Ruka kwenda kwenye maudhui
  Nenda mbele ili upate matokeo yaliyopendekezwa
  Habari za hivi punde kuhusu COVID-19
  Ili upate machaguo ya kughairi na kurejesha fedha, chagua nafasi iliyowekwa kwenye ukurasa wa Safari. Sera yetu ya sababu zisizozuilika inatumika tu kwenye nafasi fulani zilizowekwa. Tunatoa habari za hivi punde tarehe 1 na 15 ya kila mwezi.

  Sera ya Sababu Zisizozuilika

  Kumbuka: Makala haya hayazungumzii hali zinazohusiana na janga la virusi vya korona (COVID-19). Tathmini makala yetu ya sababu zisizozuilika za COVID-19 ili kupata maelezo kuhusu wigo wa hali zinazohusu COVID-19 na hasa vikomo vya wigo kwa ajili ya nafasi zilizowekwa baada ya tarehe 14 Machi, 2020.

  Sera hii inatumika kwenye uingiaji utakaofanyika mnamo au kabla ya tarehe 19 Januari, 2021. Kwa uingiaji utakaofanyika baada ya tarehe hiyo, sera iliyosasishwa inayopatikana hapa chini itatumika.

  Itatekelezwa hadi: Tarehe 19 Januari, 2021

  Jinsi inavyofanya kazi

  Tunaweza kukurejeshea fedha au tukusamehe adhabu za kughairi iwapo utalazimika kughairi kutokana na hali zisizotarajiwa ambazo ziko nje ya udhibiti wako. Hapa chini kuna orodha ya hali zinazojumuishwa kwenye Sera yetu ya Sababu Zisizozuilika. Kabla ya kughairi, hakikisha kwamba hali yako imejumuishwa katika orodha iliyo hapa chini na kwamba unaweza kutoa hati zinazohitajika.

  Ni muhimu kukumbuka kwamba kughairi bila adhabu kunapatikana tu kwa ajili ya sababu zisizozuilika zinazotokea kabla ya tarehe rasmi ya kuingia kwenye nyumba uliyoweka nafasi. Aidha, Sera yetu ya Sababu Zisizozuilika haitumiki kwenye nafasi zilizowekwa za Luxe au Luxury Retreats, ambazo zinadhibitiwa na Sera ya Kurejesha Fedha ya Mgeni wa Luxe.

  Hali ambazo zinahitaji nyaraka

  Kifo cha mwenyeji, mgeni, au mwenyeji mwenza wake, mgeni wa ziada, mtu wa karibu wa familia, au mlezi. Utaombwa utoe mojawapo ya nyaraka hizi:

  • Cheti cha kifo
  • Tangazo la tanzia
  • Tangazo la habari linalomtaja marehemu
  • Ripoti ya polisi

  Ugonjwa au jeraha hatari lisilotarajiwa linalomwathiri mwenyeji au mshiriki wa kundi linalosafiri. Utaombwa kutoa taarifa ya daktari inayothibitisha kwamba mtu huyo hawezi kukaribisha wageni au kusafiri kwa sababu ya ugonjwa au jeraha baya ambalo halikutarajiwa. Taarifa hiyo lazima pia iwe na tarehe ya baada ya kuwekwa kwa nafasi hiyo na itolewe ndani ya siku 14 baada ya kughairiwa. Kwa wakati huu, hali zilizokuwepo awali ambazo mtumiaji alizifahamu wakati wa kuweka nafasi hazishughulikiwi na Sera yetu ya Sababu Zisizozuilika.

  Majukumu yaliyoamriwa na serikali ikiwemo kushiriki kwenye baraza la kimahakama, vizuizi vya kusafiri, kwenda mahakamani na kuwekwa jeshi. Utaombwa kutoa nakala ya taarifa rasmi yenye tarehe iliyo baada ya tarehe ya kuweka nafasi, ikiwemo jina la mtu anayetimiza jukumu.

  Matatizo yasiyotarajiwa kuhusu uharibifu wa mali, udumishaji na vistawishi kwenye nyumba ya Airbnb yanayoifanya isiwe salama kukaribishia wageni, au yanayowazuia wageni kupata vistawishi vya msingi kama vile maji ya bomba. Hii haijumuishi ukarabati uliokuwa umepangwa. Utaombwa utoe nyaraka zote zifuatazo:

   Uthibitisho kwamba tatizo hilo linashughulikiwa
  • Makadirio ya muda ambao litakuwa limekamilika kushughulikiwa
  • Ankara ya ukarabati unaofanywa
  • Picha za uharibifu

  Usimamishwaji wa usafiri unaofanya isiwezekane kusafiri kwenda kwenye eneo lako, ikiwemo kufungwa kwa barabara na kughairiwa kwa safari za ndege ambapo hakuna njia mbadala za usafiri. Hii inajumuisha ufungaji na ughairi unaosababishwa na majanga ya asili kama matetemeko ya ardhi na dhoruba kali. Utaombwa kutoa taarifa ya kufungwa kwa barabara, au nyaraka za kampuni ya ndege zinazoonyesha kwamba safari ya ndege imeghairiwa na nyaraka zinazounga mkono zikithibitisha kuwa haiwezekani kusafiri kwenda kwenye eneo lako.

  Treni, basi, au kughairiwa kwa feri ambapo safari mbadala hazikuwepo kwa siku hiyohiyo. Utaombwa kutoa nyaraka zinazoonyesha wazi kwamba mtoa huduma za usafiri hakuwa akifanya kazi siku hiyo, kama vile picha ya skrini ya tovuti ya kampuni au kiunganishi cha kwenda kwenye taarifa rasmi ya mtoa huduma za usafiri.

  Hali ambazo zinahitaji tathmini mahususi

  Hakuna nyaraka zinazohitajika kwa hali hizi, lakini timu yetu mahususi itatathmini kila kisa ili kuhakikisha kuwa umeathirika moja kwa moja.

  Nafasi za Open Homes ambazo zimeghairiwa. Taarifa zaidi kuhusu Open Homes.

  Majanga ya asili, shughuli za kigaidi na machafuko ya kiraia/kisiasa yanayomzuia mgeni kusafiri kwenda au kutoka kwenye eneo, au yanayofanya isiwe salama kukaribisha wageni.

  Magonjwa au maradhi ya mlipuko yanayoathiri ghafla eneo fulani au kundi zima la watu. Hii haijumuishi magonjwa yaliyopo ambayo yanajulikana kuwepo kwenye eneo—kwa mfano, malaria nchini Thailand au homa ya dengue huko Hawaii. Mabadiliko yoyote kwenye sera yetu kuhusu mlipuko wa ugonjwa na wigo wa matumizi ya sera, yataamuliwa kulingana na matangazo ya Shirika la Afya Duniani na mamlaka za eneo husika.

   Vizuizi vya kusafiri vilivyowekwa na serikali, shirika la kutekeleza sheria, au jeshi ambavyo vinazuia kusafiri kwenda au kutoka kwenye nyumba au eneo la tukio.

   Ushauri kuhusu hatari kwa usalama na ulinzi uliotolewa kuhusiana na eneo ilipo nyumba au tukio au eneo ambapo mgeni anaanzia safari ya kuondoka.

   Ukosefu wa huduma muhimu unaoathiri eneo la nyumba au tukio.

   Mabadiliko kwenye mahitaji ya viza au pasipoti yanayofanya isiwezekane kusafiri kwenye eneo. Hii haijumuishi hati za kusafiri zilizopotea au zilizokwisha muda.

   Unachotarajiwa kufanya

   Ikiwa umethibitisha kuwa hali yako inakidhi matakwa yaliyo hapo juu, kwanza ghairi nafasi ya ukaaji wa nyumba uliyoweka au Tukio la Airbnb. Ikiwa nafasi uliyoweka ipo miongoni mwa hali zisizozuilika zinazotambuliwa, utaarifiwa kwamba unaweza kughairi nafasi uliyokuwa umeweka bila adhabu yoyote na utarejeshewa fedha zote kama wewe ni mgeni.

   Ikiwa nafasi uliyoweka haitimizi masharti moja kwa moja, endelea mbele na ughairi uwekaji nafasi wako kisha uwasiliane nasi ili ufungue madai. Tutakuongoza katika hatua zinazofuata, ambazo zitajumuisha kuwasilisha nyaraka zozote zinazohitajika na kusubiri timu yetu itathmini suala lako. Madai lazima yawasilishwe ndani ya siku 14 baada ya kughairi.

   Kumbuka: Sera ya Sababu Zisizozuilika iliyo hapa chini inatumika kwa uingiaji wote unaofanyika mnamo au baada ya tarehe 20 Januari, 2021. Kwa ajili ya uingiaji wote kabla ya tarehe 20 Januari, 2021, Sera iliyopo hapo juu itaendelea kutumika. Matumizi ya Sera hii kwenye COVID-19 hayatabadilika wakati Sera mpya itaanza kutumika tarehe 20 Januari, 2021 na hali nyingi zinazohusiana na COVID-19 zitaendelea kutojumuishwa.

   Sera ya Sababu Zisizozuilika

   Tarehe ya kuanza: Tarehe 20 Januari, 2021

   Muhtasari

   Sera hii ya Sababu Zisizozuilika inaelezea jinsi kughairi kunavyoshughulikiwa wakati matukio yasiyotarajiwa yaliyo nje ya udhibiti wako yanatokea baada ya kuweka nafasi na kufanya isiwezekane au kinyume cha sheria kukamilisha nafasi uliyoweka. Sera hii inatumika kwenye nafasi zilizowekwa kwa ajili ya malazi na pia Matukio.

   Sera hii inaporuhusu kughairi, inadhibiti na kuchukua nafasi ya kwanza juu ya sera ya kughairi ya nafasi iliyowekwa. Wageni ambao wameathiriwa na tukio linaloshughulikiwa na Sera hii wanaweza kughairi nafasi waliyoweka na kupokea, kulingana na hali, rejesho la pesa taslimu, salio la safari na au mafao mengine. Wenyeji ambao wameathiriwa na tukio linaloshughulikiwa na Sera hii wanaweza kughairi bila athari mbaya, lakini, kulingana na hali, kalenda zao zinaweza kuzuiwa kwa tarehe za nafasi iliyowekwa ambayo ilighairiwa.

   Ni matukio gani yanayoshughulikiwa

   Sera hii inatumia neno "Tukio” kurejelea hali zifuatazo ambazo hufanyika baada ya kuweka nafasi, hazitabiriki wakati wa kuweka nafasi na huzuia au hukataza kisheria kukamilishwa kwa nafasi iliyowekwa.

   Mabadiliko kwenye mahitaji ya serikali kuhusu kusafiri. Mabadiliko yasiyotarajiwa kwa mahitaji ya viza au pasipoti yanayowekwa na wakala wa serikali ambayo inazuia kusafiri kwenda kwenye eneo la safari. Hii haijumuishi nyaraka za kusafiri zilizopotea au zilizokwisha muda wake au hali nyingine za kibinafsi zinazohusiana na idhini ya mgeni kusafiri.

   Dharura na magonjwa ya mlipuko yaliyotangazwa. Dharura za eneo husika au za kitaifa, magonjwa ya mlipuko, magonjwa ya janga na dharura za afya ya umma zilizotangazwa na serikali. Hii haijumuishi magonjwa ambayo ni ya kawaida au yanayohusishwa sana na eneo—kwa mfano, malaria nchini Thailand au homa ya dengue huko Hawaii.

   Vizuizi vya kusafiri vya serikali. Vizuizi vya kusafiri vilivyowekwa na wakala wa serikali ambavyo vinazuia au kukataza kusafiri kwenda, kukaa, au kurudi kutoka kwenye eneo la Tangazo. Hii haijumuishi ushauri wa kusafiri ambao si sharti na mwongozo kama huo wa serikali.

   Vitendo vya kijeshi na uhasama mwingine. Vitendo vya vita, uhasama, uvamizi, vita vya wenyewe kwa wenyewe, ugaidi, milipuko, mabomu, uasi, ghasia na machafuko ya kiraia.

   Majanga ya asili. Majanga ya asili, matendo ya Mungu, kukatika kwa kiwango kikubwa kwa huduma muhimu za umma, milipuko ya volkano, tsunami na matukio mengine ya hali ya hewa yaliyo mabaya na yasiyo ya kawaida. Hii haijumuishi hali ya hewa au hali ya asili ambayo ni ya kawaida kiasi cha kutosha kutabiriwa katika eneo hilo—kwa mfano, vimbunga vinavyotokea wakati wa msimu wa vimbunga huko Florida.

   Kile kisichoshughulikiwa

   Kila kitu kingine. Sera hii inaruhusu tu kughairi kwa ajili ya Matukio yaliyoelezwa hapo juu. Kila kitu kingine hakijumuishwi. Mifano ya hali ambazo Sera hii hairuhusu kughairi ni pamoja na: ugonjwa usiotarajiwa, maradhi, au jeraha; majukumu ya serikali kama kushiriki kwenye jopo la wazee wa mahakama, kufika mahakamani au majukumu ya kijeshi; ushauri wa kusafiri au mwongozo mwingine wa serikali (ambao haufikii marufuku au katazo la kusafiri); kughairi au kuratibu upya hafla iliyowekewa nafasi hiyo; na usumbufu wa usafiri ambao hauhusiani na Tukio linaloshughulikiwa kama vile kufungwa kwa barabara na pia kughairiwa kwa safari za ndege, treni, basi na feri. Ukighairi nafasi uliyoweka katika hali hizi, kiasi kinachorejeshwa kitaamuliwa na sera ya kughairi inayotumika kwenye nafasi uliyoweka.

   Nini cha kufanya baadaye

   Ikiwa tutakuarifu au kuchapisha taarifa inayothibitisha kuwa Sera hii inatumika kwenye nafasi uliyoweka, tafadhali fuata maelekezo ya kughairi ambayo tunatoa. Wakati tumekuarifu au kuchapisha taarifa kuhusu jinsi Sera hii inavyotumika, unapaswa kuwa na chaguo la kughairi chini ya Sera hii kwa kwenda kwenye ukurasa wako wa Safari na kughairi nafasi iliyowekwa iliyoathiriwa. Ikiwa unaamini Sera hii inatumika kwenye nafasi uliyoweka, lakini hatujakuarifu au kuchapisha taarifa kuhusu Tukio hilo, tafadhali wasiliana nasi ili kughairi nafasi uliyoweka. Katika visa vyote, unapaswa kuwa tayari kutoa nyaraka ambazo zinaonyesha jinsi Tukio hilo limekuathiri wewe au nafasi uliyoweka.

   Ikiwa una maswali, tafadhali wasiliana nasi.

   Mambo mengine ya kufahamu

   Sera hii inatumika kwenye nafasi zote zilizowekwa zenye tarehe ya kuingia ya siku hiyo au baada ya tarehe ya kuanza kutumika. Sera hii haitumiki kwenye nafasi zilizowekwa za Luxe, ambazo zinadhibitiwa na Sera ya Kurejesha Fedha ya Mgeni ya Luxe.

   Makala yanayohusiana
   Ulipata msaada uliohitaji?

   Ingia ili kupata usaidizi mahususi

   Pata msaada na kutoridhishwa kwako, akaunti, na zaidi.
   Jisajili