Airbnb 2021

Tunakuletea maboresho mapya zaidi ya 100 kwenye tovuti yetu

Airbnb 2021

Tunakuletea maboresho mapya zaidi ya 100 kwenye tovuti yetu

Urahisi wa kubadilika uliotengenezwa kwa kuzingatia hali mpya ya kusafiri

1. Mahali pa kuzuru panapoweza kubadilika

Njia mpya kwa wageni kugundua sehemu za kukaa za kipekee ambazo vinginevyo wangezikosa.

2. Uoanishaji unaoweza kubadilika

Inajumuisha matangazo ambayo yako nje ya utafutaji mahususi, ili kuonyesha wageni machaguo zaidi.

3. Tarehe zinazoweza kubadilika

Wageni sasa wanaweza kutafuta machaguo mapya, kuanzia safari ya wikendi hadi sehemu za kukaa za mwezi mmoja au zaidi.

Uzoefu wa mgeni ambao ni rahisi na unaohamasisha zaidi

4. Orodha za matamanio zilizopangwa

Mikusanyiko iliyoratibiwa ya maeneo ya kukaa yanayovutia pamoja na Matukio—yakiwemo Mandhari Bora ya Nje.

5. Mwongozo wa kuwasili

Taarifa ya kuwasili ambayo wageni wanahitaji, kuanzia kwa maelekezo hadi Wi-Fi, sasa iko katika mahali pamoja.

6. Mchakato wa haraka wa kutoka

Tumepunguza hatua zinazohitajika kwa ajili ya wageni wapya kuthibitisha nafasi ya kwanza wanayoweka.

7. Kujiunga papo hapo

Wageni wa mara ya kwanza sasa wanaweza kuunda akaunti ya Airbnb kwa urahisi wakati wa mchakato wa kwanza wa kuweka nafasi.

8. Upau wa kichujio

Vichujio maarufu sasa vinaonekana zaidi wakati wa kutafuta tangazo linalokufaa.

9. Menyu ya kichujio iliyosasishwa

Vigezo vipya na vilivyoboreshwa vya utafutaji ili kuongeza uwazi na urahisi wakati wa kutafuta.

10. Vichujio kulingana na msimu

Vichujio vinavyohusiana na muktadha husika vinaonekana wakati wa msimu—kwa mfano, malazi ya skii.

11. Vichujio ambavyo ni mahususi kulingana na eneo

Machaguo ya vichujio sasa yanaonekana tu ikiwa yanafaa kwa ajili ya mahali ambapo mgeni anapendelea kuenda.

12. Vistawishi vya kina

Maelezo mahususi zaidi ya vistawishi, kama vile ikiwa jiko linatumia gesi au kuni.

13. Sifa mpya

Mwonekano wa bahari? Baiskeli isiyosonga? Maelezo haya muhimu sasa yanatajwa kwenye matangazo.

14. Onyesha upya ramani kiotomatiki

Huweka matokeo ya utafutaji panapoonekana zaidi kwenye ramani wakati unavinjari.

15. Pini zinazonata

Pini za ramani hazipotei na kuonekana tena kinasibu wakati wa kuleta picha karibu au mbali na kusogeza kamera iliyokuwa kwa mkao wima. Safi!

16. Ikoni za ramani zilizoboreshwa

Picha ya ramani iliyoundwa upya inaonyesha vivutio maarufu na kadhalika wakati wa kutafuta.

17. Matukio ya Karibu

Ramani sasa inaonyesha mahali Matukio ya Airbnb yalipo kuhusiana na ukaaji wa mgeni.

18. Ramani za skrini nzima kwenye kompyuta ya mezani

Hapo awali zilipatikana tu kwenye simu ya mkononi, lakini sasa ramani za skrini nzima zinawezesha utafutaji mpana zaidi kwenye kompyuta ya mezani.

19. Urambazaji wa wageni

Menyu mpya ya wageni inatoa ufikiaji wa moja kwa moja kwa sehemu za kukaa, Matukio, kuwa Mwenyeji na kadhalika.

20. Vichujio vya ufikiaji

Vichujio vya utafutaji vilivyopangwa upya vinafanya iwe rahisi kupata sehemu za kukaa zilizo na vipengele vinavyohusiana na ufikiaji.

21. Zingatia ufikiaji

Ongezeko katika idadi ya sehemu za kukaa na Matukio kwenye Airbnb na vipengele vya ufikiaji.

22. Nyumba za kipekee zinazofikika

Nyumba zaidi za kipekee zilizo na vipengele vya ufikiaji ili kukidhi mahitaji ya jumuiya yetu.

23. Kichujio cha matukio

Kichujio kipya kinaruhusu wageni kutafuta shughuli za ana kwa ana zilizo na vipengele vya ufikiaji.

24. Matukio mapya jumuishi

Shughuli za mtandaoni na za ana kwa ana zilizobuniwa kujumuisha jumuiya ya walemavu.

25. Bei ya watunzaji

Wenyeji wa Matukio wanaweza kutoa bei ya bila malipo kwa watunzaji wanaowasaidia wageni wenye ulemavu.

26. Mandhari ya Nje ya Kuvutia

Sehemu za kukaa na Matukio ambayo yanaongoza safari yako kwenye mazingira ya asili.

27. Kushiriki Matamanio yaliyopangwa

Shiriki Matamanio ya Airbnb unayopenda pamoja na marafiki, familia na wafuasi kwenye mitandao ya kijamii.

28. Kughairi wazi zaidi

Sera za kughairi zimebadilishwa ili kuongeza uwazi kwa wageni na Wenyeji.

29. Mawazo ya kupanga safari

Wakati wa kupanga ukaaji, Matukio yanayofaa yanapendekezwa kwa wageni.

30. Mambo ya kufanya

Kichupo cha Safari sasa kinapendekeza shughuli nzuri, za karibu ukiwa safarini.

31. Mapendekezo ya wenyeji

Wenyeji wanaweza kutuma ujumbe kwa wageni wa sasa ulio na Matukio yaliyopendekezwa ya eneo jirani wakati wa ukaaji wao.

32. Leseni za matukio

Husaidia kuhakikisha kuwa leseni ya Mwenyeji na taarifa ya bima imesasishwa kwa ajili ya Matukio kama vile michezo ya kuendesha boti.

33. Maelezo ya matukio

Wenyeji wa Matukio sasa wanaweza kurekebisha maelezo ya tangazo ili kuhakiki usahihi.

34. Ufikiaji rahisi wa timu

Ni rahisi zaidi kuliko hapo awali kwa wafanyakazi wenza kudai viti vyao kwenye kundi la Matukio ya Mtandaoni.

35. Wenyeji wa Matukio ya Mtandaoni

Jumuiya ya Wenyeji iliyotengwa kimahususi kwa ajili ya familia yetu inayokua ya Wenyeji wa Matukio ya Mtandaoni.

36. Bei inayofaa familia

Wenyeji wa Matukio sasa wanaweza kutoa mapunguzo ili iwe rahisi kwa familia zaidi kushiriki.

37. Vipengele vya nyumba za kipekee

Vipengele 9 vipya vya nyumba za kipekee zinazoweza kuchaguliwa vimeongezwa—kuanzia nyumba zilizojengwa kwa matofali na udongo hadi mabehewa.

38. Nyumba za kipekee katika mazingira ya asili

Kipengele kipya cha sehemu za kukaa za kipekee zinazopatikana katika mazingira ya asili—kuanzia mahema angavu yanayopuliziwa upepo hadi ranchi zenye mifugo.

39. Sehemu za kukaa karibu na vivutio

Wageni wanaweza kupata sehemu za kukaa karibu na maporomoko ya maji au kiwanda cha mvinyo.

Njia rahisi za kukaribisha wageni—kuanzia kujisajili hadi kuwa Mwenyeji Bingwa

40. Karibu kwenye ukurasa wa kukaribisha wageni

Kituo kilichobuniwa upya ili kukidhi vizuri mahitaji ya Wenyeji wapya wanapoanza safari.

41. Kuwa Mwenyeji katika hatua 10

Sasa ni rahisi zaidi kutangaza sehemu yako kwenye Airbnb na upate msaada unapofanya hivyo.

42. Kichupo cha Leo

Njia mpya ya Wenyeji kusimamia kwa urahisi nafasi zilizowekwa, kazi na zaidi katika sehemu moja.

43. Nyenzo za Mwenyeji wa Matukio

Ukurasa wa "Kuwa Mwenyeji" uliobadilishwa una sehemu mpya na nyenzo kwa ajili ya Wenyeji wa Matukio.

44. Ushuhuda wa Wenyeji

Maktaba ya makala muhimu na video za kuhamasisha Wenyeji wapya na waliopo.

45. Eneo langu lina thamani gani?

Kikokotozi kilichofanyiwa mabadiliko hukusaidia kukadiria haraka mapato ya sehemu yako.

46. Andaa Matukio kwa urahisi

Mchakato ulioboreshwa wa kutoa mafunzo unatoa njia rahisi ya kuwa Mwenyeji wa Matukio.

47. Video kwa ajili ya Matukio

Wenyeji wengi wa Matukio sasa wanaweza kupakia video kwa urahisi ili kuonyesha shauku yao ya pamoja.

48. Maelezo yaliyojazwa kiotomatiki

Maelezo ya nyumba kutoka kwenye data ya umma huwasaidia Wenyeji kuweka tangazo haraka.

49. Weka vistawishi kwa urahisi

Ikoni zilizohuishwa hufanya iwe rahisi kuchagua na kuonyesha vipengele muhimu vya tangazo.

50. Kupanga picha kiotomatiki

Modeli za hali ya juu za mwonekano za kompyuta zinachambua picha na kuzipanga upya kwa ajili ya mpangilio mzuri.

51. Kichwa kilichopendekezwa

Pendekezo la maandishi la kiotomatiki kwa ajili ya kuunda kichwa cha tangazo chenye kuvutia kulingana na taarifa iliyotolewa.

52. Kuanza kwa ufafanuzi

Inawasaidia Wenyeji wapya waeleze kwa haraka sifa za kipekee na za kutamanika za tangazo lao.

53. Upangaji rahisi wa bei

Kuweka bei inayofaa kwa ajili ya tangazo lako sasa ni wazi na rahisi.

54. Kiwango cha bei kilichopendekezwa

Sasa tunatoa kiwango cha bei kinachokadiriwa kwa ajili ya sehemu yako kulingana na matangazo yanayofanana na lako.

55. Shukrani

Tumeboresha na kurahisisha hatua za mwisho mwishoni mwa mchakato wa kuweka tangazo.

56. Hakiki kabla ya kutangaza

Pata hakiki ya jinsi tangazo lako jipya litaonekana kwa wageni kabla ya kuchapishwa. Hatimaye!

57. Ukaribisho wa tangazo jipya

Unapomaliza tangazo lako jipya, Sandy na Brian watakuwepo kusherehekea.

58. Mwongozo wa Mwenyeji mpya

Makala yanawasaidia Wenyeji wapya wakati wote wa mchakato wa kuanza kukaribisha wageni.

59. Utangulizi wa madarasa ya kukaribisha wageni

Mafunzo yatolewayo na Wenyeji Bingwa huwasaidia Wenyeji wapya waelewe mapema.

60. 1:1 ushauri

Wenyeji wapya wanaofanya mafunzo ya mtandaoni wanaweza kusaidiwa na Wenyeji Bingwa.

61. Muulize Mwenyeji Bingwa

Wakati wa kuweka tangazo, Wenyeji wapya wanaweza kushauriwa na Mwenyeji Bingwa.

62. Vidokezi vya kukaribisha wageni

Wenyeji wa Matukio ya Mtandaoni watajifunza vidokezi kutoka kwa Wenyeji wenye uzoefu.

63. Jitayarishe kwa ajili ya mgeni wako wa kwanza

Baada ya kutangaza sehemu mpya, mwongozo hutolewa kuhusu hatua zinazofuata—kama vile kuweka sheria za nyumba.

64. Kalenda mahususi na bei

Wenyeji wapya wanapewa vidokezi kuhusu jinsi ya kuwekewa nafasi wanazotaka kwa bei wanayotarajia.

65. Thibitisha jinsi wageni wanavyoweka nafasi

Wenyeji wanaweza kuweka matakwa kwa ajili ya wageni wanaoweka nafasi, kama vile mapendekezo kutoka kwa Wenyeji wengine.

66. Chagua jinsi utakavyolipwa

Arifa ya kiotomatiki inawakumbusha Wenyeji wapya kuweka njia ya kupokea malipo, ili waweze kulipwa bila kukawia.

67. Maombi ya kuweka nafasi

Kichupo kipya cha Leo kinaruhusu Wenyeji kutazama kwa urahisi maombi yoyote yanayosubiri ya kuweka nafasi na maulizo.

68. Nafasi ulizoweka

Kichupo cha Leo pia kinaruhusu Wenyeji kutazama nafasi za wageni zilizowekwa ambazo zipo na zinazosubiri kwa kutupia jicho.

69. Viunganishi vya haraka

Kichupo cha Leo kinatoa njia rahisi kwa Wenyeji kupata nyenzo za kupanga bei na upatikanaji.

70. Habari na masasisho kwa Wenyeji

Makala katika kichupo cha Leo hushauri kuhusu mikakati ya kufanikiwa kukaribisha wageni.

71. Arifa za mwenyeji

Arifa zinasaidia kuhakikisha kuwa Wenyeji wanakumbushwa kuhusu chochote kinachohitaji umakini wao.

72. Kutuma ujumbe kwa haraka

Ujumbe kati ya wageni na Wenyeji sasa unapakia kwa kasi ya hadi mara 10 zaidi.

73. Utafutaji wa kikasha

Inaruhusu Wenyeji kupata ujumbe kwenye kikasha chao kwa urahisi kwa kutumia vigezo anuwai vya utafutaji.

74. Vichujio vipya vya kikasha

Mabadiliko kwenye kikasha yanawezesha Wenyeji kuchuja ujumbe haraka—pamoja na ule ambao haujasomwa.

75. Majibu ya Haraka Mahususi

Wenyeji wanaweza kutumia Majibu ya Haraka kwa maswali ya wageni yanayoulizwa sana.

76. Ujumbe ulioratibiwa

Unda ujumbe ambao unatuma makumbusho ya kirafiki kiotomatiki, kama vile maelekezo ya kutoka.

77. Vidokezi vya kukaribisha wageni

Kichupo cha Vidokezi huelezea mienendo ya eneo husika ili kuwanufaisha Wenyeji.

78. Maarifa kwa ajili ya Matukio

Zana iliyosasishwa kwa ajili ya Wenyeji wa Matukio yenye na data kuhusu mapato na ukadiriaji.

79. Mtiririko wa tathmini ulioboreshwa

Njia rahisi kwa wageni kuwasilisha tathmini ambazo zinawapa Wenyeji maoni muhimu.

80. Maoni ya kina

Vidokezi vya maoni huwakumbusha wageni kuwapatia Wenyeji tathmini za maana.

81. Vipengele zaidi vya maoni

Vipengele vipya katika mtiririko wa tathmini huwasaidia wageni kuelezea ukaaji wao.

82. Tathmini zilizosasishwa

Wageni sasa wana wigo kamili, kuanzia kukosolewa hadi kusifiwa, ili kukadiria ukaaji wao!

83. Mafanikio ya maisha ya Mwenyeji

Metriki mpya husherehekea kila kitu kuanzia jumla ya wageni waliokaribishwa hadi vitu ambavyo walifurahia zaidi.

84. Vidokezi vya kukaribisha wageni vinavyoweza kushirikiwa

Njia mpya ya Wenyeji kushiriki na kusherehekea metriki za utendaji wa maisha kupitia mitandao ya kijamii.

85. Maelezo ya mwenyeji

Maelezo ya tangazo sasa yanaangazia upekee wa kila Mwenyeji na nyumba yake.

Usaidizi wa kiwango cha kimataifa kwa ajili ya jumuiya yetu ya kimataifa

86. Kituo cha Msaada kilichobuniwa upya

Njia rahisi ya kuvinjari Kituo cha Msaada na usaidizi kamili kwa ajili ya wageni na Wenyeji.

87. Masuluhisho janja

Mwongozo uliofanywa mahususi unawasaidia wageni na Wenyeji kutatua matatizo ya kawaida kwa urahisi katika hatua chache.

88. Arifa za malipo

Arifa zote za malipo ya wageni sasa ziko katika eneo moja ambalo ni rahisi kupata.

89. Nyenzo za usalama zilizosasishwa

Usaidizi safarini una simu ya usaidizi ya sekunde 30 ikiwa na tafsiri katika lugha nyingi.

90. Taarifa ya dharura ya eneo husika

Taarifa ya huduma ya dharura ya eneo husika kwa ajili ya moto, polisi na EMT katika maeneo mengi.

91. Upanuzi wa usaidizi wa haraka

Usaidizi wa haraka ukiwa safarini sasa unatolewa kwa mamia ya lugha.

92. Simu mahususi ya Wenyeji Bingwa

Usaidizi ulioboreshwa kwa Wenyeji Bingwa—Amerika Kaskazini kwanza, kisha kimataifa.

93. Usaidizi wa Kiongozi wa Jumuiya

Usaidizi mpya kabisa wa kipaumbele kwa ajili ya Viongozi wa Jumuiya yetu ya Wenyeji.

94. Msaada ukiwa safarini

Njia bora ya kusaidia wageni na Wenyeji wakati wa safari yao kwa kuwapa taarifa muhimu zaidi.

95. Utafutaji wa jumla

Tafuta kwa wakati mmoja kwenye bidhaa zote za usaidizi za Airbnb ili upate majibu haraka.

96. Usaidizi ng'amuzi zaidi

Makala rahisi za usaidizi hutoa taarifa sahihi—mahali na wakati zinapohitajika.

97. Mwongozo wa usuluhishi

Msaada wa hatua kwa hatua unaotatua matatizo ya kawaida ukiwa safarini kama vile vistawishi vilivyovunjika au vinavyokosekana.

98. Kituo cha sera ya jumuiya

Sera za kueleweka na rahisi zaidi zipo katika eneo moja ndani ya Kituo cha Msaada.

99. Zana mpya za Tovuti-unganishi ya Jiji

Zana mpya za kuwasaidia maofisa wa jiji kusimamia taratibu za upangishaji wa muda mfupi.

100. Tathmini habari za mizozo

Sera mpya inayoruhusu Wenyeji kupinga tathmini zilizoachwa na wageni wanaokiuka marufuku ya sherehe.

101. Wakala zaidi wa usaidizi

Tumeongeza mara 2 idadi ya wafanyakazi wetu wa usaidizi wa kimataifa ili kuboresha huduma.

102. Usaidizi katika lugha zaidi

Tumepanua wigo wetu wa usaidizi kutoka lugha 11 hadi 42.

103. Nyenzo za mwenyeji

Menyu mpya ya Mwenyeji hufanya ufikie moja kwa moja usaidizi, matangazo, na zaidi.

Kutolewa kwa kipengele na upatikanaji wa huduma unaweza kutofautiana kulingana na eneo.