Jumuiya yetu pana ya kimataifa huwezesha Airbnb kufanya kazi

Kujenga tovuti jumuishi ya wenyeji na wageni wote ndilo lengo letu kuu, na tunatia juhudi kila wakati kuiboresha.

Katika kiini cha misheni yetu ni dhana kuwa watu ni wazuri na kila jumuiya ni eneo ambapo unaweza kujihisi nyumbani. Ninaamini kwa dhati kwamba [ubaguzi] ni changamoto kuu zaidi tunayokumbana nayo kama kampuni. Hukata kiini cha maelezo kutuhusu na maadili tunayotetea.
Brian Chesky
Brian Chesky
Mkurugenzi Mtendaji (CEO), mwanzilishi mwenza wa Airbnb

Ubaguzi hauna nafasi kwenye tovuti yetu
Kutoka kwenye godoro la hewa katika fleti ya mwanzilishi wetu hadi kwa jumuiya ya kimataifa ya mamilioni, Airbnb daima inazidi kukua na hivyo ni wajibu wetu kuhakikisha kuwa wenyeji na wageni wanaweza kutumia tovuti yetu bila kukumbana na dhuluma au ubaguzi. Tunafanya kazi kila wakati ili kupata matokeo bora zaidi na tunashukuru kwa fursa ya kusikiza na kujifunza kutoka kwa jumuiya yetu.
Mwaka 2016 tulimwomba Laura Murphy, aliyekuwa mkuu wa Ofisi ya Kisheria ya Washington D.C., kuongoza tathmini ya kila kipengele cha uanuwai na ujumuishaji kwenye tovuti ya Airbnb. Baada ya miezi ya utafiti na ushirikiano tumetoa ripoti ambayo tunaalika kila mmoja wa jumuiya yetu kuisoma.
Shukrani kwa tathmini ya Laura na uhusishaji wa timu nyingi hapa kwenye Airbnb, tumetangaza masasisho kadhaa. Makubaliano yetu mapya ya Jumuiya, Sera ya Kutobagua iliyo dhabiti na maendeleo ya timu ya kudumu iliyojitolea kupigana na upendeleo huku ikihimiza uanuwai ni hatua chache tu tunazochukua kupigana na upendeleo. Mchango wa jumuiya yetu ya kimataifa ulikuwa muhimu kwa ripoti hii na kwa maendeleo ya mipango hii. Kazi hii ni mwanzo tu wa kujizatiti kwetu kunakoendelea kwa kushughulikia changamoto hizi na tunatarajia kushiriki habari zaidi, ushirikiano na rasilimali zaidi hapa.

Wenyeji na wageni wetu wanaongoza njia
Daima tunafanya juhudi kujenga tovuti bora zaidi, na ni usaidizi wa pamoja wa wenyeji wetu, wageni na jumuiya ya kimataifa ambayo hufanya kila tukio la Airbnb kuwezekana. Tunaamini katika kusherehekea hadithi hizi na kushiriki jinsi ambavyo hutuhamasisha kufikiria tena inavyomaanisha kujisikia nyumbani tunapotia bidii zaidi katika kumaliza ubaguzi.

Kila mwenyeji anapaswa kufikia zana za ufanisi
Kuanzia kusimamia kalenda na mawasiliano hadi kuwakaribisha wageni nyumbani kwao, wenyeji wetu wanafanya kazi kwa bidii kuwezesha kuwa na uzoefu wa pekee wa safari na mahusiano ya watu. Tuko hapa kutoa usaidizi kwa kazi hiyo ya bidii kwa rasilimali ili kusaidia wenyeji wetu.

Kuelewa upendeleo na kujisikia nyumbani

Njia moja tunayoitumia kupigana na ubaguzi ni kupitia mafunzo ya upendeleo bila kufahamu. Ili kuwasaidia wanachama wetu kuelewa ubaguzi na mapendeleo yanayousababisha, tumeunda zana hii ya kujielimisha tukichunguza upendeleo na vipengele vingine ambavyo huathiri maamuzi ya watu, hata bila ufahamu wao.

Kuchukua hatua pamoja

Airbnb Citizen hutetea maendeleo kwa kufanya kazi pamoja na jamii yetu ya kimataifa. Hapa ndipo sisi hushiriki zana za mafundisho na utetezi, mawazo kutoka kwa wawazaji wakuu, habari kuhusu hali ya kukodisha nyumba na njia za kuchukua hatua.

Kuwasaidia wenyeji wetu kujenga kujihisi nyumbani

Uelewa wa pamoja ni muhimu katika kujenga matukio yanayokaribisha zaidi na ya kujumuisha ya Airbnb. Kituo chetu cha cha msaada kilichopanuliwa kina majibu ya maswali mengi ya ulimwengu halisi kuhusu sera ya kutobagua.

Tungependa kusikia kutoka kwako

Tunatiwa moyo naKituo cha Jumuiya,ambapo wenyeji wetu hushiriki dhana, ambazo hutufurahisha na kutupa motisha ya kujenga tovuti bora zaidi. Shiriki uzoefu wako wa uingiliano wa kibinadamu na uanzishe majadiliano.

Tunaamini katika uungaji mkono wa mabadiliko kupitia ushirikiano wa ndani na nje wa Airbnb
Maendeleo huwa na matokeo makubwa wakati ambapo mashirika yaliyo na maadili ya pamoja hufanya kazi pamoja kuhudumia jumuiya zao. Hapa ni machache ya ushiriakiano wetu wa nje ambo unakuza majadiliano ya wazi, na kuinua sauti tofauti katika kiwango cha kimataifa na mtaa.
Eneo letu la kazi ni sehemu muhimu ya jumuiya ya Airbnb
Airbnb ni kweli uwezeshwa na watu - wenyeji wetu na wageni duniani kote na jumuiya ya ndani ya wafanyakazi na washiriki wa biashara huunda jinsi tunavyofanya kazi na kukua. Tunaamini kuwa uanuwai ni muhimu kwa kujenga ulimwengu ambapo kila mtu anaweza kujisikia nyumbani, na tunachukua hatua ya kukomesha ubaguzi na kujenga kampuni jumuishi zaidi. Tumejitolewa kwa uwazi tunapofanya kazi kuifanya Airbnb eneo la kazi ambapo kila mmoja huhisi kuwa amekaribishwa na sauti zote zinasikika.
Kuajiri na Ujumuishaji kwenye Airbnb