Ruka kwenda kwenye maudhui
  Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Habari za hivi punde kuhusu COVID-19
  Ili upate machaguo ya kughairi na kurejesha fedha, chagua nafasi iliyowekwa kwenye ukurasa wa Safari. Sera yetu ya sababu zisizozuilika inatumika tu kwenye nafasi fulani zilizowekwa. Tunatoa habari za hivi punde tarehe 1 na 15 ya kila mwezi.

  Itakuaje kama nitahitaji kughairi kwa sababu ya dharura au hali isiyoepukika?

  Tafadhali kumbuka: Makala haya hayazungumzii hali zinazohusiana na janga la virusi vya korona (COVID-19). Pitia makala yetu ya kina ya sababu zisizozuilika za COVID-19 ili upate maelezo zaidi kuhusu ujumuishaji wa hali zinazohusiana na COVID-19 na kwa umahususi zaidi, masharti yanayotumika kwa uwekaji nafasi uliofanyika baada ya tarehe 14 Machi, 2020.

  Jinsi inavyofanya kazi

  Tunaweza kukurejeshea fedha au tukusamehe adhabu za kughairi iwapo utalazimika kughairi kutokana na hali zisizotarajiwa ambazo ziko nje ya udhibiti wako. Hapa chini kuna orodha ya hali zinazojumuishwa kwenye Sera yetu ya Sababu Zisizozuilika. Kabla ya kughairi, hakikisha kwamba hali yako imejumuishwa katika orodha iliyo hapa chini na kwamba unaweza kutoa hati zinazohitajika.

  Ni muhimu kukumbuka kwamba kughairi bila adhabu kunapatikana tu kwa ajili ya sababu zisizozuilika zinazotokea kabla ya tarehe rasmi ya kuingia kwenye nyumba uliyoweka nafasi. Kwa kuongezea, Sera yetu ya Sababu Zisizozuilika haitumiki kwenye nafasi zilizowekwa za Luxe au Luxury Retreats, ambazo zinadhibitiwa na Sera ya Kurejesha Fedha ya Mgeni ya Luxe.

  Hali ambazo zinahitaji nyaraka

  Kifo cha mwenyeji, mgeni, au mwenyeji mwenza wake, mgeni wa ziada, mtu wa karibu wa familia, au mtunzaji. Utaombwa utoe mojawapo ya nyaraka hizi:

  • Cheti cha kifo
  • Tangazo la tanzia
  • Tangazo la habari linalomtaja marehemu
  • Ripoti ya polisi

  Ugonjwa au jeraha hatari lisilotarajiwa linalomwathiri mwenyeji au mshiriki wa kundi linalosafiri. Utaombwa kutoa taarifa ya daktari inayothibitisha kwamba mtu huyo hawezi kukaribisha wageni au kusafiri kwa sababu ya ugonjwa au jeraha baya ambalo halikutarajiwa. Taarifa hiyo lazima pia iwe na tarehe ya baada ya kuwekwa kwa nafasi hiyo na itolewe ndani ya siku 14 baada ya kughairiwa. Kwa wakati huu, hali zilizokuwepo awali ambazo mtumiaji alizifahamu wakati wa kuweka nafasi hazishughulikiwi na Sera yetu ya Sababu Zisizozuilika.

  Majukumu yaliyoamriwa na serikali ikiwemo kushiriki kwenye baraza la kimahakama, vizuizi vya kusafiri, kwenda mahakamani na kuwekwa jeshi. Utaombwa kutoa nakala ya taarifa rasmi yenye tarehe iliyo baada ya tarehe ya kuweka nafasi, ikiwemo jina la mtu anayetimiza jukumu.

  Masuala yasiyotarajiwa kuhusu uharibifu wa mali, udumishaji na vistawishi kwenye nyumba ya Airbnb yanayoifanya isiwe salama kukaribishia wageni, au yanayowazuia wageni kupata vistawishi vya msingi kama maji ya bomba. Hii haijumuishi ukarabati uliokuwa umepangwa. Utaombwa utoe nyaraka zote zifuatazo:

   Uthibitisho kwamba suala hilo linashughulikiwa
  • Makadirio ya muda ambao litakuwa limekamilika kushughulikiwa
  • Ankara ya ukarabati unaofanywa
  • Picha za uharibifu

  Usimamishwaji wa usafiri unaofanya isiwezekane kusafiri kwenda kwenye eneo lako, ikiwemo kufungwa kwa barabara na kughairiwa kwa safari za ndege ambapo hakuna njia mbadala za usafiri. Hii inajumuisha ufungaji na ughairi unaosababishwa na majanga ya asili kama matetemeko ya ardhi na dhoruba kali. Utaombwa kutoa taarifa ya kufungwa kwa barabara, au nyaraka za kampuni ya ndege zinazoonyesha kwamba safari ya ndege imeghairiwa na nyaraka zinazounga mkono zikithibitisha kuwa haiwezekani kusafiri kwenda kwenye eneo lako.

  Treni, basi, au kughairiwa kwa feri ambapo safari mbadala hazikuwepo kwa siku hiyohiyo. Utaombwa kutoa nyaraka zinazoonyesha wazi kwamba mtoa huduma za usafiri hakuwa akifanya kazi siku hiyo, kama vile picha ya skrini ya tovuti ya kampuni au kiunganishi cha kwenda kwenye taarifa rasmi ya mtoa huduma za usafiri.

  Hali ambazo zinahitaji tathmini mahususi

  Hakuna nyaraka zinazohitajika kwa hali hizi, lakini timu yetu mahususi itatathmini kila kisa ili kuhakikisha kuwa umeathirika moja kwa moja.

  Nafasi za Open Homes ambazo zimeghairiwa. Taarifa zaidi kuhusu Open Homes.

  Misiba ya asili, shughuli za kigaidi, na machafuko ya kiraia/kisiasa yanayomzuia mgeni kusafiri kwenda au kutoka kwenye eneo, au yanayofanya isiwe salama kukaribisha wageni.

  Magonjwa au maradhi ya mlipuko yanayoathiri ghafla eneo fulani au kundi zima la watu. Hii haijumuishi magonjwa yaliyopo ambayo yanajulikana kuwepo kwenye eneo—kwa mfano, malaria nchini Thailand au homa ya dengue Hawaii. Mabadiliko yoyote kwenye sera yetu kuhusu mlipuko wa ugonjwa, na wigo wa matumizi ya sera, yataamuliwa kulingana na matangazo ya Shirika la Afya Duniani na mamlaka za eneo.

   Vizuizi vya kusafiri vilivyowekwa na serikali, shirika la kutekeleza sheria, au jeshi ambavyo vinazuia kusafiri kwenda au kutoka kwenye nyumba au eneo la tukio.

   Ushauri kuhusu hatari kwa usalama na ulinzi uliotolewa kuhusiana na eneo ilipo nyumba au tukio au eneo ambapo mgeni anaanzia safari ya kuondoka.

   Ukosefu wa huduma muhimu unaoathiri eneo la nyumba au tukio.

   Mabadiliko kwenye mahitaji ya viza au pasipoti yanayofanya isiwezekane kusafiri kwenye eneo. Hii haijumuishi hati za kusafiri zilizopotea au zilizokwisha muda.

   Unachotarajiwa kufanya

   Ikiwa umethibitisha kuwa hali yako inakidhi matakwa yaliyo hapo juu, kwanza ghairi nafasi ya ukaaji wa nyumba uliyoweka au Tukio la Airbnb. Ikiwa nafasi uliyoweka ipo miongoni mwa hali zisizozuilika zinazotambuliwa, utaarifiwa kwamba unaweza kughairi nafasi uliyokuwa umeweka bila adhabu yoyote na utarejeshewa fedha zote kama wewe ni mgeni.

   Ikiwa nafasi uliyoweka haitimizi masharti moja kwa moja, endelea mbele na ughairi uwekaji nafasi wako kisha uwasiliane nasi ili ufungue madai. Tutakuongoza katika hatua zinazofuata, ambazo zitajumuisha kuwasilisha nyaraka zozote zinazohitajika na kusubiri timu yetu itathmini suala lako. Madai lazima yawasilishwe ndani ya siku 14 baada ya kughairi.

   Makala yanayohusiana
   Ulipata msaada uliohitaji?

   Ingia ili kupata usaidizi mahususi

   Pata msaada na kutoridhishwa kwako, akaunti, na zaidi.
   Jisajili