Ruka kwenda kwenye maudhui

Tafuta eneo la kukaa kwa ajili ya wahudumu wanaopambana na COVID-19

Sehemu za kukaa za mstari wa mbele ni kwa ajili ya watu wanaofanya kazi ya misaada ya COVID-19.
Sehemu ya kukaa ya mstari wa mbele ni nini?
Wenyeji wanasamehe au kupunguza bei zao ili kuunga mkono kazi ya wahudumu wa dharura wanaopambana na COVID-19 katika jumuiya yao. Ikiwa unastahiki, utapata sehemu za kukaa za bila malipo na zenye punguzo.
Sehemu hizi za kukaa ni kwa ajili ya:
  • Wahudumu wa dharura
  • Wataalamu wa matibabu
  • Wahudumu wa afya wa jamii
Tutathibitisha kama sehemu yako inastahiki kwa ajili ya mpango huo.
Unaweza kuweka nafasi ya kukaa ya mstari wa mbele ikiwa:
  • Unahitaji kuwa karibu na kazi, katika eneo lako au katika eneo jipya kwa ajili ya mgawo wa kazi
  • Ungependa kujitenga ili kulinda afya ya familia au watu unaoishi nao chumbani na kwa sasa huna COVID-19
Fahamu ikiwa unastahiki
Utahitaji kujibu maswali kadhaa na uthibitishe ya jukumu la kazi. Mara tutakapowasiliana na mwajiri wako na kuthibitisha taarifa yako, tutakualika uweke nafasi ya sehemu ya kukaa.