi ya mapendekezo:

  • Kigundua moshi na kaboni monoksidi (CO) kinachofanya kazi kwenye kila ghorofa na katika maeneo yote ya kulala
  • Kitanda cha mtoto kinachobebeka chenye shuka linalotoshea vizuri, kilichowekwa mbali na madirisha na luva
  • Vizuizi vya usalama vinavyoweza kuondolewa kwa ajili ya ngazi na ikiwa una bwawa, kizuizi kinacholizunguka
  • Luva za dirisha zisizo na kamba
  • Hifadhi salama kwa ajili ya bidhaa zote za kufanyia usafi za nyumba, paketi za sabuni iliyo majimaji, dawa na kemikali
  • Majiko, mabirika na vitu vingine vinavyohatarisha usalama vinapaswa kuwa na makufuli ya watoto au kuwekwa mbali na watoto
  • Weka televisheni bapa ukutani au utumie fanicha za chini na zilizo imara ili kuwekea televisheni nzito
  • Tumia miango, magango au vishikio vya kuta ili kukaza fanicha zisizo imara na zenye uzito upande wa juu ili kuepuka uangukaji
  • Weka hali-joto ya hita za maji isiyozidi nyuzi 120 Farenhaiti ili kuepuka kuungua kwa maji moto

Jamuiya ya Airbnb imejizatiti kujenga ulimwengu ambapo familia kutoka katika kila mazingira zinahisi kukaribishwa na kuheshimiwa, bila kujali wamesafiri umbali kiasi gani kutoka nyumbani. Tathmini Sera yetu ya Kutobagua kwa taarifa zaidi.

Unaweza pia kutathmini vidokezi hivi vya usalama ambavyo ni muhimu kwa sehemu zote za kukaa na si tu zile zenye watoto na/au watoto wachanga. 

Shiriki taarifa za usalama zinazofaa kwa familia

  1. Nenda kwenye Matangazo kisha uchague kadi ya tangazo unalotaka kubadilisha
  2. Chini ya Sehemu yako, sogeza chini hadi kwenye Usalama wa wageni
  3. Bofya Usalama wa wageni
  4. Chagua kutoka kwenye machaguo, Mazingatio ya usalama, Vifaa vya usalama, na Taarifa za nyumba
Je, makala hii ilikusaidia?

Makala yanayohusiana

  • Mwenyeji

    Wanyama hatari

    Tafuta sheria kwa wenyeji kuhusu kufuga wanyama hatari.
  • Mwenyeji

    Jinsi matangazo yanavyoainishwa

    Pata maelezo kuhusu aina za Airbnb ili kuelewa jinsi ya kuamua tangazo lako lipo kwenye aina gani.
  • Mgeni

    Kusafiri na watoto

    Ndiyo, watoto wanaweza kusafiri kwenye Airbnb, lakini baadhi ya Wenyeji wamebainisha kuwa sehemu yao huenda isiwe salama au isiwafae watoto …
Pata msaada kuhusu nafasi ulizoweka, akaunti na kadhalika.
Ingia au ujisajili