MATUKIO YA AIRBNB

Andaa tukio la mtandaoni

Jiunge na jumuiya ya wenyeji inayounganisha ulimwengu kwa njia mpya kabisa.

Jiunge na jumuiya ya wenyeji inayounganisha ulimwengu kwa njia mpya kabisa.

Matukio ya Airbnb ni shughuli jumuishi zinazobuniwa na wenyeji ambazo ni zaidi ya utalii au mafunzo ya kawaida. Na sasa unaweza kuyaandaa kwa ajili ya yeyote, popote.

Matukio ya Airbnb ni shughuli jumuishi zinazobuniwa na wenyeji ambazo ni zaidi ya utalii au mafunzo ya kawaida. Na sasa unaweza kuyaandaa kwa ajili ya yeyote, popote.

Fanya ukiwa nyumbani

Shiriki utaalamu wako na ulimwengu.

Kutana na wageni wa kimataifa

Fanya ulimwengu uonekane mdogo na wenye urafiki zaidi.

Jenga biashara

Pata pesa huku ukifanya kitu unachopenda kwa kusaidiwa na Airbnb.

Jinsi inavyofanya kazi

Ikiwa tayari wewe ni mwenyeji wa tukio, karibu tena! Ili kuanza kukaribisha wageni mtandaoni, utahitaji kuunda tukio jipya kabisa na uliwasilishe kwa ajili ya kutathminiwa kwa kufuata utaratibu ulio hapa chini.

Buni tukio lako

Matukio yote huanza na viwango vyetu vya ubora—weledi, ufikiaji na muunganisho. Lakini pia fikiria kuhusu jinsi ya kuingiliana na wageni mtandaoni na upunguze kabisa vifaa ambavyo watahitaji kuwa navyo ili kushiriki. Unapokuwa na wazo, anza mchakato wa kuwasilisha.

Shiriki wazo lako

Kisha, utahitaji kuelezea shughuli zako kwenye ombi na pia kwenye ukurasa wa tukio lako la baadaye. Tunapendekeza ushiriki thamani ya kile unachotoa kwa undani, uanzie bei ya chini hadi utakapokuwa na tathmini kadhaa na uweke urefu usiozidi dakika 90.

Wasilisha tukio lako

Unakaribia kumaliza! Unapofika kwenye sehemu ya Mahali, tia alama kwenye kisanduku cha Ndiyo, hili ni tukio la mtandaoni. Kila kitu kitakapokamilika, utakuwa uko tayari kuwasilisha. Timu yetu itasoma na kukujulisha ikiwa imeidhinishwa ndani ya wiki 2-4.

Unda na uanze kukaribisha wageni

Unapoendelea kusubiri, unaweza kuchagua eneo ambalo linakuwakilisha wewe na shughuli zako na uanze kutayarisha mipangilio ya kamera yako, mwangaza na sauti. Unaweza pia kuanza kujifunza tovuti ya mikutano ya mtandaoni ya Zoom. Usiwe na wasiwasi, kabla hujaanza kukaribisha wageni, tutashiriki nawe nyenzo nyingi ili kukufanikisha.

Jinsi wenyeji wanavyoshiriki ulimwengu wao

Wenyeji hawa huleta mvuto wa matukio kwenye skrini pamoja na shughuli za kipekee za makundi madogo za kufanya pamoja wakati tumetengana.

Tafakari pamoja na Kondoo
Uzingativu wa moja kwa moja kutoka kwenye shamba la Uskochi, pamoja na kukutana na marafiki wa mbali.
Furaha ya Kuoka Mikate kama Familia
Muda wa furaha jikoni kwa ajili ya watoto na watu wazima vilevile ambao mwishowe unazalisha keki tamu.
Siri za Kiinimacho
Matukio hayo ni maonyesho kwa sehemu na mafunzo kwa upande mwingine, na wageni wanajifunza saikolojia ya kiini macho na ujanja wanaoweza kufanyia nyumbani.

Tupo nyuma yako

Hutakuwa peke yako—utaweza kupata vifaa vya elimu na fursa za kukusaidia kukua kama mwenyeji na mjasiriamali.

Nyenzo

Miongozo, vidokezi na ujanja wa kufanya matukio ya mtandaoni yenye ufanisi.

Matukio ya mtandaoni

Fahamu jinsi ya kuwa mtaalamu wa kukaribisha wageni, mtandaoni na vinginevyo.

Usaidizi wa jumuiya

Ungana na wenyeji wengine kupitia vikundi na mikutano kwenye Facebook.

Maswali yanayoulizwa mara kwa mara

Je, nitajisajili jinsi gani?

Utatumia fomu ileile ya kuwasilisha kama ilivyo kwa matukio mengine yote. Unapofika kwenye sehemu ya Mahali, tia alama kwenye kisanduku cha **Ndiyo, hili ni tukio la mtandaoni **. Kisha timu yetu itatathmini fomu uliyowasilisha haraka iwezekanavyo na kukujulisha ikiwa imeidhinishwa ndani ya wiki 2-4.

Ni nini tofauti kuhusu kufanya tukio la mtandaoni?

Matukio ya mtandaoni yenye kuvutia zaidi na kujumuisha huhitaji tu muda wa saa 1-2 na vifaa vichache ili kushiriki. Gharama za tukio la mtandaoni pia kwa ujumla zipo chini kuliko gharama za tukio la ana kwa ana, kwa hivyo bei yako inapaswa kuzingatia hilo. Pia inahitaji kamera na muunganisho imara wa intaneti ili uweze kutiririsha sauti na video wakati wa tukio lako.

Nitapeperushaje tukio langu mtandaoni?

Utatumia tovuti inayoitwa Zoom ambayo huwaruhusu wageni wako wote kujiunga na tukio hilo mara moja, huwezesha sauti na video ili watu wote wawe na maingiliano na hutoa nyenzo nyingine za kukusaidia kuandaa tukio. Mara tukio lako la mtandaoni litakapoidhinishwa, utapokea mwaliko wa kujisajili kupata akaunti ya Zoom ya bila malipo. Baada ya kujisajili, jaribu muunganisho wako wa intaneti kwa kujiunga na mkutano wa majaribio ili uweze kuelewa namna ya kuitumia.

Je, Matukio ya Mtandaoni ni nini?

Matukio ya Mtandaoni, sawa na yale halisi, huwaunganisha wageni na wenyeji weledi, huandaa njia ya kukutana na kuingiliana na wageni na hutoa muundo rahisi wa kumuunganisha kwa mbali kila mtu ambaye amewekwa karantini na aliye nyumbani. Watu wanaweza kujiunga na matukio ya mtandaoni wakiwa nyumbani au mahali popote ulimwenguni—wanachohitaji tu ni muunganisho wa intaneti. Si lazima wawe kwenye eneo fulani mahususi au wawe na vifaa vingi ili kushiriki.

Pata maelezo zaidi kuhusu kukaribisha wageni kwenye Matukio ya Airbnb