ULINZI WA MWENYEJI

Bima ya Ulinzi ya Tukio

Katika tukio la nadra ambapo mtu anajeruhiwa au mali yake inaharibiwa wakati wa tukio linalokingwa, wenyeji wanaweza kulindwa na bima ya dhima ya hadi dola 1,000,000 USD.

Inapatikana kwa wenyeji wa matukio mengi
Inalinda wenyeji tangu mwanzo hadi mwisho wa tukio
Hailinganishwi katika tasnia ya safari

Mpango huu unatumika kwa wenyeji wa matukio, isipokuwa huko China bara na Japani. Hautumiki kwa wenyeji wa malazi.

Ni nini kimejumuishwa?

Bima ya Ulinzi ya Tukio inaweza kushughulikia:

-Jukumu lako la kisheria kwa majeraha ya mwili kwa wageni au watu wengineo -Jukumu lako la kisheria kwa uharibifu wa mali ya wageni au watu wengineo

Bima ya Ulinzi ya Tukio haishughulikii:

  • Majeraha ya mwili au uharibifu wa mali unaotokana na kitu kilichofanywa kwa makusudi (si ajali)
  • Uharibifu, upotezaji, au wizi kwenye mali binafsi ya mwenyeji
  • Matukio yanayohusisha ndege au aina fulani za shughuli ngumu (kama vile kuruka kutoka juu kwa kamba na utelezaji wa kupandishwa kwa helikopta)

Karibisha wageni kwa ujasiri

Muda wa kutayarisha tukio

Bima ya Ulinzi ya Tukio inaweza kuwakinga wenyeji wakati wa tukio na pia wanapotayarisha eneo kwa ajili ya tukio, kabla halijaanza au baada ya kumalizika, chini ya sheria, masharti na vighairi vya sera.

Bima kwa ajili ya wenyeji wenza

Wenyeji wenza ambao hutoa huduma husiani zinazohusiana na tukio wanaweza pia kukingwa chini ya Bima ya Ulinzi ya Tukio, chini ya sheria, masharti na vighairi vya sera.

Tumejitolea kuendeleza jumuiya salama na inayoaminika duniani kote.

Utaratibu wa kudai

1. Fomu ya kuandikishwa imejazwa

Mwenyeji, mgeni, au mhusika mwingine atakamilisha na kuwasilisha Fomu ya Kujiandikisha Kwenye Mpango wa Bima.

2. Kampuni ya bima inamteua mkadiriaji wa madai, ambaye atatathmini dai hilo

Baada ya fomu ya kuandikishwa kujazwa, mkadiriaji wa madai kwa niaba ya kampuni ya bima atawasiliana nawe ili kujadili dai hilo na kukusanya taarifa.

3. Dai hilo linachunguzwa na mkadiriaji wa madai aliyewekwa

Mkadiriaji wa madai ya mhusika mwingine anashughulikia dai hilo kulingana na masharti ya sera ya Bima ya Ulinzi ya Mwenyeji na sheria na kanuni husika katika himaya inayotumika.

Bima ya Ulinzi ya Tukio inadhibitiwa na sheria fulani, masharti na vighairi. 
 Ili kupata maelezo zaidi, pakua muhtasari kamili wa mpango.

Majibu kwa maswali yako

Je, ninahitaji kufanya chochote ili nikingwe chini ya Bima ya Ulinzi ya Tukio?

Hapana. Unapokuwa mwenyeji wa tukio na kukubali Masharti ya Huduma ya Airbnb, unakubali pia kukingwa chini ya Bima ya Ulinzi ya Tukio kwa mambo yanayotokea wakati wa matukio ya Airbnb. Kumbuka kuwa Bima ya Ulinzi ya Tukio inadhibitiwa na sheria, masharti na vighairi vya sera.

Ikiwa ungependa kujiondoa kwenye mpango wa bima ya Ulinzi ya Tukio, lazima ufanye yafuatayo:

  • [Tutumie barua pepe] (mailto:epi-opt-out@airbnb.com) kutoka kwenye anwani ya barua pepe inayohusishwa na akaunti yako ya mwenyeji wa tukio
  • Jumuisha jina lako kamili na nambari ya simu inayohusishwa na akaunti yako ya mwenyeji wa tukio
  • Jumuisha kichwa halisi cha tukio lako lililofanyika

Tafadhali kumbuka anwani ya barua pepe ya kujiondoa haitafuatiliwa isipokuwa kushughulikia maombi ya kujiondoa.

Je, Bima ya Ulinzi ya Tukio inatumika kwenye matukio ya mtandaoni?

Wenyeji wa matukio ya mtandaoni wanaweza kukingwa na Bima ya Ulinzi ya Tukio katika hali nadra ambapo mgeni anajeruhiwa au mali yake kuharibiwa wakati wa mojawapo ya vipindi hivi vya maingiliano ya video na mwenyeji anawajibika kisheria. Bima ya Ulinzi ya Tukio haikingi hatari husika za wenyeji za mtandaoni kama vile kukashifu, au wizi wa data ya kielektroniki au ukiukaji wa hakimiliki.

Ili kupata maelezo zaidi kuhusu kuandaa matukio, tembelea [Kituo cha Msaada] (/msaada/mwanzo).

Uko tayari kuanza kuunda tukio lako?