ULINZI WA MWENYEJI

Karibisha wageni kwa ujasiri

Wenyeji wa nyumba wanapata ulinzi wa hadi Dola za Marekani 1,000,000 kwa uharibifu wa mali na hadi Dola za Marekani 1,000,000 kwa bima ya dhima.

Wenyeji wa nyumba wanapata ulinzi wa hadi Dola za Marekani 1,000,000 kwa uharibifu wa mali na hadi Dola za Marekani 1,000,000 kwa bima ya dhima.

Ulinzi kwa ajili ya kila mwenyeji. Kila tangazo. Kila mahali.

Ulinzi kwa ajili ya kila mwenyeji. Kila tangazo. Kila mahali.

Inapatikana kwa wenyeji duniani kote*
Huwalinda wenyeji tangu kuingia hadi kuondoka
Hailinganishwi katika tasnia ya safari

*Doesn’t apply to hosts who offer accommodations through Airbnb Travel, LLC, hosts in mainland China, hosts in Japan, or hosts of experiences.

Jinsi wenyeji wa Airbnb wanavyolindwa

Garantii ya Mwenyeji wa Airbnb

Ikiwa mgeni ataharibu sehemu au mali yako wakati wa ukaaji wake na akashindwa au hayupo tayari kukurudishia gharama, unaweza kulindwa na hadi Dola 1,000,000 za Marekani kama ulinzi wa uharibifu wa mali

Garantii ya Mwenyeji wa Airbnb huweza kulinda:

  • Uharibifu katika sehemu yako uliosababishwa na wageni
  • Uharibifu wa mali yako uliosababishwa na wageni
  • Uharibifu uliosababishwa na mnyama wa usaidizi wa mgeni

Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji

Katika hali ambayo ni nadra kutokea ikiwa mtu ataumia au mali yake kuharibika wakati wa ukaaji katika sehemu yako, unaweza kupewa hadi Dola 1,000,000 za Marekani kama bima ya dhima ya msingi.

Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji inaweza kushughulikia:

  • Jukumu lako la kisheria kwa jeraha la kimwili kwa wageni au watu wengineo
  • Jukumu lako la kisheria kwa uharibifu wa mali ya wageni au watu wengineo
  • Jukumu lako la kisheria la uharibifu kwa maeneo ya pamoja, kama vile kumbi za jengo na mali za jirani, uliosababishwa na mgeni au watu wengineo

Tuko tayari kukusaidia

Uthibitisho wa utambulisho

Unaweza kuhitaji kwamba wageni wako wapitie mchakato wa kuthibitisha utambulisho wao kabla hatujathibitisha nafasi waliyoweka. Wageni huenda wakahitajika kutoa taarifa ya binafsi ili Airbnb iithibitishe, kama vile kitambulisho rasmi cha serikali.

Mawasiliano salama

Kisa fulani kikitokea, tovuti yetu ya kutuma ujumbe inakuruhusu uwasiliane na wageni na kusuluhisha matatizo. Ikiwa suluhisho haliwezi kufikiwa, Airbnb itakuongoza katika hatua zinazofuata.

Usaidizi wa saa 24

Ikiwa wewe, mali zako au wageni wako mtakumbwa na jambo fulani, timu yetu ya kimataifa ya Usaidizi wa Jumuiya iko tayari kutoa msaada.

Kuwa na Garantii ya Mwenyeji hutupa utulivu, kwa sababu ajali zinaweza kutokea. Kuwa na mpango wa ulinzi hukupa utulivu zaidi."
Kuwa na Garantii ya Mwenyeji hutupa utulivu, kwa sababu ajali zinaweza kutokea. Kuwa na mpango wa ulinzi hukupa utulivu zaidi."

Silvia na Mateo, wenyeji jijini London

Silvia na Mateo, wenyeji jijini London

Kuwa na Garantii ya Mwenyeji hutupa utulivu, kwa sababu ajali zinaweza kutokea. Kuwa na mpango wa ulinzi hukupa utulivu zaidi."
Kuwa na Garantii ya Mwenyeji hutupa utulivu, kwa sababu ajali zinaweza kutokea. Kuwa na mpango wa ulinzi hukupa utulivu zaidi."

Silvia na Mateo, wenyeji jijini London

Silvia na Mateo, wenyeji jijini London

Majibu kwa maswali yako

Garantii ya Mwenyeji wa Airbnb ni nini?

Garantii ya Mwenyeji wa Airbnb hutoa ulinzi wa hadi Dola za Marekani 1,000,000 kwa mwenyeji kwa uharibifu wa mali iliyowekewa bima katika hali ambayo ni ya nadra mgeni amefanya uharibifu unaozidi amana ya ulinzi au ikiwa amana ya ulinzi haijawekwa.

Mpango wa Garantii ya Mwenyeji haushughulikii pesa taslimu au hisa, vitu vya kukusanywa, sanaa adimu, vito, wanyama vipenzi au dhima ya mtu binafsi. Tunapendekeza wenyeji waweke vitu vyao vya thamani mahali salama au waviondoe wanapopangisha nyumba yao. Mpango huu pia haushughulikii kupotea au uharibifu wa mali kwa sababu ya uchakavu. Pata maelezo zaidi

Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji ni nini?

Mpango wa Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji hutoa kinga ya dhima ya msingi ya hadi dola 1,000,000 kwa kila kisa iwapo kutakuwepo na mtu mwingine atakayedai kujeruhiwa mwili au kuharibiwa mali kunakohusiana na ukaaji wa Airbnb.

Kinga hii inadhibitiwa na kikomo cha dola 1,000,000 kwa kila eneo la tangazo na hali fulani, vikomo na mazuio yanaweza kutumika. Pata maelezo zaidi

Kuna tofauti gani kati ya Garantii ya Mwenyeji wa Airbnb na Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji?

Mpango wa Garantii ya Mwenyeji na Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji ni mipango miwili tofauti ambayo Airbnb inatoa ili kuwalinda wenyeji iwapo uharibifu au majeraha yatatokea.

Garantii ya Mwenyeji: Garantii ya Mwenyeji wa Airbnb imebuniwa ili kulinda wenyeji katika kisa nadra cha uharibifu wa mali zao, chumba au nyumba unaosababishwa na mgeni anayekaa kwenye sehemu hiyo. Garantii ya Mwenyeji si bima na haichukui mahali pa bima yako ya mmiliki wa nyumba au mpangaji wa nyumba.

Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji: Mpango wa Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji ni bima na umebuniwa ili kuwalinda wenyeji katika hali ambapo mtu mwingine anatoa madai ya kujeruhiwa mwili au uharibifu wa mali. Mpango wa Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji unapatikana kwa wenyeji bila kujali mipango mingine ya bima, lakini itafanya kazi tu kama kinga ya bima ya msingi kwa visa vinavyohusiana na ukaaji wa Airbnb. Pata maelezo zaidi

Ninaombaje kurudishiwa gharama chini ya Garantii ya Mwenyeji?

Wenyeji na wageni mara nyingi hutatua matatizo wenyewe kupitia Kituo chetu cha Usuluhishi. Ikiwa hujafanya hivyo bado, wasiliana na mgeni wako kwanza ili umwarifu kuhusu malalamiko yako na uwasilishe ombi la malipo katika Kituo chetu cha Usuluhishi.

Ikiwa huwezi kutatua tatizo na mgeni: Kwanza, tafadhali jifahamishe sheria na masharti ya Garantii ya Mwenyeji. Kumbuka kwamba maombi lazima yawasilishwe katika siku 14 tangu kuondoka kwa mgeni, au kabla ya mgeni mwingine kuingia, lolote litakalotokea kwanza. Pata maelezo zaidi

Bima ya mmiliki wa nyumba hufanyaje kazi kwenye Airbnb?

Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji ya Airbnb itafanya kazi kama bima ya msingi na hutoa kinga ya dhima kwa wenyeji na pale inapofaa, wamiliki wao wa nyumba, chini ya masharti fulani, vikomo na vighairi.

Ikiwa una maswali kuhusu jinsi sera hii inavyoingiliana na bima yoyote ya mmiliki wa nyumba au ya mpangaji, unapaswa kujadili kinga yako ya bima na mtoa huduma wako wa bima. Baadhi ya sera zinawalinda wamiliki wa nyumba na wapangaji kutokana na mashtaka fulani yanayotokana na kujeruhiwa kwa mgeni, lakini nyingine hazifanyi hivyo. Daima ni wazo zuri kuijulisha kampuni yako ya bima kuhusu shughuli ya upangaji kwenye sehemu yako hata ingawa dhima inayotokea wakati wa ukaaji wa Airbnb inapaswa kushughulikiwa na sera ya Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji. Pata maelezo zaidi

Bima ya Ulinzi ya Tukio ni nini?

Bima ya Ulinzi ya Tukio ni dhima ya bima ya msingi kwa ajili ya wenyeji wa tukio kwa mtu mwingine ikiwa mgeni au mtu mwingine atajeruhiwa au mali itaharibiwa wakati wa kufanya tukio. Bima hiyo hufikia hadi Dola milioni 1 za Marekani kwa kila tukio, na ustahili huo wa malipo hutegemea aina ya tukio. Wageni wako chini ya kikomo cha jumla ya Dola milioni 1 za Marekani wakati wa muda wa sera, na masharti fulani, vikomo na mazuio huweza kutumika. Pata maelezo zaidi

Je, uko tayari kuanza kukaribisha wageni?

Je, uko tayari kuanza kukaribisha wageni?