Ujumbe kwa wenyeji wetu kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Brian Chesky

Habari Mwenyeji,

Miezi hii kadhaa imekuwa ya madhara makubwa kwetu sote. Kama wengi wenu, mimi huamka kila siku nikiwa mbali na marafiki na wafanyakazi wenza, nikishangaa ni nini ninapaswa kutazamia. Ninapotazama taarifa ya habari kila siku, ninasikitikia nchi, jamii, na familia zote ambazo zimezidiwa na kiwango na athari za tatizo hili.

Wakati huu wote, tasnia ya usafiri ulimwenguni imekoma. Ndege zimezuiliwa kuruka na mipaka imefungwa. Wengi wetu—pamoja na wageni wetu—tumewekwa kwenye karantini kwa maagizo ya serikali, na hatuwezi kutoka kwenye nyumba zetu. Kusafiri kama tunavyojua kumekuwa vigumu.

Mnamo tarehe 11 Machi, wakati Shirika la Afya Duniani lilitangaza janga la kimataifa, tulikabiliwa na tatizo. Ikiwa tungeruhusu wageni kughairi na kurejeshewa fedha, tulijua ingeweza kuwa na athari kubwa kwa riziki yako. Lakini hatukutaka kuwashinikiza wageni na wenyeji wajiweke katika hali isiyo salama na kuunda hatari nyingine ya afya ya umma. Tuliamua kwamba tumelazimika kuwaruhusu wageni wako kughairi na kurejeshewa fedha kamili—pamoja na ada zetu zote. Tafadhali fahamu kuwa uamuzi huu haukuwa uamuzi wa kibiashara, lakini ni kwa kuzingatia afya ya umma.

Hata hivyo, ingawa ninaamini tulifanya jambo sahihi katika kuweka kipaumbele afya na usalama, samahani kwamba tuliwasiliana na wageni kuhusu uamuzi huu bila kushauriana nawe—kama washirika wanavyopaswa kufanya. Tumesikia kutoka kwako na tunajua tungeweza kuwa washirika bora zaidi.

Ingawa huenda haikuonekana hivyo, sisi ni washirika. Wakati biashara yako inaathirika, biashara yetu inaathirika. Tunajua kuwa hivi sasa wengi wenu mnaumia, na kile mnachohitaji ni hatua kutoka kwetu ili kuwasaidia, sio maneno tu.

Hizi hapa ni hatua kadhaa tunazochukua ili kukusaidia kustahimili tatizo hili.

Tutalipa dola milioni 250 USD kwa wenyeji ili kusaidia kugharamia ughairi kwa sababu ya COVID-19. Mgeni akighairi nafasi aliyoweka kwa sababu ya hali inayohusiana na COVID-19, iliyo na tarehe ya kuingia kati ya tarehe 14 Machi na tarehe 31 Mei, tutakulipa asilimia 25 ya yale ambayo kwa kawaida ungepokea kupitia sera yako ya kughairi. Hii inatumika kuanzia wakati huo kwa ughairi wote unaohusiana na COVID-19 katika kipindi hiki. Gharama hii itashughulikiwa kikamilifu na Airbnb. Malipo haya yataanza kutolewa Aprili. Wageni walioweka nafasi mnamo au kabla ya tarehe 14 Machi bado wataweza kughairi na kurejeshewa fedha ya kawaida au salio la safari sawa na asilimia 100 ya waliyolipa. Unaweza kwenda kwenye airbnb.com/250Msupport kwa maelezo zaidi.

Tunaunda Mfuko wa Msaada kwa Mwenyeji Bingwa wa dola milioni 10 USD. Hii imeundwa kwa Wenyeji Bingwa ambao hupangisha nyumba yao wenyewe na wanahitaji msaada kulipa kodi au rehani, pamoja na wenyeji wa muda mrefu wa Matukio wanaojaribu kupata riziki. Wafanyakazi wetu walianzisha mfuko huu na dola milioni 1 USD kwa michango kutoka mifuko yao wenyewe, na Joe, Nate na mimi tunachangia dola milioni 9 USD zilizobaki. Kuanzia Aprili, wenyeji wanaweza kuomba ruzuku za hadi dola 5,000 USD ambazo hazihitaji kulipwa. Unaweza kwenda kwenye airbnb.com/superhostrelief kwa maelezo zaidi.

Tunafanya iwe rahisi kwa wageni wako wa zamani kutuma msaada wa kifedha kwako moja kwa moja. Tumesikia kutoka kwa wageni wengi ambao wanashukuru sana kwa unyumbufu wa wenyeji wa Airbnb na wangependa kukusaidia kifedha. Tunaunda njia ya wageni kutuma ujumbe pamoja na mchango kwa mwenyeji yeyote ambaye wameishi naye hapo awali. Tunatarajia hii iwekwe mtandaoni Aprili. Tunajua kuwa hata mchango mdogo una manufaa makubwa kwa wakati huu mgumu.

Tumefanya kazi pamoja ili kupata usaidizi kwa wenyeji katika Mswada wa Kichocheo wa COVID-19 wa hivi karibuni wa Serikali ya Marekani. Sheria hii sasa inaruhusu wenyeji wa Marekani kunufaika na hatua nyingi za misaada, ikiwemo ruzuku za biashara ndogo ndogo, mikopo ya biashara ndogo ndogo, na usaidizi wa ukosefu wa ajira. Asanteni sana kwa simu zaidi ya 105,000 mlizopiga na barua pepe mlizotuma kwa Wabunge.

Tunashughulikia mipango mingine pia na tutatoa maelezo zaidi katika wiki zijazo. Hii ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii na wataalamu na matabibu wa kudhibiti magonjwa kuhusu viwango vya usafi ili kukuweka wewe pamoja na wageni wako salama, bima ya kusafiri kwako na wageni wako, na mipango ya kutoa mahitaji ya kusaidia kujenga tena biashara yako.

Ahadi yangu kwako ni kujenga upya ushirikiano wetu. Tunapofanya kazi pamoja, tunafanikiwa zaidi. Nimeona mfano wa jambo hili ukitokea hivi karibuni katika juhudi zetu za pamoja za kuwapa makazi wahudumu wa dharura wa kimatibabu walio kwenye mstari wa mbele. Pamoja tunasaidiana kuwapa makazi watoa huduma ya afya, wahudumu wa misaada, na wahudumu wa dharura zaidi ya 100,000 kwa kuwapa makazi ya bure au yenye ruzuku. Zaidi ya 40,000 kati yenu tayari mmeinua mikono yenu ili kusaidia. Tembelea airbnb.com/covid19relief ili kujiunga nao.

Uaminifu ni msingi wa ushirikiano, na huchukua muda mrefu kuunda. Tunajua kuwa tuna jukumu la kutekeleza katika kuimarisha biashara yako, lakini ni kipaumbele chetu na tumejitolea. Wakati usafiri utarudi—na ni hakika—tunatarajia kuwakaribisha tena mamilioni ya wageni pamoja.

Brian Chesky

% {}

<spacing large>% {}

Ujumbe huu unapatikana katika lugha zifuatazo.

Italiano | [Français] (/d/host-message?locale=fr) | Deutsch | Português | Español | Русский | 中文 | 日本語 | 한국어