AIRBNB NA UHIFADHI WA BAHARI WANAKULETEA

Antarctic Sabbatical

Safari ya utafiti kwenda sehemu
ya mbali zaidi ya Dunia

Five passionate individuals have been selected from tens of thousands of applicants to travel to Earth’s most remote continent on a first-of-its-kind scientific research mission spearheaded by Airbnb and Ocean Conservancy and led by Kirstie Jones-Williams. Hailing from Hawaii, Arizona, Norway, India and Dubai, the volunteers have been chosen from more than 140,000 applications from over 200 countries around the world.

Utaratibu wa safari ya kiuchunguzi

Wiki 1-2

Treni nchini Chile: Utaanza kwa kukutana na wenzako na kiongozi wa msafara, Kirstie Jones-Williams. Baada ya kujitambulisha, utakuwa na mafunzo ya wiki mbili, ya mwili na ya akili, ili uwe tayari kufanya utafiti katika mazingira hatari ya Antaktika. Hapa utazoea lugha ya kisayansi, uangalie magwanda yako, uungane na washirika wa ndani, na uchunguze maeneo ya nje ya Chile.

Wiki 3

Utafiti Antaktika: Mara utakapowasili kwenye Union Glacier Camp, utatumia siku kumi zilizojaa kazi na uchunguzi wa saa nyingi. Utapata nafasi ya kutembelea Ncha ya Kusini na kugundua uzuri wa maeneo ya Antaktika kama Drake Icefall, Charles Peak Windscoop, na Elephant's Head. Halafu, katikati ya safari za kuendesha magari ya kwenye theluji na baiskeli nzito, utatumia muda wako mwingi ukiwa bega kwa bega na timu yako, mkikusanya sampuli za theluji zitakazochunguzwa kwenye maabara, na kuendeleza utafiti wenu ili kuona ikiwa maikroplastiki zipo katika sehemu ya ndani ya Antaktika.

Wiki 4

Tayarisha matokeo yako: Baada ya muda wako katika eneo husika, wewe na timu yako mtarudi Chile kutumia siku chache kuchakata mambo mliyojifunza, ili kuonyesha jinsi wanadamu wameathiri eneo la mbali zaidi Duniani. Mtafanya kazi na Ocean Conservancy ili kuwa mabalozi wa kulinda bahari, mkishiriki na ulimwengu jinsi wengine wanavyoweza kusaidia kupunguza plastiki na kutenda kama wahudumu wa sayari yetu.

Nenda na kusudi

Kama Mwanasayansi Raia, utakuwa na nafasi ya kuchangia utafiti wa kisayansi juu ya jinsi wanadamu wanavyoathiri mazingira. Kwa muda wa mwezi, mtafanya kazi kama timu, kukusanya na kuchambua sampuli za msingi za theluji ili kutambua ikiwa maikroplastiki zimeingia sehemu za ndani za bara. Matokeo haya yanaweza kusaidia kubadilisha sera ya umma inayohusu jinsi tunavyotumia plastiki na jinsi ya kuiondoa ipasavyo. Ikiwa itafanikiwa, safari hii inaweza kusababisha utafiti zaidi kuhusu jinsi ya kulinda vyema mfumo huu wa pekee wa ikolojia na sayari yetu kwa ujumla.

Kutana na kiongozi wako wa msafara

Kirstie Jones-Williams ni mwanasayansi wa mazingira anayependa sana kuelewa na kuilinda Dunia dhidi ya athari za wanadamu. Ana Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Mazingira, Shahada ya Pili ya Sayansi ya Bahari na Sera, na kwa sasa anafuatilia Udaktari wa Falsafa kwa kuchunguza athari za maikroplastiki kwenye zuplanktoni za baharini kwenye ncha ya dunia kule Antaktika, Chuo Kikuu cha Exeter, naye anafadhiliwa na ushirika wa mafunzo ya udaktari wa GW4+. Kama kiongozi wa msafara huu, Kirstie atatusaidia kuelewa njia za maikroplastiki kwenda maeneo ya mbali kama vile Antaktika na kuangazia jukumu letu la kulinda ulimwengu wetu wa asili.

"Natafuta watu wenye motisha wanaotamani kushiriki katika kazi hii na warudi nyumbani wakiwa na hamu ya kushiriki matokeo yetu na ulimwengu." -Kirstie Jones-Williams

Kwa kushirikiana na Uhifadhi wa Bahari

Ocean Conservancy inafanya kazi kulinda bahari dhidi ya changamoto kuu zinazoukumba ulimwengu. Njia moja ya kupata mafanikio ni kuungana na wale walio na maoni ya kuwajibika kama hayo. Airbnb imejitolea kutoa fursa ya usafiri endelevu kwa jumuiya yake katika kila hatua ya safari na hii ndiyo sababu Ocean Conservancy inafurahi sana kushirikiana kwenye Antarctic Sabbatical. Airbnb pamoja na Ocean Conservancy watatumia matokeo ya utafiti unaotokana na safari hii kutoa ufahamu kwa juhudi za kielimu na za utetezi, kuangazia suala la uchafuzi wa plastiki, jinsi unavyotuathiri sisi sote na hatua tunazoweza kuchukua.

Safari za Kimafunzo za Airbnb

Programu hiyo ya likizo ya kuongeza masomo inatoa fursa za ufahamu kwa watu ulimwenguni kote kusafiri wakiwa na kusudi na kutenda mema. Uwe macho kutambua fursa za likizo hizo za masomo wakati ujao.

Safari ya kimafunzo ya Kiitaliano

Mnamo Juni 2019, mpango wa miezi mitatu iliyojumuisha watu wa kujitolea kutoka ulimwenguni kote ulianzishwa ili kuhuisha kijiji kidogo cha Italia kilichokuwa katika hatari ya kutoweka.

Various images and footage courtesy of Antarctic Logistics & Expeditions and Studiocanoe.