Watu wanaweza kubadilika zaidi kuliko hapo awali kuhusu mahali na wakati wanaposafiri. Ili kuwasaidia wanufaike na fursa hizi mpya, tunawaletea mabadiliko yetu makubwa zaidi katika muongo mmoja, ikiwemo njia mpya kabisa ya kutafuta, njia bora ya kukaa muda mrefu na kiwango cha ulinzi kisicho na kifani.
Tunakuletea muundo mpya kabisa, unaotegemea Aina za Airbnb, ili kuwasaidia wageni wetu wachunguze ulimwengu wa Airbnb kwa urahisi na kugundua maeneo ambayo wasingeyajua ili watafute.
Wenyeji wetu hutoa mamilioni ya nyumba za kipekee duniani kote. Aina za Airbnb huzipanga kwenye mkusanyo kukiwa na zaidi ya aina 50 za nyumba zilizochaguliwa kwa ajili ya mtindo wake, eneo au shughuli za karibu. Zinajumuisha:
Wageni sasa wanaweza kugundua kwa urahisi nyumba zaidi ya 20,000 zilizochaguliwa kwa sababu ya usanifu na sehemu zake za ndani ambazo ni maarufu, ikiwemo kazi bora za wasanifu majengo kama vile Frank Lloyd Wright na Le Corbusier.
Wenyeji wa Airbnb hutoa mkusanyiko mkubwa zaidi wa nyumba za kipekee ulimwenguni, kuanzia nyumba za kwenye miti hadi vijumba, katika zaidi ya miji 100,000 katika nchi 220.
Tunatathmini matangazo kwenye Airbnb kupitia uchanganuzi wa kiotomatiki wa kikompyuta ili kuchambua vichwa, maelezo yaliyoandikwa, tathmini za wageni, maelezo mafupi ya picha na takwimu nyinginezo.
Wanatimu wa upangaji wa Airbnb hutathmini matangazo na kuchagua kwa makini picha zilizoonyeshwa. Kisha kila aina hupitia tathmini ya mwisho ili kukagua uthabiti na ubora wa picha.
Watu wengi wanaenda safari ndefu kuliko hapo awali. Ili kuwapa machaguo mengi hata zaidi wanapopanga, tumeanzisha huduma ya Kukaa kwenye Nyumba Mbili, kipengele kipya cha ubunifu kinachogawanya safari kati ya nyumba mbili tofauti, sasa wageni wanaweza kupata wastani wa matangazo asilimia 40 zaidi wanapotafuta sehemu hizo za kukaa za muda mrefu.
Wageni wanapotafuta sehemu ya kukaa ya muda mrefu katika eneo moja, tutampa chaguo la kugawanya safari yake kati ya nyumba mbili tofauti katika eneo hilo.
Sehemu za Kukaa kwenye Nyumba Mbili pia hutolewa katika aina 14 tofauti, ikiwemo Kupiga Kambi, Hifadhi za Taifa, Kuteleza Mawimbini na kadhalika, ili wageni wafurahie nyumba zinazofanana au shughuli katika maeneo mawili. Kwa mfano, mgeni anayechunguza Aina ya Hifadhi za Taifa anaweza kupata sehemu ya Kukaa kwenye Nyumba Mbili inayopendekeza nyumba karibu na Zion na nyingine karibu na Grand Canyon.
Nyumba mbili zinapangwa kiweledi, zikilingana na eneo, aina ya nyumba na vistawishi.
Sehemu za Kukaa kwenye Nyumba Mbili zimeunganishwa kwenye ramani na michoro iliyohuishwa inayoonyesha wazi umbali kati ya nyumba hizo na mfuatano wa sehemu hizo za kukaa.
Mara baada ya mgeni kuchagua sehemu ya Kukaa kwenye Nyumba Mbili, anaongozwa kupitia mtiririko rahisi kutumia ili kuweka nafasi ya kila nyumba, moja baada ya nyingine.
AirCover ni ulinzi wa kina zaidi wa bila malipo katika tasnia ya usafiri nayo huwapa wageni wetu uhakika wa kujua kwamba ikiwa jambo litakwenda vibaya, tutawasaidia.
Katika tukio nadra ambapo Mwenyeji anahitaji kughairi nafasi uliyoweka ndani ya siku 30 baada ya kuingia, tutakutafutia nyumba sawa na hiyo au bora zaidi au tutakurejeshea fedha.
Ikiwa mgeni hawezi kuingia kwenye nyumba yake na Mwenyeji hawezi kutatua tatizo hilo, tutamtafutia nyumba sawa na hiyo au bora zaidi kwa muda wa ukaaji wake wa awali au tutamrejeshea fedha.
Ikiwa wakati wowote wakati wa ukaaji wa mgeni atagundua kwamba nyumba yake si kama ilivyotangazwa, kwa mfano, friji inaacha kufanya kazi na Mwenyeji hawezi kuirekebisha kwa urahisi au ina vyumba vichache vya kulala kuliko ilivyotangazwa, wageni watakuwa na siku tatu za kuripoti na tutawatafutia nyumba sawa na hiyo au bora zaidi au tutawarejeshea fedha.
Ikiwa mgeni atajihisi kwamba hayuko salama, atapata kipaumbele cha kuhudumiwa na maafisa wa usalama waliopata mafunzo mahususi, mchana au usiku.
Faida za AirCover ikilinganishwa na ulinzi kamili unaotolewa bila malipo na washindani wetu wakuu.
AirCover imeundwa moja kwa moja ndani ya programu na tovuti ya Airbnb na hivyo kufanya iwe rahisi kwa wageni kuwasiliana na wakala wakati wowote na kutatua matatizo haraka. Ili kutoa AirCover, tumeunda timu ya mawakala walio na mafunzo maalumu ili kutoa msaada wa kuweka nafasi tena dakika za mwisho na tumepania huduma yetu ya Mawasiliano ya Usalama Saa 24 ili itolewe kwa lugha nyingi zaidi kuliko hapo awali.