Airbnb 2021
Toleo la mwezi Novemba

Zaidi ya maboresho 50 ili kufanya Airbnb iwe bora zaidi

Tunawaletea AirCover

Ulinzi kamili. Bila malipo kwa kila Mwenyeji. Kwenye Airbnb pekee.

Ulinzi kamili. Bila malipo kwa kila Mwenyeji. Kwenye Airbnb pekee.

Bima ya dhima ya dola USD milioni 1

Unalindwa, hata katika hali nadra ya mgeni kuumia.

Ulinzi wa dola USD milioni 1 dhidi ya uharibifu

Tunagharimia uharibifu unaofanywa na wageni katika sehemu na mali zako, ikiwa ni pamoja na vitu vya thamani.

Ulinzi dhidi ya uharibifu wa wanyama

Usiwe na wasiwasi: uharibifu usiotarajiwa unaofanywa na mbwa na paka wageni pia unagharimiwa.

Ulinzi dhidi ya usafishaji wa kina

Tunakufidia kwa gharama zisizotarajiwa za kusafisha.

Ulinzi dhidi ya kupoteza mapato

Airbnb hufidia mapato yaliyopotea ikiwa utaghairi nafasi iliyowekwa na kuthibitishwa kwa sababu ya uharibifu.

Dirisha la siku 14 za kuripoti

Sasa una siku 14 za kuripoti uharibifu—hata ikiwa umeweka nafasi ya kukaribisha wageni mmoja baada ya mwingine.

Kurudishiwa pesa haraka

Wenyeji hurudishiwa pesa haraka ili kugharimia uharibifu wa wageni (siku 9 kwa wastani).

Kipaumbele kwa Wenyeji Bbingwa

Wenyeji bingwa hupewa kipaumbele katika kupata msaada.

Pata maelezo zaidi kuhusu AirCover na manufaa yake yote, pamoja na sheria na masharti, .

Uvumbuzi ambao utaupata kwenye Airbnb pekee

Translation Engine

Teknolojia bora zaidi ya tafsiri kuwahi kutolewa katika jumuiya yetu.

Ukaguzi wa ufikiaji

Huwa tunakagua kila kipengele cha ufikiaji kinachowasilishwa na Wenyeji wa sehemu za kukaa ili kuhakikisha ni sahihi kwa 100%.

WiFi imethibitishwa

Zana yetu mpya ya kujaribu kasi inawezesha wageni kuwa na hakika kuwa WiFi iliyo katika tangazo inakidhi mahitaji yao.

Ninaweza kubadilika (hata zaidi)

Tafuta hadi miezi 12 mapema, na ugundue aina zaidi za sehemu za kipekee za kukaa.

Kichupo mahiri cha Safari

Kichupo kilichosanifiwa upya cha Safari huweka maelezo yako yote ya lazima ya safari katika sehemu moja rahisi.

Upanuzi wa Muulize Mwenyeji Bingwa

Wenyeji wapya wanaweza kuunganishwa na Mwenyeji Bingwa ili wapate msaada wa ana kwa ana kutoka kwa mtu mzoefu.

Uzoefu wa wageni ambao ni mahiri na rahisi

Tafsiri ya papo hapo

Sasa huhitaji tena kubofya kitufe cha kutafsiri ili usome maudhui katika lugha yako.

Tafsiri bora

Tafsiri zilizoboreshwa kwa zaidi ya 99% ya matangazo kwenye Airbnb, hii ni kulingana na utafiti uliofanywa na shirika la nje.

Njia 62 za kusema “Karibu”

Kila tangazo na tathmini inapatikana mara moja katika lugha zote tunazotumia kutoa huduma kote duniani.

Vichujio vya utafutaji vilivyoboreshwa

Vichujio maarufu zaidi vya ufikiaji hufanya iwe rahisi kupata sehemu za kukaa kwa ajili ya mahitaji anuwai.

Ufikiaji katika Matukio

Vipengele kama “lugha ya ishara” au “hakuna ngazi” sasa vimeonyeshwa waziwazi kwenye Matukio.

Historia ya malipo ya wageni

Miamala ya wageni (kurejeshewa fedha, risiti, na zaidi) sasa inapatikana kwa urahisi.

Siku zilizosalia kabla ya kuingia

Kichupo mahiri, wasilianifu zaidi sasa kinaweza kuhesabu vizuri muda kabla ya kuwasili.

Maelezo muafaka ya kuingia

Maelezo yako ya kuingia sasa yanaonekana pamoja na maelezo yako ya kuweka nafasi.

Furahia kidokezo cha Matukio

Pata msukumo kutokana na video za kusisimua za Matukio karibu na unakoenda.

Aikoni mpya za ramani ya Matukio

Ramani inaangazia Matukio yaliyopangwa kulingana na aina, kama vile chakula, maeneo ya nje, na zaidi.

Mambo ya kufanya, kwa ajili yako tu

Tunakupendekezea Matukio bora kwako kulingana na watu ulio nao na mahali utakapokuwa.

Orodha ya matamanio pamoja na marafiki

Rafiki zako sasa wanaweza kuona Orodha yako ya matamanio kwa kubofya au kugusa mara moja tu, hakuna haja ya kuingia kwenye akaunti.

Kadi za zawadi sasa zimeboreshwa

Wape unaowaenzi zawadi ya safari mwaka huu ukitumia njia zaidi za kupata, kununua, na kutumia kadi za zawadi za Airbnb.

Kadi za zawadi ulimwenguni kote

Tuma shangwe kupitia kadi za zawadi za Airbnb, zinapatikana AU, CA, DE, FR, IT, SP na UK.

Utafutaji wa sera katika Kituo cha Msaada

Unatafuta sera mahususi? Pata unachohitaji kwa kutumia zana yetu ya utafutaji.

Kukaribisha wageni kulikorahisishwa

Uoanishaji wa Muulize Mwenyeji Bingwa

Tutakuunganisha na Mwenyeji Bingwa, kulingana na eneo lako, lugha yako, na tangazo lako.

Usaidizi wa wajuzi wa kukaribisha

Unahitaji jicho la pili kwenye tangazo lako? Pata vidokezo kutoka kwa Mwenyeji Bingwa kuhusu kile walichofanikisha.

Ulimwengu wa msaada wa Mwenyeji Bingwa

Habari! ¡Hola! Bonjour! Ungana na Mwenyeji Bingwa katika zaidi ya lugha 30 kwenye nchi 196.

Ni rahisi kuanza

Karibisha wageni wapya kwa hatua moja ukitumia mtiririko rahisi wa kuingia ndani kwenye kichupo cha Leo.

Nafasi kwenye kichupo cha Leo

Pitia na ujibu haraka uwekaji mpya wa nafasi bila kuondoka katika kichupo cha Leo.

Arifa katika kichupo cha Leo

Kichupo cha Leo sasa kinaonyesha tu arifa za Wenyeji, si arifa za wageni unazopata ukisafiri.

Vidokezo maalumu vya Leo

Pata vidokezo mahususi kwako kuhusu kukuza tangazo lako, kama vile kuongeza vistawishi vinavyopendwa na wageni.

Kichupo cha Leo kwa Wenyeji Weledi

Furaha kwa watumiaji weledi! Sasa unaweza kutumia kichupo cha Leo hata kama una matangazo mengi.

Nyenzo ya kupima kasi ya Wi-Fi

Wenyeji wanaweza kupima kwa urahisi kasi ya Wi-Fi ya tangazo lao katika programu ya Airbnb.

Uhakiki wa Bei kwa Wenyeji

Angalia bei ya tangazo lako jinsi linavyoonekana kwa wageni.

Ada ya usafi ya ukaaji wa muda mfupi

Chagua kuweka ada ya chini ya usafi kwa ukaaji wa usiku mmoja na usiku mbili.

Chaguo la ada ya wanyama vipenzi

Sasa unaweza kuchagua kuongeza ada ya wanyama vipenzi kwenye bei yako ya kila usiku.

Kurejesha fedha kwa ajili ya Matukio

Chagua kuwarudishia wageni fedha kamili ikiwa wataghairi hadi saa 24 mapema.

Mwongozo wa vipengele umeboreshwa

Mwongozo bora huwasaidia Wenyeji kuonyesha vipengele vyao vya ufikiaji kwa usahihi zaidi.

Upakiaji wa video umerahisishwa

Unataka kuunda mushtasari wa Tukio lako kwa video? Sasa ni rahisi kupakia klipu.

Tafuta kwenye Kikasha cha Mwenyeji kwa maandishi

Hakuna tena kusogeza bila mwisho: sasa ni rahisi kupata ujumbe na kwa kuweka maandishi kwa urahisi.

Kipakiaji picha kimeboreshwa

Kipangaji cha kiotomatiki sasa kinafanya kazi unapopakia picha moja baada ya nyingine.

Bei ya ofa ya tangazo jipya

Pigia debe tangazo lako jipya kwa punguzo maalumu kama sehemu ya mtiririko wa hatua 10.

Utafutaji ulioboreshwa

Matokeo ya utafutaji yaliyoboreshwa huonesha vizuri Wenyeji wenye ubora na thamani kubwa.

Mawasiliano ya Luxe

Ubawabu wa Luxe sasa unaweza kujumuisha wageni na Wenyeji katika mawasiliano ya pande tatu.

Onyesha upya kalenda ya kompyuta ya mezani

Kalenda ya Mwenyeji kwenye kompyuta ya mezani imepangiliwa ili iweze kuonekana vizuri unapotupia jicho na kurahisisha utumiaji.

Mapendeleo ya kalenda

Geuza taarifa inayoonyeshwa kwenye seli za tarehe iweze kukufaa zaidi (kompyuta ya mezani pekee).

Uboreshaji wa kuonyesha bei

Wenyeji sasa wanaweza kuangalia bei zao kwenye kalenda ikiwa na mwonekano wa mwaka mzima (kompyuta pekee).

Uchunguzi wa hatari umepanuliwa

Hatua za kupunguza shughuli za hafla kwa Wenyeji nchini Ureno na Uingereza.

Usuluhishaji umeboreshwa

Mchakato mpya wa usimamizi wa madai unawezesha usuluhishaji rahisi na wa haraka kwa Wenyeji.

Usaidizi Zaidi Kwenye Kitongoji

Nambari ya simu ya usaidizi wa dharura kwa ajili ya majirani wa Wenyeji imepanuliwa kuwa na lugha 12 katika nchi 29.

Kurejeshwa kwa tangazo

Matangazo yanaweza kurejeshwa tena katika Tovuti Unganishi ya Jiji baada ya Wenyeji kusasisha usajili wao.

Kutolewa kwa kipengele na upatikanaji wa huduma unaweza kutofautiana kulingana na eneo.