ULINZI WA MWENYEJI

Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji

Katika hali ambayo ni nadra kutokea, ikiwa mtu ataumia au mali yake imeharibika wakati wa ukaaji ambao unakingwa, unaweza kupata ulinzi wa hadi Dola za Marekani 1,000,000 wa bima ya dhima ya msingi.

*Haitumiki kwa wenyeji wanaotoa malazi kupitia Airbnb Travel, LLC, wenyeji huko China bara, wenyeji huko Japan, au wenyeji wa matukio.

Ni nini kimejumuishwa?

Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji inaweza kushughulikia:

  • Jukumu lako la kisheria kwa jeraha la mwili kwa wageni au watu wengineo
  • Jukumu lako la kisheria kwa uharibifu wa mali ya wageni au watu wengineo
  • Jukumu lako la kisheria kwa uharibifu kwenye maeneo ya pamoja, kama vile kumbi za jengo na mali za jirani, uliosababishwa na mgeni au watu wengineo

Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji haishughulikii:

  • Uharibifu au jeraha linalotokana na kitu kilichofanywa kwa makusudi (si ajali)
  • Kupoteza mapato
  • Uharibifu kwenye sehemu yako au kwa mali yako (hayo yanaweza kulindwa na Garantii ya Mwenyeji wa Airbnb*)

*Garantii ya Mwenyeji wa Airbnb haihusiani na Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji au Airbnb UK Services Limited.

Tumejitolea kuendeleza jumuiya salama na inayoaminika duniani kote.

Kwa kuwa ulikuwa mgeni hapo awali, wasiwasi mwingi ulikuwa tayari umeshapunguzwa. Nilijua sehemu yangu itakuwa imekatiwa bima ... na nilijua wageni watakuwa wenye heshima."

Uslan, mwenyeji jijini London

Kwa kuwa ulikuwa mgeni hapo awali, wasiwasi mwingi ulikuwa tayari umeshapunguzwa. Nilijua sehemu yangu itakuwa imekatiwa bima ... na nilijua wageni watakuwa wenye heshima."

Uslan, mwenyeji jijini London

Utaratibu wa kudai

1. Fomu ya kiingizio imejazwa

Wakati mwenyeji, mgeni au mtu mwingine anapowasiliana na Usaidizi wa Jumuiya, Airbnb itatoa taarifa kuhusu utaratibu wa kuandikisha dai.

2. Kampuni ya bima inamteua mkadiriaji wa madai, ambaye kisha anatathmini dai hilo

Baada ya fomu ya kiingizio kujazwa, mkadiriaji wa madai kwa niaba ya kampuni ya bima atawasiliana nawe ili kujadili dai hilo na kukusanya taarifa.

3. Dai linachunguzwa

Mkadiriaji wa madai ya mtu mwingine anashughulikia dai hilo kulingana na masharti ya sera ya Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji na sheria na kanuni husika katika himaya inayotumika.

Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji inadhibitiwa na sheria, masharti na vighairi fulani.
 Ili kupata maelezo zaidi, pakua muhtasari kamili wa mpango.

Majibu kwa maswali yako

Je, ninahitaji kufanya chochote ili nikingwe chini ya Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji?

Hapana. Kwa kukubali kutangaza nyumba kwenye Airbnb, au kwa kuendelea kutangaza nyumba kwenye Airbnb, wenyeji* wanakubali kukingwa chini ya Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji kwa ajili ya matatizo yanayotokea wakati wa ukaaji kwenye Airbnb. Kumbuka kwamba Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji inadhibitiwa na sheria, masharti na vighairi vya sera.

Wenyeji wanaotaka kujiondoa kwenye mpango wa Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji lazima wafanye mambo yafuatayo:

  • Tutumie barua pepe kutoka kwenye barua pepe inayohusishwa na akaunti yako ya mwenyeji
  • Jumuisha jina lako kamili na nambari ya simu inayohusishwa na akaunti yako ya mwenyeji
  • Jumuisha kichwa halisi cha tangazo lako

Tafadhali kumbuka anwani ya barua pepe ya kujiondoa haitafuatiliwa isipokuwa kwa madhumuni ya kuchakata maombi ya kujiondoa.

*Haitumiki kwa wenyeji wanaotoa malazi kupitia Airbnb Travel, LLC, wenyeji huko China bara, wenyeji huko Japan na wenyeji wa matukio.

Je, uko tayari kuanza kukaribisha wageni?

Inapatikana kwa wenyeji duniani kote*
Huwalinda wenyeji tangu kuingia hadi kuondoka