SIMULIZI ZA WENYEJI

Jinsi Dennis anavyokaribisha wageni

Dennis hukaribisha wageni jijini Londoni kwa sababu ana uhuru wa kubadilisha mambo

Dennis hukaribisha wageni jijini Londoni kwa sababu ana uhuru wa kubadilisha mambo

Ni nini kilichokupa motisha yako ya kuanza kukaribisha wageni?

Nilikuwa na mpangaji kichaa. Jamaa mzuri lakini kuishi naye balaa, kwa hivyo alipohama, rafiki yangu wa karibu alinipendekezea Airbnb na nikaamua kujitosa ndani.

Ulikuwa na wasiwasi upi kabla ya kuanza kukaribisha wageni?

Sitawahi kusahau nilipofikiria "Ninafanya nini? Ninaweza kuwa namwalika muuaji wa shoka akae nyumbani kwangu" usiku kabla ya mgeni wangu wa kwanza kuwasili. Alikuwa jamaa mzuri kweli kutoka Boston ambaye aliwasili akitembea kwa magongo. Alikuwa ukumbusho mzuri kwangu kwamba nastahili kufuata ndoto zangu kila wakati.

Je, unajiandaa vipi kuhakikisha kuwa wageni wanafurahia wanapowasili?

Kuweka habari nyingi kuhusu ujirani wangu kadiri niwezavyo, kuhakikisha kila kitu kiko safi na nadhifu na kuwa makini kuhusu mambo madogo, kama vile kuhakikisha nina karatasi ya kutosha ya chooni; nimestaajabishwa na idadi ya wageni wanaopatwa na hofu kuhusiana na jambo hili.

Je, kuwa mwenyeji kumebadilisha mtindo wako wa maisha?

Si sana kwa sababu niratibu shughuli zangu za Airbnb ziingianae na maisha kadri iwezekanavyo na wakati ninahitaji mapumziko, ninaweza kuzuia "wakati wangu binafsi" kwenye kalenda yangu ya Airbnb.

Ni nini unachopenda zaidi kuhusu kuwa mwenyeji?

Kupelekwa na wageni kupata chakula cha jioni.

Je, Garantii ya Mwenyeji ni jambo muhimu kwako?

Naam, bila shaka. Lilikuwa mojawapo ya mambo ambayo yalinisaidia kufanya uamuzi wa kujiunga na Airbnb, kwa sababu ikiwa kutatokea uharibifu au matatzio, ninao kama mpango wa dharura. Nina bango la mwimbaji maarufu ninalolipenda sana, na nadhani nimekuwa nalo kwa zaidi ya miaka 37; hilo likaharibiwa, ninaweza kukasirika sana. Kwa hivyo kujua kwamba kitu kama hicho kinalindwa na Garantii ya Mwenyeji ni jambo la faraja kweli.

Je, ni nini unachojivunia zaidi kwa wakati ambao umekuwa mwenyeji?

Jinsi tangazo langu linavyoweza kuchaguliwa lionekane katika tangazo la Airbnb. Safi!

Simulizi zingine za wenyeji

Anza kutayarisha tangazo lako

Anza kutayarisha tangazo lako